Kisa cha 03
Hichi kisa nilihadithiwa na mzee Fulani nilipata kuzoeana alikuwa rafiki tu na tulikuwa tukikutana nae katika vijiwe vya kahawa maana nlikuwa napenda jion nikae na wazee nipate mawili matatu nae alikuwa mganga wa kienyeji huyu mzee alikuwa na mtoto wake mkubwa nae alikuwa mganga ila alishakufa
Story ni hivi anasema mwanae ktk shughuli za uganga alikuwa akisaidiana nae siku moja akaletwa mmama wa makamo kama mwenye late 40s kwa kukisia anasema alikuwa ametupiwa majini kwa hyo aliachwa hapo auguzwe basi wakaanza kumtibu yule mmama akapandisha majini wakawaambia sisi hatutaki kutoka kwenye kichwa cha huyu mtu nyie wadanganyeni tu walieni pesa zao waambieni kapona na sisi tutatulia kwa mda ila sisi msitulazimishe kutoka laasivyo tutakuja kwenu
Mzee akaguna halafu ukicheki ktk kipindi chote cha uganga hajawahi kutana na mgonjwa mgumu kama huyo akamwambia mwanangu embu tumuache naona kama roho haitaki nifanye hivo mwanae kwa kutaka sifa akamwambia kama baba umeshindwa kazi kwa uwoga wako niachie Mimi yule mzee akakaa zake pembeni akawa mtazamaji akasema sawa
Basi kijana akapiga kazi kwelikweli na akafanikiwa kuwatoa na hio kazi ilimpa sifa kweli na pesa maana wenye mgonjwa walishakata tamaa lakini wakashangaa mfumbuzi kapatikana walifurahi sana anasema kazi ilianza alfajiri ikaisha saa sita mchana
Jioni mzee akiwa kwenye kijiwe chake cha kahawa anaambiwa wahi haraka nyumbani maana walikuja vijana kumpa taarifa kijana wake walimuokota njiani na damu puani mida ya saa Tisa ameanguka mzee akawahi haraka nyumban kujua kulikoni na akamkuta kijana wake anahema kwa shida akamuuliza kulikoni
Mwanae akasema baba nilikuwa napita barabarani sasa nikakutana na watu wawili wamevaa mavazi ya rangirangi halafu warefu mno wakanisimamisha kwa kupeana mkono walikuwa na vidole vyembamba virefu wakanisalimia nikajiuliza hawa watakuwa wa kina nani au wateja nini lakini wakaniambia "we si tulikwambia usitutoe lakini hukutuskia sasa tunakuja kwako" jamaa hapohapo kizunguzungu akazimia ndo akashtuka yupo kwao kitandani akujua kilichoendelea
Yule mzee alimuugua mwanae siku hiyohiyo kesho yake jioni mwanae alikutwa amekata ringi kitandani na damu zikitoka puani
Anamalizia kusimulia hvyo akaniambia kijana wangu we ni mgeni ktk huu mji na dunia kwa ujumla kuishi kingi ni kuona mengi hii dunia INA mambo ya ajabu ya kustaajabisha mwanzo sikumuelewa ila baada ya miaka kadhaa na mkasa mkubwa niliokumbana nao ktk maisha yangu japo sio wa uchawahi na hausiani na uchawi nilikuja kumuelewa dunia hadaa ulimwengu shujaa
Sent using
Jamii Forums mobile app