Anasimulia dereva wa Fuso Jangwani.
Hiyo siku wamekaa maskani kama kawaida wakisubiri wateja, haukupita muda akaja mzee wa kiarabu hivi(mburushi).
Mzee akaulizia huduma ya kupelekewa mizigo yake wanapopandia boti za kwenda Mafia, wapo waliomkatalia, akajitokeza kidume, akamwambia mzee twende. Akamwambia kuna vity vyangu nimenunua vingi viko Kariakoo, twende tuvipitie, swala la muda lisikupe tabu, nitakulipa kijana.
Huyu alikuwa ni mzee wa makamo kidogo, basi jamaa mpaka Kkoo, wakapakia safari ikaanza. Kufika pa kupandia boti, mzee akamwambia dereva sasa kijana wangu naomba unielewe hili, naomba twende nyumbani tuvuke pamoja nikakupe pesa yako, swala la muda wa kukuweka huku isikupe tabu. Dereva keshayavulia tena ikabidi akubali tu, safari ikaanza. Wamekwenda, boti ikafika pahala ni kwenye maji bado, yule mzee akamwambia muendeshaji kuwa simamisha hapo mi nimefika.
Kila mtu mle ndani haamin mzee anachokisema, mzee akawaambia simamisha, kweli nahodha wa chombo akatii, mzee akakuta wameshamsubiri tayari vijana wake, wakaanza kupakua mzigo ukaisha boti ikaendelea na safari. Sasa yule dereva akaamua kuwa mpole tu, akaambiwa na yule mzee kwa ukarimu kabisa, usiogope kijana karibu nyumbani, yule jomba akashukuru, wakaingia ndani, kwanza aliposhuka toka chomboni akaona bonge moja la mji, hajawahi fikiria kuliona. Kakirimiwa vizuri, akaambiwa ukitaka kuoa, njoo tu huku nina mabinti zangu hawajaolewa usiogope. Jamaa akapewa pesa yake akapelekwa pale pale aliposhukia akapandishwa chomboni mpaka ng'ambo. Baada ya tukio lile yule jomba hata umwambie nina mzigo nipelekee Temeke, humpeleki.