Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Hiki kisa kilinitokea mimi mwenyewe miaka ya 80, kati ya 86/87. Sikumbuki mwaka sahihi sababu ya umri mdogo niliokuwa nao, ila nilikua najitambua. Tukio hilo lilitokea sehemu ambayo baadaye nilikuja kujua kuwa inaitwa makuburi jijini Dar, baada ya kuwauliza wazee nikiwa na umri wa kutosha kwenye miaka ya 90. Maana ni tukio ambalo hadi leo huwa tunataniana sana tukikutana familia nzima. Nakumbuka ilikuwa kipindi hicho Mzee alikuja Dar kwa ajili ya kusoma UDSM baada ya kuamua kujiendeleza. Sasa akaona ili asome vizuri, ni vema awe pamoja na familia yake. Kwahiyo baada ya kumaliza taratibu za kujisajili chuoni, akaamua kutafuta nyumba. Ndio akapata nyumba nzima huko makuburi. Basi akafuata familia yake, mama, mimi na dada yangu. Basi tukafika jijini Dar, na kuanza maisha mapya. Lakini hatukuchukua raundi, ndani ya mwezi mmoja tu. Ndio likatokea tukio hilo. Siku hiyo ilikuwa ni usiku mnene, sikumbuki ilikuwa ni wa saa ngapi. Ila nilikuwa sijapata usingizi bado. Hata dada angu alikuwa hajalala. Maana tulikuwa tunalala kitanda kimoja(mzungu wa nne). Pia tulikuwa tunalala na binti wa nyumba ya jirani, alimuomba bimkubwa ili atupe kampani maana tulikiwa wadogo kuliko yeye. Pia ni mwenyeji. Mimi kidume niko upande wangu kimya, nasubiria usingizi wakati wao wanapiga tu stori. Hapo tumeshazima taa yetu ya chemli. Nimekaaaa....mara ghafla nikashtuka naona mtu mweupe amesimama pembeni ya kitanda tena usawa wangu!! Nikashtuka, ila sikufanya chochote. Nikawa namtazama tu. Baadae nikamuona anaanza kutembea kukizunguka kitanda. Kapiga raundi moja kisha akakaa juu ya kingo za kitanda upande walikoweka vichwa dada na mwenzie. Mi namuangalia tu! Akapiga raundi ya pili, akakaa tena palepale! Ikabidi nimshtue sista,(nikamwita jina lake) mtu huyo!! Wakashtuka...wakaangaliaa...hawajaona kitu. Akanimaindi"hebu lala huko...usitusumbue!" Mmmh...nikaona hili balaa! Yaan mtu huyu hapa halafu wanasema hawamuoni! Itakuwaje?! Ikabidi nitulie tu...akapiga raundi ya tatu halafu akaja usawa wangu akiwa ukutani akasimama! Nikabaki nashangaa, kitanda kimegota hadi ukutani, huyu anawezaje kutembea bila shida?! Wakati najiuliza nikashangaa kuona ananisogezea mkono wake!! Akisogeza, na mimi nasogea kimyakimya... hadi nikafikia kwenye ukingo wa kitanda, yaani kinachofuata ni kudondoka!! Ujasiri ukanishinda, ikabidi nipige yowee...""baba mtuuuuu!!!" Hapo niko chini tayari!! Sista na mwenzie walivyoskia hivyo ikawa vurugu mechi, na lile giza. Ilikuwa ni mwendo wa kuparamiana tu!!!Dingilai alikurupuka geto kwake na taulo huku kashika panga huku bimkubwa akiwa nyuma yake! Kufika pale kuwasha chemli, akapekuwa hadi uvunguni. Wakaambulia chenga tu, nikawasimulia ilivyokuwa. Ingawa sista nae alidai walivyokurupuka walimuona kabla hajatoeka ingawa simuamini sana. Tangu siku hiyo wote tukawa tunalala chumba kimoja. Na yule binti akakataa kuja kulala. Wiki hiyo hiyo tukarudishwa kwa bibi, dingi akarudi hostel za chuo.
Na kisa kingine nilikutana nacho mwaka ya 2008, ingawa hakikunilenga mimi ila kiliashiria ulozi moja kwa moja. Mimi huwa nilikuwa na tabia ya kupenda kurudi usiku sana nyumbani. Utakuta nakaa home kuanzia asubuh, nafanya shughuli zote. Ila ikifika saa 10 jioni, ndio natoka. Na kurudi ni kuanzia saa 3 hadi 6. Sasa siku hiyo narudi zangu, mida ya saa 4 usiku. Njia ya mkato ina makaburi, naogopa. Njia ndefu kuna kakichaka karefu, kanatisha! Ila huwa napita bila shida. Ila siku hiyo nikajikuta tu naingiwa hofu! Ikabidi nipige moyo konde, maana lazima nirudi home. Basi nikatembea kwa kasi balaa, nikapanga nikikaribia karibu na hicho kichaka nipite kwa kasi ya upepo!! Basi nakaendaaa, nilipokaribia kichaka nywele na mwili vyote vikasisimka. Nikasema leo kazi ipo, nikajikoki...nikatoka nduki la hatari na nakimbia(huwa napenda). Kufika katika ya hicho kichaka nikakuta bonge la kinu limefunikwa!! Hiyo breki na kona niliyokata, Mungu tu ndiyo anajua. Na kipindi hicho nilikuwa niko vizuri kwa mazoezi. Sikugeuka nyuma hadi nyumbani. Niliwaza sana, karibu wiki nzima. Hizi ningekigonga na kubinuka ingekuwaje?! Baada ya mwezi nilimsimulia bimkubwa, alinisema sana! Nikapunguza kutembea usiku. Saa mbili niko home.
Walikuwa wanatwanga nyama za usiku huo ili zinoge vizuri ili siziwabughudhi wakati wa kula[emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nataka siku moja nipige tungi niwashe na kitu Cha R alafu saa sita usiku niende pale katikati ya makaburi ya kaloleni nikae kwa kutulia
Nione nitaona Nini Manake hizi stories nazisikiag tu oh Mara majitu,mashetani,vibwengu blah blah nyingi nataka nione live alafu nikikutana nalo niliulize kwanini wanatisha na kuua watu
Nenda ukiwa mzima!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupiga mtungi na kuvuta bangi inaonesha bado unauoga na hofu moyoni. Nenda ukiwa haujatumia hivyo vitu sababu ukiona halafu ukatoka nduki ukaenda kuwasimuliwa watu watakuona bangi na pombe ndizo zinakuchanganya. Hapo utakuwa umefuta ushahidi wote. Nenda ukiwa mzima. Uvute bangi na umelewa halafu uje uniambie umeona mchawi makaburini siwezi kukuelewa.

Wacha na Mimi niwape mkasa niliyoshuhudia katika mahakama moja miongoni mwa wilaya za Tanga.
Nikiwa katika harakati za kutekeleza majukumu ya kikazi nilipanga nyumba moja hivi iko vizuri tu.wapangaji tulikuwa watatu tu, baba mwenye nyumba Ni kijana mwenzetu ana mishe zake. Sasa bhana huyu baba mwenye nyumba kwenye biashara zake akafanya magumashi yaliyompelekea kushatakiwa na kufunguliwa kesi mahakamani. Kesi ilikuwa kubwa ya kumfunga kifungo kirefu tu. Kwa kuwa huyu baba mwenye nyumba tulikuwa tukielewana stori kwa Sana akanambia nimsindikize mahali kwa mganga. Tukaenda aisee tulipofika mganga akatueleza shida tuliyoendea kesi jinsi ilivyo na imebaki shahidi tu kuja kutoa ushahidi siku ya kesi jamaa ahukumiwe kwa namna yoyote jamaa hachomoki. Mganga akasema kanileteeni Nazi moja tu na si kitu kingine duh tukasema hapa hamna mganga. Tukaenda nunua Nazi tukampelekea, mganga akaandika maneno ya kiarabu kwenye ile Nazi kwa juu ikiwa haijapasuliwa ( maandishi yalikuwa ya rangi nyekundu). Kisha akasema saa 8 usiku ile Nazi ikapasuliwe njia panda ya kuelekea mahakamani.
Tuliporudi home tukawa tunasema mganga mzinguwaji kesi kubwa yy anatufanyia mzaha, basi saa nane usiku tukaenda njia panda ya kuelekea mahakamani jamaa jamaa akajifunga kaniki nyeusi Kisha akaipasua kama alivyoelekeza mganga.
Siku ya kesi ikafika ndipo nilipojuwa kuwa dunia no Zaidi ya tunavyoiona. Jamaa kafikishwa kizimbani kasomewa mashtaka kakataa akaitwa shahidi wa Kwanza, hakimu Kila swali akimuuliza shahidi anasema kasahau hakumbuki kitu, shahidi wa pili ndiye was muhimu Sana aisee jamaa alivyopanda kutoa ushahidi alikuwa bubu seriousky kudadeki acheni tu Kila akiulizwa anashindwa kuongea anabaki baaaa...baaaa...mmmm. Hakimu alidata akaahurisha kesi.
Siku tajwa ya kesi kufika hakuna shihidi alokuja Tena na Tena. Hakimu akafuta kesi na jamaa akawa huru.
Hivi vitu vipo aisee Ni mpaka ushuhudie ndiyo utaamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duhh, maninaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasilisha kama ilivyosimuliwa :

Kuna mwalimu Shule X, huko kanda ya ziwa, aliamka saa tisa usiku kuwahi usafiri asubiri gari kwenda mjini, kijiji cha ndani huko mkoa mpya uliopo ziwani.

Akasubiri gari na baada ya mda likaja, akasimamisha na kuingia. Gari ikaondoka, kakaa baada ya mda kumcheki abiria mwenzake kainama, akahisi labda ni usingz, lakini alipocheki waliopo nyuma pia dizaini kila mtu kainama. Akaona isiwe shida akamsemesha jamaa kainama tu kwa siti yake.

Sasa na yeye akatulia, gari imeenda lakini ghfla kama kausingz kakamwingia, akshtuka ghafla ni saa kumi na mbili asubuh na amesimama pale pale alipokuwa saa tisa kituoni.

Akapanic, kachukua baiskeli hadi wilayani hakurudi tena, ikabidi afisa elimu aende kule na timu yake kuongea na waalimu na wananchi ila jamaa hakuweza kukubali kurudi kituoni. In short walimpa uhamisho.

Nyingine mwalimu kapangiwa kituo Shule X huko kanda ya nyonyo. Kama ujuavyo vita ya kugombea mwalim binti mpya kati ya wanakijiji na wafanyakazi wenzake. Kumbe akawa kawakatalia, ikawa nongwa!

Siku moja anaosha ndizi kamaliza vizuri kwa sufuria, ghafla kikashuka kinyesi kingi kika replace ndizi zote, kinyesi fresh kinatoa hadi Moshi. Madam yule alikimbia kwenda kwa Bro nae ni mwalimu jirani Yake. Hakurudi tena kwa ile nyumba anaogopa.

Nina visa kama 10 kidogo ila mzembe kuhadithia.

Haya Mambo yapo kanda ya Nyonyo hasa kwa tuliokulia Bush huwa hata hatutetereki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana hawaendelei

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemkumbuka mwanangu pengo o level mkoa flan aliwahi kumuibia mzee mmoja iv km ustadh mwanangu pengo alikuwa kipofu yan haoni ndan ya week nzima huezi amini hospital walishindwa kujua tatizo, pongezi ticha mitomingi aka alijiongeza tukampeleka mwanetu kwa mtaalamu yai, nazi, sindano ndio vitu vilivyomfanya mwanangu aone tena ndan ya dk40. Tokea siku iyo nikiskia mtu ananiambia ntakuonyesha wew huwa nakuwa km piriton.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haha! Huyo jamaa huwa ananiacha hoi sana! Kuna siku kuna mwanamke alipandisha majini bhana! Wakaja viongozi wa dini kufanya kisomo. Si tulikuwa pembeni tunaangalia picha jinsi linavyokwenda. Yule jini akaanza huyu mwanamke nampenda siwezi kumuacha!

Huyo mshikaji si akanyanyuka bhana akamsogelea huyo mwanamke aliyepandisha majini. Jamaa akaanza; Nyie majini washenzi sana! Kwenu hamna mademu! Unampenda unampenda nani rudi kwenu huko!
hahahahahah kuna watu waniona kama chizi hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa kingine nilikisikia kilitokea maeneo ya sumbawanga

Kuna mzee wamakamo alikua ni tajiri sana, pesa zake haweki benk na hata akienda kufanya manunuzi hua haweki kwenye wallet kuzistiri zisionekane yeye hua anazishikilia tu kama wanafunzi wanavyoshika vitini vyao mikononi

Siku moja kuna kosi la majambazi lilijipanga kwenda kumvamia

Walimkuta yuko nyumbani kwake ameshikilia pesa akipata upepo kwenye garden yake

Wakamnyooshea bastola na kumwambia atulie kimya kisha atoe kila kitu alichonacho

Yule mzee akachukua zile pesa akazibana kwenye kwapa lake huku akitetemeka kwa woga

majambazi wakamsisitiza kua anyanyue mikono juu, mzee akatii amri kwa kunyanyua mikono juu kisha pesa alizozibana kwapani zikaanguka chini majambazi wakaziokota

Wakamwambia tena "toa kila kitu ulichonacho"

Round hii unaambiwa mzee alichomoa kichwa chake akakishika mkononi halafu kile kichwa kikiwa mkononi kikatoa sauti ikisema "sina chochote jamani nina kichwa tu hapa"
🤣 🤣 🤣 🤣🤣Hapo walizimia na bastola zao..
 
UKITAKA KUWAONA WACHAWI (Hii Dawa ni hatari kama hauna kinga ya kutosha mwilini tafadhali usijaribu kabisa)

jua kabisa jambo hili ni hiyari yako lakin ni zuri sana kama utalifanya kwa hakii basi fanya yafuatayo,chukua Muhogo wa aina ya Kisamvu Mpira (Muhogo Mpira) majani yake pamoja na Majani ya mbaazi Hayo Majani ya aina 2 twanga kwa pamoja kisha kamua maji yake unawe usoni wakati wa usiku mwingi hakika utaona ajabuu sana utawaona wachawi wote wanao kusumbuwa usiku.
Mkuu shikamoo[emoji44]..heshima kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nakumbuka siku moja nimetoka kula chakula usiku, mida ya sa mbili, kuingia chumbani kitandani ile nalala kabla sijafumba macho nilijiona napaa live juu ya kitanda mara tatu.....nkakemea kwa jina la yesu nkaachiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu umesahau na maandaz hapa[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jirani yangu kuna siku alikuwa ananisimulia alikuwa anasafiri na broo wake usiku walikuwa kwenye gari yao. Safari ilivyokuwa inachanganya mbele wakamuona mtu kwa mbali kama anasimamisha gari. Kumuangalia vizuri kumbe ni mwanamke, halafu ni mrembo tu! Dogo akamwambia bro huyu mwanamke atakuwa jini tu haiwezekani usiku huu wote asimame njiani peke yake, tumpite tu.

Brother yake akamwambia usihofu. Akasimamisha gari. Akamwambie ndio mrembo! Yule mwanamke akamwambia naombeni lift nimekwama huu usiku naelekea eneo fulani. Brother yake akamwambia yule mwanamke ingia. Safari inachanja mbuga brother yake akaanza kumwambia yule mwanamke. Inakuaje unatusumbua unasimamisha gari wakati eneo unalotaka kwenda unaouwezo wa kufika?

Yule mwanamke akajibu sielewi unachozungumza. Brother yake akamwambia yule mwanamke, usi' panic! Sisi tuliokupa lift tunajua kwamba wewe ni jini! Ndiyo tunakuuliza kwa nini umetusumbua kusimamisha gari wakati kufika eneo unalotaka uwezo huo unao wewe kama wewe?

Yule mwanamke akawaambia simamisheni gari! Majamaa wakasimamisha. Wakasikia mlango wa siti ya nyuma unafunguliwa. Kugeuka yule mwanamke hawamuoni tena! Brother yake akasema, unatusumbua wakati uwezo wa kufika unao. Wakaendelea na safari.

Nikamuuliza sa mbona huyo jini katumia style ya zamani sana? Jamaa akanijibu, majini ni wapumbavu wapumbavu tu.
Hahaha ....dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anasimulia dereva wa Fuso Jangwani.

Hiyo siku wamekaa maskani kama kawaida wakisubiri wateja, haukupita muda akaja mzee wa kiarabu hivi(mburushi).

Mzee akaulizia huduma ya kupelekewa mizigo yake wanapopandia boti za kwenda Mafia, wapo waliomkatalia, akajitokeza kidume, akamwambia mzee twende. Akamwambia kuna vity vyangu nimenunua vingi viko Kariakoo, twende tuvipitie, swala la muda lisikupe tabu, nitakulipa kijana.

Huyu alikuwa ni mzee wa makamo kidogo, basi jamaa mpaka Kkoo, wakapakia safari ikaanza. Kufika pa kupandia boti, mzee akamwambia dereva sasa kijana wangu naomba unielewe hili, naomba twende nyumbani tuvuke pamoja nikakupe pesa yako, swala la muda wa kukuweka huku isikupe tabu. Dereva keshayavulia tena ikabidi akubali tu, safari ikaanza. Wamekwenda, boti ikafika pahala ni kwenye maji bado, yule mzee akamwambia muendeshaji kuwa simamisha hapo mi nimefika.

Kila mtu mle ndani haamin mzee anachokisema, mzee akawaambia simamisha, kweli nahodha wa chombo akatii, mzee akakuta wameshamsubiri tayari vijana wake, wakaanza kupakua mzigo ukaisha boti ikaendelea na safari. Sasa yule dereva akaamua kuwa mpole tu, akaambiwa na yule mzee kwa ukarimu kabisa, usiogope kijana karibu nyumbani, yule jomba akashukuru, wakaingia ndani, kwanza aliposhuka toka chomboni akaona bonge moja la mji, hajawahi fikiria kuliona. Kakirimiwa vizuri, akaambiwa ukitaka kuoa, njoo tu huku nina mabinti zangu hawajaolewa usiogope. Jamaa akapewa pesa yake akapelekwa pale pale aliposhukia akapandishwa chomboni mpaka ng'ambo. Baada ya tukio lile yule jomba hata umwambie nina mzigo nipelekee Temeke, humpeleki.
 
Hahahaaha kubaababke hata mimi sipeleki hata Buza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom