thewajibu
JF-Expert Member
- Jan 14, 2017
- 236
- 306
Pole mkuu juzi tu tarehe 26 nilikuwa Bukokwa hadi sukuma ni kwa mara ya kwanza tangu nizaliwe nilivyoyaona hayo mazingira yalivyo na wasukuma wengi nilihisi kutakuwa na uchawi mwingi
Sent using Jamii Forums mobile app
Uchawi ni kweli Upo, Nikiwa Nimeenda Kurudia Shule Baada ya kukosa Nafasi ya kujiunga Form One 1994..Baba yangu Mkubwa..Tumbo moja na Baba Alikuwa anafundisha Shule ya Msingi Nyabhutanga Jimbo La Buchosa wilaya ya Sengerema 1990--1995.. Mzee wangu Alikuwa Anatembeza Bakora kama hana Akili nzuri siku moja Akachapa mwanafunzi wa Darasa la 6 na inasemekana Alikuwa hachapwi na walimu sababu ya Mama yake kuogopwa kwa Uchawi.. sasa baada ya Kwenda kushitaki kwa Mother yake, Saa 2 Usiku mother mtu Alikuja kumuonya Mzee wangu Home Asirudie tena kumchapa Binti yake.. Mzee Akamwambia Asimtishe na Asirudie tena kuja kumletea vitisho..
Siku nyingine tena Miezi kama 3 Baada ya Tukio la mwanzo.. Yule Binti sijui Alikosea nini bhana Mzee Akamcharaza tena Bakora za Kutosha, mother usiku saa 1 Akaibuka home Kwetu Akamfokea sana Mzee wangu na kumuonya tena, Sasa Ba mkubwa Alivyokuwa mbishi sijui nini kilimpa si Akamdaka yule mother Akaanza kumtembezea Bakora za kutosha hadi walimu Jirani wanakuja kuamua Alikuwa Amemvuruga sana.. Hakwenda Polisi wala Hospital Alijiuguza hadi Akapona.. mwisho kwa Ile Fedheha Akahama Kijiji. Lakini mwaka Mmoja Baadae Ba mkubwa Akiwa Anakunywa Pombe kijiji Jirani cha Bukokwa Alishangaa Kumuona Yule mother Akiwa miongoni mwa wahudumu, Akashangaa Sana Ile bado Akiwa hajui La kufanya Akamwambia Afanye Matengenezo ya maisha yake Kisha ghafla kama upepo Akapotea.. Ba mkubwa Akiwa na Pombe kidogo kichwani Alimpuuza Lakini Alikuja Kutusimulia Kesho yake..
Baada ya Mwezi mmoja Ba mkubwa Akiwa Anatoka Kijiji cha Sukuma Akija Nyabhutanga Usiku Kama Saa 6 hivi Akiwa Anaendesha Baiskeli Ghafla Aliona Fuso Linakuja kwa kasi(Na kwa siku hiyo huo muda Hakuna Gari lilikokuja hapo kijijini kwa muda huo) Alijaribu kulikwepa na Kuishia kuanguka na kupoteza Faham. Alikaa Sengerema Hosptl miezi 3 baadae Tukamhamishia Bugando..Baada ya miezi 3 Akiwa Bugando Hospital Alifariki.. Huwa Naumia sana Kila nikitafakari tukio Hilo Maana Nilikuwa Nasomea Hapo kwake na Ndo Alikuwa kila kitu kwangu kwa wakati huo..
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app