Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Nakumbuka kipindi hicho baada ya kusota sota hapo nishamaliza chuo sua nikapata kazi ya udereva wa haice route ilikuwa mwahako to raskazone hii mishe niliipata tanga . wakazi wa tanga watakuwa wanazijua hizi haice na route zake mi sinaga mambo yakuweka mkoa x maana nilichokutana nacho ni cha ukweli.

Ujuzi wa udereva niliupata moro maana baada ya chuo nilikuwa sina kazi uzuri nilikuwa konda Moro mjini kidogo nikapata ka ujuzi wa kuendesha gari pia nishawahi Fanya kazi gereji mbalimbali kwahyo nilivyounganishwa na jamaa tanga alinunua haice aliniamini sana na kutokea kunikubali ambae tulitokea kufahamiana Moro kwenye shughuli zangu maana yeye alikuwa anamiliki gereji nilikuwa nafanyia kazi ya kilocal local tu

Basi nikapewa haice route zangu zilikuwa mwahako kwenda raskazone tunaamka alfajiri piga kazi kwelikweli na konda wangu nakumbuka madereva wenzangu walikuwa Mara nyingi SAA tatu na kuendelea hawafiki kile kituo cha raskazone pale karibia na zile beach sjui sahiv kama wanafika au wanaishia stend sasa kwa tamaa zangu nishakusanya hesabu ya bosi mapema na ela ka zote.

Kwakua madereva wenzangu wengi wa mwahako waliishia stendi mida ya tatu na unusu usiku kugombania wateja nikasema wacha mi nisifupishe route niende na haice hadi raskazone niwazombe wale ambao watakuwa wanakuja stand kwa miguu kupata haice maana haice usku ni shida kidogo.

Basi bwana tukafika pale kituo cha mwisho kulikuwa na wadada wawili wa makamu wamevaa vizuri mmoja suruali mwengine sketi ndefu tuu kidogo ni usku palikuwa pamechangamka nikashangaa kweli cha ajabu tunageuza haice mpaka tunapita mitaa ya bombo hospital hatukupakia habaria hata mmoja kama tulivyotegemea kuwazomba nje kumetulia tukaendelea kukimbiza haice huku tunapiga nao story huku nyuma kuelekea stend ikafika mda pakawa na ukimya nikawa naongea na konda huku gari linaenda hatukuwapatiliza.

"Daah mwanangu M bora tungeishia stend tumekuja huko tumeambulia vichwa viwili " konda ananiambia huko mi naendesha gari uelekeo barabarani "embu waulize hao masister wanashuka wapi ''nilimwambia konda wakati huo tushafika zile hostel za usagara nikaskia konda anasema " tobaaa" nikageuka nyuma na Mimi maana wote tulikuwa tunaangalia mbele nijue kuna nini kuangalia wale abiria wadada hawapo na niseme tu gari lilikuwa spidi walitokaje ?mpaka leo najiuliza japo hio kazi niliachaga kitambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee! Mimi ninachojua niliambiwa babu yangu alikuwa mtu wa dini sana! Alifika tu mkoa fulani, akaoa na akafia hapo. Hawajui ni wapi alipotokea na sijawahi kumuona! Ajabu hata picha hakuwahi kupiga! Baadhi ya ndugu waliyomuona babu akiwa hai wakimuota wanamuona amesimama huku nyuma yake kukiwa na nyumba inang'aa sana.
Huyo babu yako alikuwa na vinasaba flani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa cha pili 02


Kipindi bado nipo hapo hapo tanga nakapata ka off kidogo nikasema ngoja niende chichi club nikaenjoy nikasafishe macho sikuwa na rafiki zaidi ya konda wangu ambae tulikuwa tumezoeana nakumbuka ilikuwa jmosi hatukuendesha haice ilikuwa mbovu kwahyo ikawa kama ni mapumziko


Wakati huo Nina ka ugwadu kwelikweli na bibie sijamwambia Niko tanga nilimdanganya Niko Moro kuna mkoa nazurura kujitafutia yeye alibahatika kupata kazi baada ya chuo nilisoma nae chuo primary na olevel kasoro advance na tulikuwa wote orphanage sikutaka kumwambia hali ninazopitia sikutaka kumpa majoz pia na kuwa burden kwake


Basi bwana baharia mwandamizi [emoji3]nikaone zile chipsi zetu pendwa chips funga nikaifata ilikuwa refu nyeusi macho mazur kama mnywarwanda vile tukakubaliana bei maana chichi ni machimbo yao tukaingie lodge kakaenda kuoga funguo nikaichukua nikaificha kwa ajili ya usalama tulielewana mpaka asubuhi nikavua boksa nikavaa taulo na Mimi nijiandae kuoga


Nikaona huyu mtu anachukua mda kutoka nikasema ngoja nimfate bafuni cha kushangaza naingia simuon mtu ni mbomba la mvua tu linatoa maji nikajiuliza huyu yupo wapi kama angetoka singemuona chumba chenyewe ni self


Nikavaa haraka nikatoka nikiwa na uoga mpaka pale reception nikamuuliza receptionist ujaona mdada alietoka niliekuja nae akaniambia si mlitoka wote hapa baada ya dk 5 mlivyoingia kwenye room tena wakati mnatoka hapa mkaniambia bado mpo mnatoka Mara moja kutafuta chakula daah nilichoka nikaamua nikabidhi funguo

Natoka nje kidogo mlinzi aliongea ki friendly tu ananiambia boss uko chap Mara hii umerudi na mmeniaga mnaenda zurura nje shemu umemuacha wapi ? Nilishtuka nikajichekesha nikasema tulihairisha lakini kichwan nilikuwa na maswali huyo aliefanana na Mimi ni nani au kivuli changu ?huyo mwanamke ni nani amenipoteaje poteaje ?


Na hili tukio ktk matukio yangu ya kustaajabisha sikuwah mwambia mpenz wangu maana alivyojua nilienda tanga nikamficha ulikuwa mtiti halafu tena nimwambie nilikutana na kisanga nilivyonunua chipsi funga aka Dada biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Kiranga embu njoo mara moja upande huu utoe ufafanuzi kidogo
Mimi mtoto wa "kishua" lakini nimekaa mpaka Uswahilini kwenye nyumba za vyumba sita zenye vyoo vya passport size na kuhesabu buibui kwenye dari la kuangalia fito na mabati lisilo na ceiling. By choice, ku experience maisha.

Zile nyumba za mtoto kukugongea asubuhi na kukuambia "mama kasema anaomba shilingi mia".

Zile nyumba ambazo ukitoka asubuhi kwenda mjini, ukiwa na nauli tu, unaonekana umeyapatia maisha.

Ushawahi kusikia sehemu inaitwa Ubaya Ubaya? Washkaji walikuwa wanakuja na magari yao kutoka Oysterbay wakija mara moja hawarudi tena, barabara ilikuwa na mashimo mengine utafikiri umefika ziwa Victoria, gari zima linaweza kuzama lisitoke.

So don't let anybody box me in "mtoto wa kishua".

Kuhusu uchawi, nishatoa kidau hapa mtu aniloge, wachawi wote na ndugu zao hapa JF wameshindwa.

Let's prove things by experiment. Mtu aloge nishindwe kuja hapa JF siku zilizobakia za 2019.

Akifanikiwa kuna $1000 atachukua kwangu.Akishindwa nichukue $1000 kwake.

I tell them put your money where your mouth is.
 
Kiranga, Mkuu iko hivi principle ya wachawi huwa wanamroga mtu wanayemjua.
Au hata Kama hawamjui basi lazima ndugu yake mmoja afanye connection.

Kwa sababu ili mtu akuroge Kuna details zako muhimu lazima azipate kwa mfano majina yako yote au sehemu unazopita na kukanyaga unyayo au nguo zako.

Sasa ni ngumu kumwambia mtu akuroge wakati umejificha humu jf na hakuna anayekujua na kukuona live Sasa atakurogaje.

Ukitaka kujua watu wanarogaje safuri uende Kigoma,Sumbawanga au Kigoma vijijini huko halafu utangaze kwamba una hamu ya kurogwa halafu usikilizie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani wewe ukisema uchawi haupo ndo haupo kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijataka kusema tu.

Nimeweka dau la $1000 hapo juu.

Thibitisha uchawi upo kwa kuniloga nisiweze kupost kitu JF kwa siku zilizobakia za 2019.

Ukiweza nakupa $1,000.

Ukishindwa unanipa $1,000.

Unakubali challenge hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbu wa dengue, Uchawi ni stories tu na kucheza na saikolojia za watu.

Hakuna uchawi kama inavyosemwa.

Mababu zetu ambao hawakuelewa redio zinafanyaje kazi, waliwaona wazungu wana uchawi kwa uwezo wao wa kutumia redio.

Wazungu walivyoweza jutaburi kuoatwa kwa jua, mababu zetu waliwaona wachawi.

Ukiamini uchawi, hata kitu kinachielezeka bika kuhitaji uchawi, utaona kinaenda kwa uchawi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
digba sowey kabla sijasimulia visa vyangu vya kichawi tuwekane sawa kwenye haya mambo

1.Mwaka 2009 chuo SAUT mtwara ndio kilikuwa kinaanzishwa kwa maana ya intake ya kwanza iliyomaliza 2012. Na kama field walienda 2010.

2. Kuhusu mwanafunzi wa chuo kufariki kwa kipindi hicho hakuna aliefia uwanjani.
Waliopat kufariki kwa hiyo intake yako ni Aron Seda(ajali), na wengine siwakimbuki lkn walifariki kwa magonjwa mengineyo.

Na declare kwamba kipindi hicho nilkuwa mfanyakazi chuoni hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom