Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Hii nilisimuliwa na Anko wangu Arusha.
....
Kulitokea msiba wa ndugu yao akina anko, maiti ikaletwa ili wazike wakaweka ndani ili kujiandaa baadae mazishi. Baadae wamezika wamemaliza muda wakaona gari lile lililoleta maiti limeleta maiti tena. Ajabu zaidi ilileta maiti ile ile iliyozikwa na watu waliokuja mara ya kwanza ndio wale wale wamerudi na maiti iliyozikwa.

Anakwambia watu walitoka mbio ussein bolt cha mtoto...
 
Ni kweli,mzaliwa wa kwanza Ni lango.

Ila wachawi wajinga sana aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu funguka kidogo,umetuacha na maswali mengi sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mwalimu alipangwa kufundisha somo la biology katika shule x Mpanda. Katika darasa alilokuwa anafundisha kulikuwa na mtoto mmoja ambaye alikuwa anafanya walimu waonekane wakiwa uchi wa mnyama wakati wanafundisha darasani kwa kutumia uchawi. Yaani mwalimu anapoingia tu kwenye darasa hilo, huyo mwanafunzi anayafanya mambo yake mwalimu anaonekana akifundisha uchi kwa wanafunzi wote darasani.Walimu walifahamu hili baada ya kuwa wanaona wanafunzi wanacheka sana wakati wote wakiwa darasani ndipo baada ya kudodosa sana mwanafunzi mmoja akamwambia kuwa huwa wanaona wakifundisha uchi wakienda darasani. Toka siku hiyo walimu wakagoma kufundisha darasa hilo mpaka afisa elimu alipokuja kukemea vitendo hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa kingine....

Kuna mwalimu alimchapa mwanafunzi kwenye shule moja huko Shinyanga. Mwanafunzi akakimbia akilia mpaka nyumbani kwao. Akarudi akiwa ameshikilia kitu kimefungwa kwenye kitambaa chekundu akawa anamtafuta huyo mwalimu ampige nacho. Mwalimu alipoambiwa alikimbia na hakuwahi kurudi shuleni hapo tena na vitu vyake hata hakurudi kuvichukua.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufika ukauziwa musukule wa kulimia ina maana na wewe ni mshirikina,je huko mwanza gamboshi iko wilaya gani, wanapokuwa wamalima hao musukule wewe wawaona live au unapeleka order then unakuta shamba limelimwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Msukule hautumiwi na mshirikina peke yake Mkuu,Mimi nilinunua Mara moja nikashindwa masharti nikamrudisha,so nikawa nalipa fedha kwa Mshirika(Mchawi) Nampa na eneo nalolitaka kufanyiwa kazi na si kilimo pekee kazi nyingi wanafanya tofaut na ulimaji.

Hapana Mimi si mshirikina mteja wao tu kwa wakati huo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 


Wenyewe walisurrender wakasema mtoto atawatafuta mwenyewe badae akikua dogo nae adai kammisi mumewe na muda mwingin ananitoroka anaenda badae anarudi tehteh. .anasema as long as mumewe hasapoti uchawi mungu atawatetea

Ila sisi kama ndugu sasa ndio hatuelewi tunataka waachane kwani familia nzito ile

Cc Smart911
 
Wasiachane..
Kama mume Yuko vizuri basi haina haja ya kuachana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


kweli hata huyo houseg wangu alisema. .kuna kazi mbali mbali wanapewa kama yeye kazi yake ilikua jikoni na kutumwa kuua tu. . kuna wengine wanalima ndani ya mda mchache wanamaliza eti pia kuna siku za kusherekea tu hio siku wanaimba wanakula wanafurahiii. .lakini pia alisema kule hawawi na maumbo ya kibinadamu bali wanakua na maumbo ya wanyama au ndege wengine ng'ombe kuku n.k sasa Sijui inakuaje hapo

pia yule binti aliyeletwa kanisani baada ya kuonekana kwa miaka 5 kupita alikua anakula kwa mkono ila kama ndege au kuku yani kama anadonoa vile iwe wali iwe ugali
sijui inakuaje hapo

Cc Smart911
 


kweli hata huyo houseg wangu alisema. .kuna kazi mbali mbali wanapewa kama yeye kazi yake ilikua jikoni na kutumwa kuua tu. .eti pia kuna siku za kusherekea tu hio siku wanaimba wanakula wanafurahiii. .lakini pia alisema kule hawawi na maumbo ya kibinadamu bali wanakua na maumbo ya wanyama au ndege wengine ng'ombe kuku n.k sasa Sijui inakuaje hapo

pia yule binti aliyeletwa kanisani baada ya kuonekana kwa miaka 5 kupita alikua anakula kwa mkono ila kama ndege au kuku yani kama anadonoa vile iwe wali iwe ugali
sijui inakuaje hapo

Cc Smart911
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…