Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

aisee kuna kisa kimoja sitakisahau 2005 hapo nipo kidato cha kwanza.ilitokea msiba wa ndugu yangu baada ya mazishi siku hiyo tulipewa jukumu la kulinda kaburi usiku kijijini huko full migomba ya ndizi. na hiyo huwa ni mira zetu kulinda kaburi ndani ya wiki moja.tunakesha usiku kulinda kaburi mapaka asubuhi. siku ya kwanza ilipita fresh.siku ya pili aah! mida ya saa tisa kasoro tulikumbwa na vitu vya ajabu. nikaamini uchawi upo

Sent using Jamii Forums mobile app

Vitu gani vya ajabu vilivyotokea
 
Mwaka 1999 nilipita kwenye ukuta live bila chenga, ilikua hivi nimetoka kuoga nakatiza dinning room, nika teleza bahati mbaya nilidondokea meza ya msosi mama aka nipa kipigo cha haja na kunifungia chumbani, kwakua nilikua na hasira za kupigwa kwa kuonewa na kufungiwa chumbani, nili ukuazia macho ukuta uku na ufata, niliona ukuta ukijigawa kati kati nikapita nikatokea sitting room nyuma ya kiti cha mzee, Wote wali pigwa butwaa na kwakua nilikua nime kasirika amna alie nisemesha. Hadi leo kila Niki jaribu kupita tena sijawahi fanikiwa. ILA NAHISI NILIIKUA KWENYE MAJARIBU YA KUWA MCHAWI.

Mmh
 
Mimi n mtu wa maombi sana,huwa wanakujaga wenzangu home tunapiga story then tunaanza ku praise ku worship kisha tunazama kwenye maombi,unajua mnapoomba zile kelele sasa Tuna shout sana.

siku moja nimelala usiku nikaota kuna bibi mmoja nyumba ya jirani alinifata usiku akaanza kunirushia mawe anipige,ila kila akirusha mawe kuna mkono ulikua mbele yangu unayazuia yale mawe,yule bibi akawa anawambia wafuasi wake pigeni mawe huyo

amezoea kutupigia makelele usiku na wenzake,walirusha mawe sana mwisho wakasema na kesho tutakuja tena leo ni trela tu,hapo kumbuka nilikua ndotoni.

Palipokucha asubuhi nilikuta chumbani kumejaa mawe vipande vya matofali mawe ya kila aina,sikuamini macho yangu nilihisi naota,maana ni vingi vingi vingi.

Basi nikavikusanya nikaenda vitupa nnje,mchana umefika nikawa nataka kugongelea msumari mahali,nyundo sina nikasema asubuhi nilitupa mawe ngoja nikachukue kipande kimoja nije kugongea,kwenda pale nilitupa yale mawe Sijakuta hata kipande cha mchanga.
 
Siku moja zamani sana tuliharibikiwa na bus maeneo fluni panaitwa makuyuni Arusha tukiwa tunatoka Dodoma tunaelekea Moshi kwa Bus enzi hizo ni mabus yalikuwa ni ya kampuni ya Rali hakuna mabasi mengine.

Kipindi hicho barabara ni mbovu sana gari inachukuwa siku mbili kufika Moshi.

Ikabidi konda na abiria mmoja wafuate spear Dodoma nayo ilichuwa siku mbili.

Ilibidi wazazi waniojiongeze tutafute nyumba za jirani ili angalau tupate huduma kama chakula, kuoga na kadhalika wazee na familia zingine walifanya hivyo pia.

Kutoka hapo kwenye bus mpaka kwenye nyumba ni umbali wa kama kilometa tano hivi tukakuta nyumba mbili tu lakini tunashukuru nyumba tuliofika tukawaeleza shida zetu walituelewa ambapo walikuwa wanaishi watu wawili tu kijana mmoja na mke wake ambaye alikuwa mrembo kweli wengi tulishangaa kwanini waliamua kuishi porini ili hali kwa muonekano walikuwa ni watu wastaarabu sana.

Basi baada ya wazazi wetu kupokelewa wakaanza mandalizi ya kupika na mambo mengine sisi watoto mimi na mdogo wangu na watoto wawili wa familia moja tulienda kucheza eneo fulani kama shamba hivi lakini kulikuwa na mteremko unaelekea kwenye mto hivi pembeni ya ya huo mto kulikuwa na ndizi mbivu basi tukazikimbilia tukazichuma tukaanza kula.

Kwakuwa ule mto haukuwa na maji tukavuka upande wapili hapo tuliona matunda ambayo siyakumbuki ni matunda gani lakini yalikuwa matamu sana.

Baadaye tukaona kijumba kidogo cha udongo kimeezekwa kwa nyasi tukaenda mpaka kwenye hicho kijumba tukamkuta bibi mzee sana anachuma mboga karibu na nyumba yake tukasalimia tukamweleza sikumbuki nini lakini akatuletea mziwa tukanywa.

Mara kukawa na wingu zito sana na radi baada ya dakika kumi mvua ilinyesha kunyesha tukaanza kukimbia nilibidi nimemshika mdogo wangu mkono alikuwa analia sana na mdogo wake na yule mwenzetu naye alikuwa analia sana, basi yule bibi alituzuia tusiondoke mpaka mvua itakatike ila mimi na na mdogo wangu tuliondoka na kuwaacha wenzetu tukaelekea mtoni ili tuvuke ngambo ya pili tuondoke ajabu ngambo ya pili tulimuona yule Bibi na fimbo yake amekunja uso anaonyesha ishara ya tukivuka tutaipata daa tulitetemeka sana huku dogo analia vibaya sana bibi anatunyooshea ile fimbo turudi.

Nyuma ya yule bibi tukaona kwa mbali mwanga wa tochi na sauti za watu kama wanaongea ndiyo kumbe mzee wanatutafuta.

Yule bibi kuona watu wanakuja akaja upande wetu huku akivuka mto huku anatembea kwa kuinama na fimbo yake tukampisha tukanza kumuita mzee huku tunatetemeka na dogo analia tumeloa chakari mzee alivyotuona walipatatwa na hofu sana wakatuuliza yaliotokea tukawaambia wenzetu wapo kwa bibi mmoja kule juu mwenyeji wetu na wazee waliwafuata kwa yule bibi huku mwenyeji akisema huyu bibi ni mchawi sana asije wazuru watoto wakakimbia kufika pale wakawakuta wapo ndani kwa yule bibi wanaota moto lakini wamejikunyata wamelegea sana hawajiwezi huku huyo bibi akiwa amejilaza kwenye kitanda chake anatamka sijui maneno gani.

Yule mwenyeji nasikia akamkoromea sana huyo bibi akamwambia lolote litakalo walata hawa watoto tunakumaliza ndiyo ikiwa salama yao.

Kufika pale kwa mwenyeji wetu hapo ni usiku kama saa 2:30 kunagiza tunawahadithia kilichotokea mh..wazazi waliogopa sana tukagombezwa sana lakini tunashukuru mpaka leo tupo salama ingawa mwenzetu mmoja alishatangulia kufa .

Hayo ndiyo nakumbula lakini ilikuwa siku mbaya sana na sitaisahau maishani.
[emoji117]Kwakuwa ule mto haukuwa na maji...

unauitaje mto ilihali hauna maji, ama ulikuwa unamaanisha bonde?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi

Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri

Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma

Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma

Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea

Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge

si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.

wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.

Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele

Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
Hahah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sitosahau niliwahi kukutana na mshkj 2013 kipindi iko ni mlevi mno wa pombe ilikuwa pub flan X maeneo ya Sinza. Mimi ni Me ila kiukwl yule mshkj alikuwa complete HB ase af anaswaga mwanzo I thought ni celebrity ule mvuto wake. Unajua tn ushkj wa hapa na pale redbull akaniambia amenikubali nipo mwana ila kanihusia niache pombe. Sitokuja kusahau nilimuona yule mshkj ana apper sehemu tatu kwa wakati mmoja nilihis ni pombe hapna the shit was real. Yan hivi nilimuacha meza ya caunter, nikielekea toilets nilipishana nae akitoka yeye yey, sikuingia toilets kwa hofu nilikimbilia nje ya bar kweny packing huwezi amini nilimkuta kwenye packing wakati alielekea caunter kwa akili za pombe nilikimbilia caunter nihakikishe ivi kweli sikumkuta na chakustajabisha nilimuuliza muhudumu wa caunter akaniambia kaka kalale ilikuwa uko mwenyew apa unaongea hukuwa na mtu..aisee pombe zilikata nilipigwa na kitu kama shoti nilianza kutapika kufika home nahofu niliumwa wiki nzima hoii. Na ndio mwisho wangu wa pombe ile siku. Miujiza ipooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ilikua jumapili nimetoka somewhere saa nane kasoro nikapita njia moja ya makaburini ile naanza kuingia kweny makaburi akaja bundi akatua mbele yangu kwa vile sijawahi ona bundi live nilianza kumshangaa kama sekunde 30 kisha nikageuza nibadili njia ambayo nayo ipo sambamba na makaburi ila kwa upande mwingine napo bundi akapita juu yangu anaelekea kwa iyo njia nikageuka kumcheki kama ni yule wa kwanza ila alikua palepale hivyo wakati nageuka sikumuona yule mwingine katua wapi nikakaza roho nikaendelea kutembea hadi nikafika home.

nataka nipite iyo njia usiku mwingine ili nione kama hao bundi wanakua hapo kazini au walikua ni bundi wa kawaida tu endapo sitawakuta tena.
Unataka kusema ilijuaje kuwa hao ni ndio bundi wenyewe ilihali hukuwahi kuwaona kabla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me ktk maisha yangu nimeshuhudia mambo mengi sana ya kichawi ingawa mengine nikatka ndoto lakini yalikua na uhalisia

Ila tukio ambalo siwezi kusahau ni ktk hizi nyumaba za kupanga ambapo nilipanga na mmama mmoja hivi wa kiha, basi kuna rafiki yangu yeye alikua na mashetani ya uganga na nilikua nalala naye

Siku moja akaniambia ndg yangu huyu mama jirani yetu mchawi nilimuona kaingia humu na Lengo lake nikutuchezea nikachukulia kawaida

Basi yule jamaa alikuja akaondoka nikabaki Mimi na ndg yangu mmoja asa hapo Yule mama akawa anafanya utawala sasa full kututesa usiku kuna kipindi nikawa namuona kabisa anaingia kupitoa mlango mida ya usiku lakini nikawa nashikwa na bumbuwazi nashindwa kusema

Siku moja nilipoona mambo yamekua si mambo ikabidi niende Kwa dr mmoja hivi akaninipa dawa na kaniambia nenda kadeki ndani na utadeki Kwa muda wa siku 3 kweli Kesho yake asubuhi nikafanya hivyo kablacjaenda kwenye Mishe

Asa nilikuja kushanga ucku nilipo lala mishale ya saa 8 ucku niliskia sauti ya paka alilia mara3 nachakushangaza alitokea mlangoni na mlango nilikua nimefunga akaelekea uvunguni wa kitanda

Mpaka kuna kucha akawa yupo mle ndani na hali ya pale nyumani ikawa imezorota Fulani yaani mtoto wa Yule mama alikua mpole sana na hata mama yake akawa haonekani ovyo na hata nikikutana naye namuona yupo katka Hali ya unyonge na kisasi cha Hali ya juu

Ila nilifuata Yule Dr nakumueleza akaniambia Yule ni adui alivyoingia mle alikuta bahari hivyo akawa hana jinsi na akaniambia nenda kamalizie kudeki hiyo dawa

Ingawa kuna siku wakati nachanganya ile Dawa ili nideki alikuja Yule mtoto wa Yule mama akainyooshea kidodole ndoo ya dawa , ila hapa usiniulize nilimuona vp majibu nitakayokupa huenda hautaamini......

Sent using Jamii Forums mobile app
sema!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dah nmesoma sana ngoja na mimi ntoe kisa kilichosababisha niape kuwa sitakwenda kwa mganga tena kwenye maisha yangu.

ilikuwa 2002,tunatoka dar tunakwenda mkoa wa kigoma kwa wanojua bara bara enzi hizo wanajua ni jinsi gani kulikuwa na majambazi hasa ndani ya mapori ya Tabora,bahati haikuwa yetu mida ya saa 5 usiku wakati tupo road tukakuta bara bara imewekwa bonge la gogo mzee akataka kujitahid aligeuze ghafla walitokea watu wamebeba bunduki ndo kwa mara yangu ya kwanza kuone mtu kashka bunduki huku kajizungushia mkanda wa risasi mwilini bro wangu ile kuwaona tu akakata moto tuliokuwa hatujazmia tulikuwa watatu 3 mimi mzee na bimkubwa.

Tulichezea sana vitasa mzee alidhalilika mno mwisho wa siku walichukua mpka viatu nakumbuka viatu vyangu vya kitoto vya kuwaka taa,then wakaondoka mpka na gari tulikaa pale mpka saa 11 ndo tukapata msaada tukaenda polisi but hawakuwa na msaada mzee akapiga simu kigoma ikatumwa nauli tukaenda moja kwa moja mpka kwa baba yake(means babu),sasa babu yeye kila alivyokuwa anahadithiwa alikuwa anacheka mno hasa akimuangalia bro na ujanja wake ote et kazimia,upande wa baba yeye alikuwa na hasira mno alichokuwa anataka yeye ni wale watu awashikishe adabu hata kufa wafe basi ilivyofika usiku tukaelekea sehemu fulani inaitwa ujiji kwa mzee fulani alikuwa anaitwa juma njemba.

Nadhani kwa watu wa kigoma wanaweza kuwa wanamjua,akaelezewa kila kitu akasema hicho ni kitu kidogo sana,huku na yeye anacheka kisha akasema kuwa pale kwake kuna mbuzi alimchinja sababu ya sherwhe ya mwanae hvyo itatubidi tumtafutie mbuzi mwengne amreplace ili iwe kama malipo yake baba akakubali,kilichofata akawaita wajukuu zake walete (ubumba) ni udongo fulani hivi wa mfinyanzi kisha akawa anatengeneza kimdoli kidogo cha udongo kama vile vya kitoto toto,baada ya kukitengeneza akaanza kukiandika maneno yake kisha akakisimamisha chini,then akaanza kuongea maneno yake aliongea sana baada kama ya saa 1 akasema mtu yoyote ndani ya hichi chumba haruhusiwi kukimbia wala kupiga kelele kwani kwa kufanya hivyo ndo itakuwa kifo chake.

Basi aliendele kusema maneno yake ghafla yule mdoli pole pole alianza kukua na kuwa mkubwa pole pole,baada kama ya dakika arobaini alikuwa ni mkubwa kama binadamu mwenye mwili mkubwa alikuwa anamkono na kifua kikubwa na mrefu,kwa mara ya pili bro tena akazimia kwa mara ya pili mim mkojo ulishantoka natetemeka kama nmepatwa na dege dege,mwisho yule mdoli akaambiwa shtaka letu kisha akaambiwa nenda hivi vitu vinatakiwa leo leo,theb yule mtu akafungua mlango akatoka mbio alikuwa ni mwanaume lakini yupo uchi na ni mweusi tii kama mkaa mpka macho hakuwa na ichi kiini cheupe ye alikuwa na kiini cha moja kwa moja cha weusi,alivyoondoka tukaanza kumpepea na kumwagia maji bro alivyoshtuka yule mzee akatuambia kazi imeshakwisha kesho mtayapata majibu yenu.


Ilivyofika asubuhi tukapigiwa simu nakumbuka enzi hizo kulikuwa kuna buzz siyo hii tigo na hata simu zilikuwa za mezani,tukaambiwa kuwa kuna gari imepatikana Tabora yenye namba kama tuliyoripoti pamoja na vitu vingine,tukaanza safari na treni mpka tabora kufika kule tukakuta vitu vyetu na vingne vingi tu ila mzee alisema vyote vilikuwa vyetu hela zilikuwa kama 1m lakini zilipatikana 7m polisi hawakuchukua hata cent na hata walivyopewa walikataa kata kata hakikupotea hata kifungo kisha baada ya kuchukua tukaambiwa kuwa hao majambazi waliotuibia walikutwa msituni wakiwa wameuwawa wakasema wanahisi ni wanyama wakali ndo waliwauwa maana walikuwa wanaalama za meno makali milini mwao na kucha.

lakini wakashndwa kuelewa kama ni wanyama ndo waliwashambulia ni wanyama aina gani na kwanini hawakuwapiga hata risasi moja hao wanyama na wakati walikuwa na silaha nzito?Baada ya maelezo mengi mzee akawasha gari mpka kigoma stend ya kwanza mpka kwa yule mganga tulinunua mbuzi na zawadi nyingne nying lakini mzee aligoma hakutaka chochote zaidi ya mbuzi tu,basi tukampka mbuzi wake, akasema imebaki kazi moja tu na kazi yenyewe ni kumrudisha yule kiumbe(mdoli mtu)ili asitudhuru na sisi maana ni wetu hapo mdipo ilipokuwa mtihani maana kuna msharti mengi tulikosea plus kujisahau sasa akawa anatuandama sisi atuue dah kila mmoja nyumbani anaalama ya yule kiumbe yangu ni kungatwa skio na kula kipande nikipata mda ntawamalizia kisa changu but mpka leo mimi kwenda kwa waganga ni big no,but thanks god tulitoka salama


picha ya nilipongatwa kwenye skio ambyo ni alama ambayo sitaweza isahau mpka kifo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ndo funga kazi. Aseee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi ni nini kwanza?

Na unajuaje huu ni uchawi, na si physics, chemistry, biology au psychology usiyoijua tu?

Mababu zetu waliwaona wazungu wachawi, kwa sababu walikuwa na redio, waliweza kutabiri kupatwa kwa jua.

Leo tunajua huu si uchawi, ni vitu vinavyoelezeka kisayansi.

Muandishi maarufu wa Science Fiction, Arthur C. Clarke, alisema, "Any sufficiently advanced technology is indistinguishable from magic".

Sasa wewe utajuaje this is magic from some technology/ trick you don't know?

Wewe utajuaje vitu unavyoita uchawi leo, ni uchawi kweli, au ni vitu vinavyoelezeka kisayansi tu, ila wewe hujajua vinaendaje?

Unajuaje kwamba haupo katika position ile ile waliyokuwa mababu zetu ya kuwaona wazungu wachawi, kwa sababu wanatumia redio na kutabiri kupatwa kwa jua?
Tumekuelewa, basi tuachue huu uzi wetu sisi..walau tupate cha kujifunza, akili za kuambiwa changanya na zako mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa na miaka Tisa ya ndoa yangu sikuwahi dhani wala kujua wife ni mchawi maana alikuwa msomi wa juu sana na mtu wa kanisa sana.siku moja nikiwa nimelala ulivuma upepo mkali mno gafla nikiwa macho nikajikuta nanyanyuliwa juu aisee nilisali sala zote gafla nikarudishwa chini.Kuangalia pembeni yangu alipolala mwenzangu naona mbwa aisee ulikuja kama usingizi hivi sekunde wife akarudi ktk hali yake ya ubinaadamu.Kesho yake nikahama home na ndoa ikafa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseee...[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
R.I.P ndugu yangu Seba wachawi sio watu wazuri. Mwaka 2000 alianza masomo ya secondary huko karagwe. Akiwa form one bado aliamka asubuhi akiwa kanyolewa nywele sehem ya mbele ya kichwa. Na wiki hiyo hiyo akachanganyikiwa kabisa. Ndugu wakahangaika mwaka mzima kwa waganga mpaka akapona. Baada ya kupona akaja Dodoma kusoma Jamhuri. Hapo akapata tatizo la macho akawa anatumia miwani mpaka alipomaliza Form 4.

Hapo tulihamia mpwapwa, tatizo lake la macho likawa kubwa zaidi akawa haoni kabisa hata kwa miwani. Hospitali walisema hawezi kupona tena. Mama akaenda kwa kanisa moja la walokole ili Seba aombewe. Seba alikua mkatoliki Safi sijapata ona. Anafunga na kusali kila siku. Muda wa jioni alikua anakusanya watoto wa mtaani pale na kuwafundisha neno la Mungu. Alikataa katakata kwenda kuombewa kwa walokole huku akirefer sehem ya kanuni ya imani Nasadiki kwa kanisa moja takatifu katoliki la mitume hivyo siwezi kwenda kwingine. Baadaye akajakukubali na akaombewa akaanza kuona tena bila miwani. Hii ni Mara yangu ya kwanza kuona muujiza maana nilikua naamin stori za mtaani kwamba wale wanaombewa hua washapangwa hakna lolote.

Baada ya kupona akahamia ulokole huko Sasa ndo akazidisha imani anafunga masaa 72, kanisani kwao anahubiri, mtaani anaombea wenye mapepo na magonjwa. Baadaye akarudi kwao karagwe akaanzisha tution center huko ikamlipa mpaka akajenga madarasa ili afungue secondary. Huyu jamaa toka nimjue ni fighter sana wa maisha af Kama alikua na bahati flani kwa kila analofanya. Akiwa amefikia kupaua madarasa na gari iloleta mabati imefika hapo shuleni akazidiwa ghafla akakimbizwa hospital ya wilaya akalazwa. Cha ajabu kesho yake hawakumkuta hospitali akaja kuokotwa Kama km 30 hv kutoka hospitali yupo porini na hali yake ni mbaya sana. Kabla ya kufika hospitali akawa kashafariki. Hivyo ndivyo wachawi walivyomsakama ndugu yangu mpaka kumuua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sad[emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 1999 nilipita kwenye ukuta live bila chenga, ilikua hivi nimetoka kuoga nakatiza dinning room, nika teleza bahati mbaya nilidondokea meza ya msosi mama aka nipa kipigo cha haja na kunifungia chumbani, kwakua nilikua na hasira za kupigwa kwa kuonewa na kufungiwa chumbani, nili ukuazia macho ukuta uku na ufata, niliona ukuta ukijigawa kati kati nikapita nikatokea sitting room nyuma ya kiti cha mzee, Wote wali pigwa butwaa na kwakua nilikua nime kasirika amna alie nisemesha. Hadi leo kila Niki jaribu kupita tena sijawahi fanikiwa. ILA NAHISI NILIIKUA KWENYE MAJARIBU YA KUWA MCHAWI.
Kwa hiyo bado unaishi hapo hapo kwenu???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie niliamini uchawi upo baada ya kumtoa mpangaji wetu aliishi kwetu kwa miaka 15! Hadi mzee alikuwa ameshaanza kusahau kuendeleza hiyo nyumba baada ya kwenda pale na wachungaji wakaomba yule mpangaji alihama pasipo kufukuzwa.
Vitimbi vilianza nyumba haikupata mpangaji miezi sita ilibidi mimi na mdogo wangu tuhamie kwenye hiyo nyumba ili tutafute mpangaji. Tulivyokuwa tumelala usiku tulisikia sauti za paka wengi sitting room wanaburuza viti na meza asubuhi kuamka tulikuta mavi ya mtu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
kwa hiyo hata hamkuuliwa??[emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom