Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kwanini Gambosh iwe mysterious place wakati ni eneo lipo kama maeneo mengine?

Mambo yake yapi?

Kwanini uyaweke siri?

Nyani Nyabu ana habari gani hizo ambazo mnazijua? Bila shaka na wewe unaabudu mysterious things za Gamboshi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kabisa, weka ushahidi kwamba Gambosh ni mysterious.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
wachawi noma,unaweza kuta wewe ni mrembo sana,ukaliwa kimasihara kichawi na mwanaume mbaya kuliko wanaume wote,tena mzee halafu kikongwe asiekua na familia na wala hakuwahi kuwa nayo kabisa maishani,bila wewe kupenda.
ndio maana kwetu sisi wanawauaga wachawi ujue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa 06

Daah kipindi hicho life limenipiga tuko pori mkoa Fulani tunachoma mkaa hapo ni mda kidogo baada ya kumaliza chuo mambo tuliyokutana nayo huku ni balaa

Kwanza kabla ya kuingia porini kuna nyumba tulifikia ya mzee anaishi peke ake ya udongo iko mbali na makazi pia alitupa info kuhusu hilo pori maana sisi ni wachomaji holela bila kibari akatuambia ili moshi usionekane au msishtukiwe nendeni mbali kidogo zamani ndan sana

siku tatu za mwanzo tulikuwa kila tukilala tuseme tuamke usiku mwingi tuchome mkaa tunaamka saa saba za mchana sio zahidi ya hapo mpaka tunajishangaa

Tulikuwa tukisikia sauti za manukato kwa mbali zile za gharama na sometimes harufu za misosi mizur lakini cha kujiuliza kule tulipo ni pori la mbali kuna kabaridi ukungu na kagiza kidogo maana hata miale ya jua inachomoza kidogo kwenye miti jinsi ilivyojitandaza huyu mtu ni nani hivi kweli kuna mtu anaishi humu ?

Katika pitapita zangu kuokota vikuni kidogo kwa ajili ya kuandaa ka ugali ketu jion kabla ya kuanza kazi za uchomaji niliziona nyayo moja nyengine moja kama vile aliepita na mguu mmoja halafu ina vidole virefu vitatu moja imepita kwenye matope imegandana nikaonyesha wadau wakasema atakuwa ni mnyama hapa hadi Leo nashindwa kuamini

Kuna mwenzetu alitoka mbio kutoka mtoni alipokuwa akioga akadai kwamba aliona mda ana nywele ndefu amekaa kwenye mawe ya mtoni japo hatukumuamini maana alikuwa anatumia viroba

Tulikuwa kumi na mbili na tulijipanga kwelikweli kuvuna hiyo mikaa kiholela tulienda mpaka na gunia la dagaa na unga tulikaa sana huko lakini kwa kipindi cha interval kama siku nne au tano hivi tunapungua mfano mmelala kumi na mbili mnaamka kumi na moja mmoja hayupo baada ya wiki kupita ni hivohivo tunapungua tulikuwa tunajua labda kazi imewashinda wamekimbia

Kila tukilala usiku kama vitu tumevipanga tunakuta vimevurugika magunia tuliyoyafunga na kuyapaki vizuri yameangushwa hovyo pamoja na kuskia vicheko kama cha mwanamke kila saa saba ya usiku hilo hatukulipatiliza

Kuna siku tunatafuta uyoga au mboga yeyote hapo porini wakati huo dagaa zimekata tukakutana na mdada mrefu ametuzidi sio sana anapita tulimsalimia tu lakini hatukujua anapoenda wala anapotoka na alijipamba kweli tulilipotezea hilo kwa sababu tulijua pengine kuna watu humu japo haingii akilini au labda ni tourist anafanya forest walk ila tulipotezea

Usiku watu wakilala kesho mmoja anaamka anasema Jana usiku nilikuwa nikiskia kama mtu ananiita tena baba yangu tukajua hzi ni bangi tu maana hilo kundi la mabaharia kulikuwa na walevi ila Mimi nilikuwa situmii chochote kile sio mlevi ila siku moja nimelala usiku nikaskia naitwa jina kabisa M amka njoo basi M amka basi uje uku chini karibia na mto na ni kweli nilikuwa naskia vishindo wenzangu wako fofo ni sauti ya thureiya wangu sasa nikawa najiuliza huyu bi Dada nimemuacha dar sijamwambia nilipo na ananitafuta kweli kweli huku amefikaje usiku huu nikaamua ni mute tu nilale tu hapo nikawaamin washkaj nikawaambia asubuhi

jion tukikaa tumepumzika kwa mbali tunaona kama kuna mtu mrefu anatembea anapotelea kusikojulikana kulala usiku kujikuta umelala juu ya mti wenzangu Mara ya kwanza wakasema hio ni sleep walking ilipo wakuta hawakuamini maana mmoja alishtuka yupo amelala juu ya jiwe mtoni na tulikuwa fofo hatujui aliendaje ye mwenyewe ajui maana kama angekanyaga maji apande kwenye mawe angeshtuka

Kulala usiku kupapaswa ikawa inatutokea sana tukasema tuwe tunalala kwa kubanana kama ndizi kwenye mkungu

Siku hiyo hali ikazidi kuwa mbaya tumebaki wanne sasa wengine hatujui walipo tukasema potelea pote tukaanza kuondoka ilo eneo hiyo ni baada ya wenzetu kuanza kupotea kwa kasi unaamka asubuhi mnakuta mko wachache tukasema haya magunia potelea pote tukaanza kusepa tumetembea weeh ila kila tukizunguka tunarudi palepale

Zunguka wee almost masaa nane tunarudi palepale akili ikatujia ghafla tuufatilie mto kweli tukafanikiwa kutoka lile eneo tukatokeza sehemu kuna kamti mvua inanyesha tukajihifadhi hapo basi mvua ikakata akatokea mmoja kati ya watu waliopotea tuliokuwa nao akasema nyie maboya mnafanya nini hapa twendeni tukabebe ule mkaa mnamuachia nani kwanza mmoja wetu akamtukana nyie wasenge mlikuwa wapi mnatutisha hvyo jamaa akacheka akasema tulienda kijiji jirani kuchukua baskeli za kubebea hayo magunia turudini basi na tumepata kenta ambayo inakibali tumeelewana nae bei akataja mzgo mkubwa kweli

Washkaji wakasema turudini wale watatu niliokuwa nao mi nikasema hapana mtanikuta huko mbele nikawaambia tuachane nae je walivyotukimbia huu si uboya na kututia wasiwasi jamaa akasema we ukienda ukizulumiwa utajua mwenyewe una uhakika kama tutapitia huko mi moyo ukawa unakataa nikakumbuka ka msemo kangu "trust your instinct" nikasema potelea pote mtanikuta mbeleni na changu mtanipa basi tulikuwa wanne mmoja wetu akatukacha akasema hawa kama wametukacha mwanzo wanaweza kimbia na chetu nyie kama hamtaki kurudi shaur yenu jamaa akageuza na yule tuliokutana nae wawili wakakubaliana na Mimi tukaendelea na safari

Tumefika mbele huko tukapumzika asubuhi mwendo tukakutana na mwengine alietoweka oyaa nimetumwa niwacheki hatupiti uko halafu mizego yetu unamwachia nani halafu usipolipwa utamlaumu nani mi nimetoka huko unapoelekea kuna ka kijiji sisi hatufiki huko nimeenda kuulizia usafiri huko magari yenyewe yanazingua mmoja niliekuwa nae katika wale wawili akaniambia niache ujinga yule jamaa Mara ya kwanza alituambaia tukakataa yani kwa kazi niliyoifanya kukesha usiku kuchoma mkaa huo uboya siufanyi wakaguze mi nikasema sirudi tena tukabaki na mmoja ambae alikuwa ni dogo tu kamaliza form 4 alizingua aliamua ajiunge kwenye hizi shughuli ye alitokea kunielewa pale porini na alikuwa rfk tu nilikuwa namshaur ile kazi asiirudie tena atafute mbadala ye kwakua alinizoea akaungana na Mimi tukaendelea na mwendo

Tumefika saa sita hivi kwenye barabara kuu mchana hapo njaa inauma siopoa yakawa yanapita magari kila tukiomba lifti pemben ya barabara haya simami hapo no wachafu kichizi kwa bahat nzur moja likasimama mbaba Fulani hivi akatupakiza akawa anatushangaa kweli akawa anatuhoji mnatoka wapi ?tukamuhadithia hakutuamini akasema huo msitu ulivyo mnawezaje kuingia humo ndani kwanza hii njia yenyewe usiku sometimes ina kuwa na mauzauza hata mchana hapo ndo nkapata wazo kweli kwa ile hali tuliyonayo ndo maana wakawa magari yanakataa kusimama tulitembea na gari almost maa mawili ndo tukafika kijiji jirani mji Fulani x

Hapo ndo nikawa najiuliza yule mwenzetu alietuambia anatoka huku tunapoelekea aliwezaje kutembea kupaona na pia hapo kwenye maji tuliuliza kama kuna mtu kavaa hivi na hivi na hivi kaja kuuliza kama kuna kenta itaweza beba mizigo wake kwa madereva wa kenta pale ambao wataukuta barabarani wakasema hapana tukaa huo mji siku mbili tukarudi kule mji wa mwanzo kupitia barabara rasmi ule ambao tulitumia kuingilia porini kwa maana tulikatiza ktk ya pori tukatokea sehemu nyingine

Tukaenda kwa yule mzee kuuliza kama wenzangu walirudi walipitia pale hili nyumba ya yule mzee sikuikuta nilimuuliza dereva tulioelewana nae Mara ya kwanza kabisa ambae kenta yake inakibali kama majamaa walirudi akasema hapana kwanza alidhani tumepata mtu mwengine kuna mmoja nilikuwa namjua namuonaga maskani ktk hao tulioenda pale maskani hawajamuona na hawajamsikia ktambo sana hata mke wake alishatoa taarifa polisi nikasema huu mji ngoja nichomoke nisije nikawa kama suspect maana watajua aliondoka na Mimi na kwa nini turudi wawili kwakua dogo ni mzaliwa wa pale nikamuaga nikasepa

Japo naskia baadae walipeleleza wakajua tulienda choma mkaa dogo alibanwa kweli polisi walimchomoa darasani alikuwa veta walifanya kuwatafuta lakini wapi

Cha kujiuliza je uchawi upo au hawa majamaa walinifanyia usanii wakasepa na magunia ya mikaa niliotoa jasho langu kuchoma wote ?

Lakini mbona magunia polisi waliyakuta ? Hawa watu wako wapi kipi kimewakuta ? Nimeshindwa kujua jibu mpaka Leo na mke wa jamaa amekataa kuweka matanga anaamin mumewe atarud ni mda sana sasa sjui kilochoendelea

Sent using Jamii Forums mobile app

Cha mwisho yule mzee tuliomkuta mwanzon kabisa kabla ya kuingia porini tulielezea watu kuhusu yeye wakasema hakuna nyumba ukivuka hapa tena wala mzee yeyote hata wakataji mbao na wachomaji mkaa wanasema tunapita kila siku ilo eneo halina nyumba wala mzee ni miti tu na ni kweli tulirudi hatukuona dalili kuwepo kwa nyumba uliyovunjwa kama ingekuwepo
 
ni kweli unavyosema wachawi wana alama zao, nilihadithiwa na binti wa kike aliekuwa housegirl kwenye nyumba moja kbl hajaombewa na kurudi ktk hali yake ya kawaida. Ni kwamba, mtu anapopelekwa uchawini kwa mara ya kwanza huwa wanachanjwa, na hizo chanjo zinawafanya watambuane hata ktk maisha/dunia yetu hii ya kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah wachawi wana mambo!

Duh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku zote uchawi una hasara hauna faida

Na wakichanjiwa navyo wanakuwa na nguvu balaa mwanaume mmoja ana nguvu za wanaume kama kumi wa mikoani kwa hyo hawa watu sio wa kugombana nao watakupoteza mtu gani anapigwa hatoi damu ,hachaniki

Mfano kama kuna kundi mmekaa kuna watu wana vidono wamechanjiwa ikitokea mmoja ametibuka au vimpenda kichwani wakaribu yake kama wanavyo nao wanatibuka

Sent using Jamii Forums mobile app
Vingefaa kuchanjia makomandoo wetu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli?

Nafahamu side effects zake.
Maana kama huyu rafiki yeye ukimchoma kisu hakiingii ila panatoka kanundu kadogo tu ila baadae kanapotea.
Halafu dawa aliyopewa imechanganywa na Mifupa ya mbwa mwitu so ukifika mwezi mpevu anapata shida sana. Si ushaona muvi za Teen wolf au Twilight saga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi mrefu huu ila acha na mimi nisimulie kidogo.

Nimekuatana na matukio mawili yanayoshabihiana na hizi story za uchawi.

1. Mwaka 2016 mzee alikuwa anamjengea bibi nyumba ya kuishi, kwenye mji mdogo X huko Simiyu. Kipindi hicho ndio nimemaliza form six, nikapewa kazi ya kusimamia ujenzi nikisaidiana na mtoto wa dada yangu.

Nikawa ninakaa kwa bibi ambaye anaishi kijiji cha ndani pembezoni ya huo mji, kama mwendo wa dakika thelathini kwa pikipiki mwendo wa kawaida. Tukawa na mazoea ya kutoka kijijini saa tisa usiku kuelekea kwenye huo mji ili kuwahi foleni ya maji.

Siku moja kama kawaida yetu, tumewahi asubuhi. Tukafika sehemu pembezoni mwa barabara tunayopita, tukakuta kundi la wanawake wamevaa nguo nyeusi saa tisa pembezoni mwa barabara. Kwa harakaharaka idadi yao ilikuwa kama kumi na mbili kwa kukadiria. Tuliwaona vizuri maana walikuwa mita chache sana kutoka barabarani na kulikuwa na mwangaza wa mwezi. Nilijiuliza jinsi walivyovaa na mda ule wa usiku kukaa pembezoni mwa barabara nikahusianisha tukio na uchawi.... Though I'm not sure na hakuna cha ajabu kilichotokea zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2. Tukio la pili ilikuwa mwaka 2018 nikiwa field kijiji fulani mkoa wa Dodoma.

Kituoni tulipokuwa tunakaa ilikuwa karibu na centre ya kijiji (kwenye maduka na soko). Hivyo mda wa jioni tulikuwa tunapenda kujichanganya centre tunarudi mida ya usiku usiku, hasa ukizingatia mimi ni mtu wa mitungi.

Lakini ili kwenda centre tulikuwa tunapita njia moja ya mkato ambayo kuna sehemu kuna mto na mbuyu mmoja mkubwa sana. Toka nimeanza kupita hiyo njia usiku nilikuwa sijawahi kukutana na mtu hata kama ni saa moja jioni, wenyeji walikuwa wanapita mwisho saa kumi na mbili.

Kuna siku nilishawahi kupita saa moja kama na nusu usiku kuna mtu akaja ananikimbilia ananiomba tupite wote, eti anaogopa wakati ni wa kiume mkubwa kabisa na midevu yake. Nilishangaa kwa vile nilikuwa sielewi chochote nilipotezea. Siku hiyohiyo wakati narudi nikiwa nimelewa kimtindo nikakutana na jamaa maeneo yaleyale ya mto na mbuyu anaongea kwa Kilugha, nadhani kilikuwa kigogo, anatumia lugha kali kama ananikaripia hivi nikaishia tu kumjibu " mimi sikuelewi unachoongea fara wewe" kumbuka nilikuwa nimelewa kidogo, jamaa alinijibu "haya"

Siku ya tukio sasa tukawa tunaenda Centre na washkaji tunaofanya nao field wawili. Ile tunaenda mshikaji wetu mmoja akatusimulia kuna mtu amemwambia tusiwe tunapita pale ikifika saa moja usiku sio pazuri ila hajaambiwa sababu ni nini. Ile tunarudi tulipofika kwenye mto tukaona kuna mzee kama anavuka mto upande wa pili yaani sisi tupo kwa nyuma yake mita chache sana. Kwa alivyokuwa anatembea polepole tulitegemea tukiibuka upande wa pili tutampita yule mzee. Lakini tulivyoibuka hatukumuona yule mzee na hatukuelewa alipotelea wapi maana kulikuwa hakuna hata vichaka ni eneo ambalo liko plain kabisa na ilikuwa mita chache sana kutoka tulipokuwepo.

Tulipofika mbele mara akaibuka bundi akawa anaruka anapaa anaenda kutua mbele, tukimfikia tena anaruka anapaa anaenda kutua mbele.Alifanya hivyo kama mara tatu. Tulipofika kituoni tunapokaa dirishani chumba tulipokuwa tunalala akaja bundi akakaa hapo mpaka tukalala tumeogopa wote kumfukuza.

Wagogo acheni uchawi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Kiranga bhana!
Hajajibu. Kama mwanasiasa aliyebanwa na muandishi wa habari mahiri.

Halafu analeta logical non sequitur.

Issue ni ku prove uchawi kwa facts. Yeye ananiambia hayajanikuta.

Namuuliza, hayajanikuta yapi? Na yakinikuta, tutajuaje ni kwa sababu ya uchawi tu, na si kingine chochote?

Sijaona jibu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyingine Sumbawanga wakati wa Ujenzi wa shule za kata ile wananchi kuchangia nguvu kazi, mzee mmoja alikuwa haendi wala nini... Afisa Mtendaji wa kata akampa adhabu kuwa hadi kesho yake asubuhi wakute kasomba tanuru mbili za tofali na kusogeza site, vinginevyo atapelekwa polisi. Mzee akasema sawa nitafanya usiku.

Asubuhi wanaamka, tanuru halipo, ila Kijiji chote, wazee, watoto, watumishi kanisani hadi Mtendaji kata wapo hoi, wamechafuka umbi la tofali. Mzee hakuguswa tena na kazi za jamii...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakuwa mchawi huyo maana kutajwa kwa makanisa kunamuumiza Sana nafsi yake.
Wote wanaotokwa na povu wapuuzieni tu,
mahondaw, Tanayzer endeleeni kutiririka tuendelee kujifunza..

hahahahah. ... ngoja kidogo mamy nimalizie kajukumu fulani hapa

Cc Smart911
 
Hivi mkuu ni kweli kuwa wachawi hula nyama za binadamu au stories tu,na je hula binadamu wepi,wafu au walio hai?

Sent using Jamii Forums mobile app

Inaonekana ni kweli si unaona hapo Alawido anavoongea juu ya niliyoyashuhudia ...

wachawi katika mambo mengi hupenda kwenda kinyume
na binadamu wa kawaida ...

Upande wa Giza unatambua sana maana ya mzaliwa wa kwanza,kitu ambacho watu wengi hawajui.
Mzaliwa wa kwanza ni Lango La kiroho.vitu vizuri au vibaya katika familia ni lazima vipitie kwake.

Mwanzo 49:3
Reubeni u mzaliwa wangu wa kwanza,nguvu zangu na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na nguvu.

i. Amebeba nguvu nyingi za familia.
ii. Amebeba Baraka za aina mbalimbali za wadogo zake.
iii. Amebeba nguvu ya upendo ndani ya familia.
iv. Mzaliwa wa kwanza ni lango, Zab 24:7-9, ambapo Baraka zote za familia kutoka mbinguni zinapitia kwake na kuwafikia wadogo zake wote.
v. Amebeba ustawi wa familia kiroho na kimwili.

Pitia na mistari hii pia itakufungua zaidi juu ya hili.
Kutoka 4:22-23
Kutoka 12:12-13
Yeremia 31:9
Mwanzo 21:9
Mwanzo 25:29-34

Sent using Jamii Forums mobile app

asante kwa ufafanuzi mkuu. .

Cc Smart911
 
Back
Top Bottom