MLEVi Mmoja
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 8,514
- 15,050
Nakumbuka kipindi hicho baada ya kusota sota hapo nishamaliza chuo sua nikapata kazi ya udereva wa haice route ilikuwa mwahako to raskazone hii mishe niliipata tanga . wakazi wa tanga watakuwa wanazijua hizi haice na route zake mi sinaga mambo yakuweka mkoa x maana nilichokutana nacho ni cha ukweli.
Ujuzi wa udereva niliupata moro maana baada ya chuo nilikuwa sina kazi uzuri nilikuwa konda Moro mjini kidogo nikapata ka ujuzi wa kuendesha gari pia nishawahi Fanya kazi gereji mbalimbali kwahyo nilivyounganishwa na jamaa tanga alinunua haice aliniamini sana na kutokea kunikubali ambae tulitokea kufahamiana Moro kwenye shughuli zangu maana yeye alikuwa anamiliki gereji nilikuwa nafanyia kazi ya kilocal local tu
Basi nikapewa haice route zangu zilikuwa mwahako kwenda raskazone tunaamka alfajiri piga kazi kwelikweli na konda wangu nakumbuka madereva wenzangu walikuwa Mara nyingi SAA tatu na kuendelea hawafiki kile kituo cha raskazone pale karibia na zile beach sjui sahiv kama wanafika au wanaishia stend sasa kwa tamaa zangu nishakusanya hesabu ya bosi mapema na ela ka zote.
Kwakua madereva wenzangu wengi wa mwahako waliishia stendi mida ya tatu na unusu usiku kugombania wateja nikasema wacha mi nisifupishe route niende na haice hadi raskazone niwazombe wale ambao watakuwa wanakuja stand kwa miguu kupata haice maana haice usku ni shida kidogo.
Basi bwana tukafika pale kituo cha mwisho kulikuwa na wadada wawili wa makamu wamevaa vizuri mmoja suruali mwengine sketi ndefu tuu kidogo ni usku palikuwa pamechangamka nikashangaa kweli cha ajabu tunageuza haice mpaka tunapita mitaa ya bombo hospital hatukupakia habaria hata mmoja kama tulivyotegemea kuwazomba nje kumetulia tukaendelea kukimbiza haice huku tunapiga nao story huku nyuma kuelekea stend ikafika mda pakawa na ukimya nikawa naongea na konda huku gari linaenda hatukuwapatiliza.
"Daah mwanangu M bora tungeishia stend tumekuja huko tumeambulia vichwa viwili " konda ananiambia huko mi naendesha gari uelekeo barabarani "embu waulize hao masister wanashuka wapi ''nilimwambia konda wakati huo tushafika zile hostel za usagara nikaskia konda anasema " tobaaa" nikageuka nyuma na Mimi maana wote tulikuwa tunaangalia mbele nijue kuna nini kuangalia wale abiria wadada hawapo na niseme tu gari lilikuwa spidi walitokaje ?mpaka leo najiuliza japo hio kazi niliachaga kitambo
Sent using Jamii Forums mobile app