Kisa 06
Daah kipindi hicho life limenipiga tuko pori mkoa Fulani tunachoma mkaa hapo ni mda kidogo baada ya kumaliza chuo mambo tuliyokutana nayo huku ni balaa
Kwanza kabla ya kuingia porini kuna nyumba tulifikia ya mzee anaishi peke ake ya udongo iko mbali na makazi pia alitupa info kuhusu hilo pori maana sisi ni wachomaji holela bila kibari akatuambia ili moshi usionekane au msishtukiwe nendeni mbali kidogo zamani ndan sana
siku tatu za mwanzo tulikuwa kila tukilala tuseme tuamke usiku mwingi tuchome mkaa tunaamka saa saba za mchana sio zahidi ya hapo mpaka tunajishangaa
Tulikuwa tukisikia sauti za manukato kwa mbali zile za gharama na sometimes harufu za misosi mizur lakini cha kujiuliza kule tulipo ni pori la mbali kuna kabaridi ukungu na kagiza kidogo maana hata miale ya jua inachomoza kidogo kwenye miti jinsi ilivyojitandaza huyu mtu ni nani hivi kweli kuna mtu anaishi humu ?
Katika pitapita zangu kuokota vikuni kidogo kwa ajili ya kuandaa ka ugali ketu jion kabla ya kuanza kazi za uchomaji niliziona nyayo moja nyengine moja kama vile aliepita na mguu mmoja halafu ina vidole virefu vitatu moja imepita kwenye matope imegandana nikaonyesha wadau wakasema atakuwa ni mnyama hapa hadi Leo nashindwa kuamini
Kuna mwenzetu alitoka mbio kutoka mtoni alipokuwa akioga akadai kwamba aliona mda ana nywele ndefu amekaa kwenye mawe ya mtoni japo hatukumuamini maana alikuwa anatumia viroba
Tulikuwa kumi na mbili na tulijipanga kwelikweli kuvuna hiyo mikaa kiholela tulienda mpaka na gunia la dagaa na unga tulikaa sana huko lakini kwa kipindi cha interval kama siku nne au tano hivi tunapungua mfano mmelala kumi na mbili mnaamka kumi na moja mmoja hayupo baada ya wiki kupita ni hivohivo tunapungua tulikuwa tunajua labda kazi imewashinda wamekimbia
Kila tukilala usiku kama vitu tumevipanga tunakuta vimevurugika magunia tuliyoyafunga na kuyapaki vizuri yameangushwa hovyo pamoja na kuskia vicheko kama cha mwanamke kila saa saba ya usiku hilo hatukulipatiliza
Kuna siku tunatafuta uyoga au mboga yeyote hapo porini wakati huo dagaa zimekata tukakutana na mdada mrefu ametuzidi sio sana anapita tulimsalimia tu lakini hatukujua anapoenda wala anapotoka na alijipamba kweli tulilipotezea hilo kwa sababu tulijua pengine kuna watu humu japo haingii akilini au labda ni tourist anafanya forest walk ila tulipotezea
Usiku watu wakilala kesho mmoja anaamka anasema Jana usiku nilikuwa nikiskia kama mtu ananiita tena baba yangu tukajua hzi ni bangi tu maana hilo kundi la mabaharia kulikuwa na walevi ila Mimi nilikuwa situmii chochote kile sio mlevi ila siku moja nimelala usiku nikaskia naitwa jina kabisa M amka njoo basi M amka basi uje uku chini karibia na mto na ni kweli nilikuwa naskia vishindo wenzangu wako fofo ni sauti ya thureiya wangu sasa nikawa najiuliza huyu bi Dada nimemuacha dar sijamwambia nilipo na ananitafuta kweli kweli huku amefikaje usiku huu nikaamua ni mute tu nilale tu hapo nikawaamin washkaj nikawaambia asubuhi
jion tukikaa tumepumzika kwa mbali tunaona kama kuna mtu mrefu anatembea anapotelea kusikojulikana kulala usiku kujikuta umelala juu ya mti wenzangu Mara ya kwanza wakasema hio ni sleep walking ilipo wakuta hawakuamini maana mmoja alishtuka yupo amelala juu ya jiwe mtoni na tulikuwa fofo hatujui aliendaje ye mwenyewe ajui maana kama angekanyaga maji apande kwenye mawe angeshtuka
Kulala usiku kupapaswa ikawa inatutokea sana tukasema tuwe tunalala kwa kubanana kama ndizi kwenye mkungu
Siku hiyo hali ikazidi kuwa mbaya tumebaki wanne sasa wengine hatujui walipo tukasema potelea pote tukaanza kuondoka ilo eneo hiyo ni baada ya wenzetu kuanza kupotea kwa kasi unaamka asubuhi mnakuta mko wachache tukasema haya magunia potelea pote tukaanza kusepa tumetembea weeh ila kila tukizunguka tunarudi palepale
Zunguka wee almost masaa nane tunarudi palepale akili ikatujia ghafla tuufatilie mto kweli tukafanikiwa kutoka lile eneo tukatokeza sehemu kuna kamti mvua inanyesha tukajihifadhi hapo basi mvua ikakata akatokea mmoja kati ya watu waliopotea tuliokuwa nao akasema nyie maboya mnafanya nini hapa twendeni tukabebe ule mkaa mnamuachia nani kwanza mmoja wetu akamtukana nyie wasenge mlikuwa wapi mnatutisha hvyo jamaa akacheka akasema tulienda kijiji jirani kuchukua baskeli za kubebea hayo magunia turudini basi na tumepata kenta ambayo inakibali tumeelewana nae bei akataja mzgo mkubwa kweli
Washkaji wakasema turudini wale watatu niliokuwa nao mi nikasema hapana mtanikuta huko mbele nikawaambia tuachane nae je walivyotukimbia huu si uboya na kututia wasiwasi jamaa akasema we ukienda ukizulumiwa utajua mwenyewe una uhakika kama tutapitia huko mi moyo ukawa unakataa nikakumbuka ka msemo kangu "trust your instinct" nikasema potelea pote mtanikuta mbeleni na changu mtanipa basi tulikuwa wanne mmoja wetu akatukacha akasema hawa kama wametukacha mwanzo wanaweza kimbia na chetu nyie kama hamtaki kurudi shaur yenu jamaa akageuza na yule tuliokutana nae wawili wakakubaliana na Mimi tukaendelea na safari
Tumefika mbele huko tukapumzika asubuhi mwendo tukakutana na mwengine alietoweka oyaa nimetumwa niwacheki hatupiti uko halafu mizego yetu unamwachia nani halafu usipolipwa utamlaumu nani mi nimetoka huko unapoelekea kuna ka kijiji sisi hatufiki huko nimeenda kuulizia usafiri huko magari yenyewe yanazingua mmoja niliekuwa nae katika wale wawili akaniambia niache ujinga yule jamaa Mara ya kwanza alituambaia tukakataa yani kwa kazi niliyoifanya kukesha usiku kuchoma mkaa huo uboya siufanyi wakaguze mi nikasema sirudi tena tukabaki na mmoja ambae alikuwa ni dogo tu kamaliza form 4 alizingua aliamua ajiunge kwenye hizi shughuli ye alitokea kunielewa pale porini na alikuwa rfk tu nilikuwa namshaur ile kazi asiirudie tena atafute mbadala ye kwakua alinizoea akaungana na Mimi tukaendelea na mwendo
Tumefika saa sita hivi kwenye barabara kuu mchana hapo njaa inauma siopoa yakawa yanapita magari kila tukiomba lifti pemben ya barabara haya simami hapo no wachafu kichizi kwa bahat nzur moja likasimama mbaba Fulani hivi akatupakiza akawa anatushangaa kweli akawa anatuhoji mnatoka wapi ?tukamuhadithia hakutuamini akasema huo msitu ulivyo mnawezaje kuingia humo ndani kwanza hii njia yenyewe usiku sometimes ina kuwa na mauzauza hata mchana hapo ndo nkapata wazo kweli kwa ile hali tuliyonayo ndo maana wakawa magari yanakataa kusimama tulitembea na gari almost maa mawili ndo tukafika kijiji jirani mji Fulani x
Hapo ndo nikawa najiuliza yule mwenzetu alietuambia anatoka huku tunapoelekea aliwezaje kutembea kupaona na pia hapo kwenye maji tuliuliza kama kuna mtu kavaa hivi na hivi na hivi kaja kuuliza kama kuna kenta itaweza beba mizigo wake kwa madereva wa kenta pale ambao wataukuta barabarani wakasema hapana tukaa huo mji siku mbili tukarudi kule mji wa mwanzo kupitia barabara rasmi ule ambao tulitumia kuingilia porini kwa maana tulikatiza ktk ya pori tukatokea sehemu nyingine
Tukaenda kwa yule mzee kuuliza kama wenzangu walirudi walipitia pale hili nyumba ya yule mzee sikuikuta nilimuuliza dereva tulioelewana nae Mara ya kwanza kabisa ambae kenta yake inakibali kama majamaa walirudi akasema hapana kwanza alidhani tumepata mtu mwengine kuna mmoja nilikuwa namjua namuonaga maskani ktk hao tulioenda pale maskani hawajamuona na hawajamsikia ktambo sana hata mke wake alishatoa taarifa polisi nikasema huu mji ngoja nichomoke nisije nikawa kama suspect maana watajua aliondoka na Mimi na kwa nini turudi wawili kwakua dogo ni mzaliwa wa pale nikamuaga nikasepa
Japo naskia baadae walipeleleza wakajua tulienda choma mkaa dogo alibanwa kweli polisi walimchomoa darasani alikuwa veta walifanya kuwatafuta lakini wapi
Cha kujiuliza je uchawi upo au hawa majamaa walinifanyia usanii wakasepa na magunia ya mikaa niliotoa jasho langu kuchoma wote ?
Lakini mbona magunia polisi waliyakuta ? Hawa watu wako wapi kipi kimewakuta ? Nimeshindwa kujua jibu mpaka Leo na mke wa jamaa amekataa kuweka matanga anaamin mumewe atarud ni mda sana sasa sjui kilochoendelea
Sent using
Jamii Forums mobile app
Cha mwisho yule mzee tuliomkuta mwanzon kabisa kabla ya kuingia porini tulielezea watu kuhusu yeye wakasema hakuna nyumba ukivuka hapa tena wala mzee yeyote hata wakataji mbao na wachomaji mkaa wanasema tunapita kila siku ilo eneo halina nyumba wala mzee ni miti tu na ni kweli tulirudi hatukuona dalili kuwepo kwa nyumba uliyovunjwa kama ingekuwepo