Ndio kuanza kukemea sasa mimi na hao watoto hadi wa la pili masikini yupo tu toka kwa jina la yesuuu ..nikawa nawambia watoto wengine waendelee kuimba nyimbo za kuabudu huku wakubwa tunakemea kemea kemea badae tukaona yule binti akiwa bado yupo kwenye hali ya kupandwa na mapepo akawa anamnyooshea kidole Kachanga akiwa ameshikwa nahuyo wa form 3 huku anacheka sauti kubwaaa anamnyooshea huku anacheka ha ha ha Haa hapo watoto mbioooo nyuma yangu nawambia hii ni vita msiache kuimba na kusali pia msiogope mnaona Mungu ametuonesha vitu tulikua hatuvijui siku zote tulikua tunaishi nae dada wa kazi bila kujua haya yote.
Baada ya kuona hivo ananyooshea Kachanga na kusema shangazi unaona umeniponza sasa shangazi umeniponza nikaanza kumemea huku namuamuru aseme yeye ninani. . na anataka nini akawa kafumba mdomo kwa nguvu namuamuru aseme wapiiiiii. .amuru wapiiiiii. .Badae akasema tu ametumwa na shangazi yake Kachanga huku akitaja jina lake halisi ( dada wa mume wa dogo ) .tukaendelea kukemea badae akawa anasema ana njaa na amechoka anaomba chakula na maji ( sasa nikawaza njaa imetoka wapi wakati tulikula kabla ya kuanza maombi? ? kumbe pale hakuwa katika hali ya kibinadamu bali alikua na hali ya kishetani / kichawi ambayo walimpa kazi hio ya kuja kuua Kachanga usiku huo ambao tulikesha kwenye maombi ila ndio akakutana na moto wa yesu maombi makali na songombingo hizo na kuishiwa nguvu hivo kudondoka )
kwahiyo ile njaa na kiu ni kutokana na nguvu ya mungu iliyokua ikifanya kazi hivo aliishiwa nguvu. na mtu wa hivo au pepo ukimpa maji au chakula tu unamuongezea nguvu upyaa .. hatukumpa chochote na baadae aliishiwa nguvu kabisa akawa kama anasota kuelekea ukutani kwenye kona ya sebule na kisha kushtuka kama mtu aliyekuwa usingizini akiwa na akili ya kibinadamu huku akitushangaa na kulalamika mbona a najisikia amechoka sana viungo vyote ??
hapo saa 11 asubuhi nikawaambia wote tulale. .tulilala hapohapo sebuleni tulitoa magodoro ila watoto walikuwa wanamkimbia na kumuogopa sana houseg hata kama yupo kwenye hali ya kawaida ya kibinadamu wakimuona mbioooo.
kesho yake Nikamwambia twende kanisani tukaenda.
Huko sasa alikuwa na mapepo kama 7000 hivi. .kumbe huyo houseg nae kwao ni wachawi. .wale wachawi nuksiiii walimuombea akasema yoooote aliyowafanyia . .( aliweka dawa na hirizi chini ya kitanda anacholala mama na mtoto kilasiku , aliwalisha dawa kwenye chakula nyingine alimuwekea kachanga kwenye kiganja cha mkono wa Kushoto usiku kiuchawi -hii usiku huo alikuja kuelekezwa na shangazi mtoto wakamuwekea mtoto ili atakapotimiza mwezi mmoja kamili waje kumchukua kiuchawi kwa urahisi )watu aliowaua watano Kachanga alikua wa 6 ila ameshindwa. .ilichukua wiki nzima akiwa kanisani huko huko alikua na madude mengi sana. .ambayo wakati anaombewa kila mmoja alikuwa anaongea sasa upande wa kwao binti na shangazi Kachanga. ..
yaliyotushangaza ni ya wifi mtu upande wa ukweni kwa dogo huko aliyetaka kumuua kwa kumchukua kiuchawi mtoto wa kaka yake kwakua kaka yake huyo ( baba Kachanga )alikataa kushirikiana nao katika mambo yao ( ya kichawi )
Muda mrefu sana walimwambia kuungana nao lakini alionekana kutovipenda / kuchukia hayo mambo ya kichawi na hataki hata kuvisikia wakati kwao ukoo ulimchagua na kumuona yeye ndiye mwenye nyota na anafaa kuwaongoza lakini alikataa hivo watawasumbua mke na watoto wake ..
pia sababu nyingine ni kwakua Kachanga alikua mtoto wa kwanza ..wachawi wanaita watoto wa kwanza nikama lango sijui lango la wapi hata ndiomana huenda kuchukua watoto wakwanza..... pia mtoto huyo Ana nguvu sana lakini pia watoto na vijana wa kiume wanapendwa na wachawi kwakua wana nguvu nyingi tofauti na wanawake hivo husaidia kazi nyingi huko kuzimu pia husaidia kunyanyua wazee wasio na nguvu huku kuzimu hivo angemchukua Kachanga angemlea mpaka angetimiza miaka 13 au 14 ( sikumbuki vizuri )angeanza kumtumia
itaendelea
Cc
Smart911