Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Salange, Hii,nishawahi kusikia watu wanaazima meno yako na kwenda kutafunia nyama huko na baadaye unarejeshewa, sometimes naskia unaweza rudishiwa yakiwa hayajasafishwa vizuri,ukiamka asubuhi meno yana damu damu + nyama nyama ,wakati usiku huo ulikula maharage[emoji3][emoji3] sayansi zipo hizi jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
ngoja tu nimalizie kisa changu kingine,but huwa nikimsikia mtu anasema uchawi hakuna namwangalia na kutikisa kichwa tu.
Nimezaliwa na mama ambae ni mgonjwa wa sicle cell hali iliyokuwa inamfanya mama yangu kuumwa mara kwa mara hasa mifupa na hata kuishiwa damu mara kwa mara naweza kusema mama yangu haikuwahi kupita week bila ya kuumwa au kulazwa hospitali,hali iliyopelekea kuwa anatumia mara kwa mara dawa za valium na hata wakati mwengine kuwa anajichoma mwenyewe sindano za valium ili apunguze maumivu apate usingizi,ilikuwa ni usiku wa saa 8 usiku nimelala na bimkubwa naskia anaugulia maumivu makali mno ya mifupa,nikaanza kutafuta dawa hakuna sindano wala vidonge na nyumba tulikuwa mimi na yeye tu wakati huo simu ni anasa na usafiri huu wa boda boda hakuna na gari ilikuwa saa 4 mwisho, basi kila akiugulia maumivu akili yangu inahangaika mwisho wa siku nikamchukua nikamuweka mgongoni kulikuwa kuna dispensari fulani hvi ipo kigoma ujiji na sisi wakati huo tunakaa bimala kwa wenyeji wa kigoma wanakujua ni umbali wa kama dakika 10 kwa gari,basi nikamuweka mama yangu mgongoni safari ikaanza wakati huo nina umri wa miaka 12 tu,tembea sana kila nikiskia anazidi kuugumia na mm ndo naongeza spidi,basi tukafika sehemu moja inaitwa shine cinema ni ukumbi fulani hivi walikuwa wanaonyesha movies na pembeni kuna shule ya msingi ujiji, baada ya kufika pale ile shule tuliona imegeuka treni watu wanashuka na kupanda wakati huo upande wa pili kwenye ule ukumbi kwa nje tukaona watu wengi mno wapo nje wanapiga kelele mno wanasherehekea wako uchi wa mnyama wanauza vichwa vya watu ulimi na viungo vingne vya binadamu na kulikuwa kunanuka damu kweli kweli cha ajabu ajabu kufika pale nikashikwa na bumbuwazi kiasi cha kanga kulegea bimkubwa akaanguka lakini kwa kusimama sasa alivyofungua macho kuona kilichopo mbele yetu nilishangaa tu amenibeba juu alitoka mbio za ajabu huku akiwa amenibeba mgongoni mpaka ujiji kwenye ile dispensary alivyofika tu akazimia pale pale nakumbuka alikuja kuzinduka siku ya tatu na mtu wa kwanza kuniita alivyoamka tu nilikuwa mimi alinikumbatia na kuanza kulia sana(kisha akanitamkia nimekusamehe leo na siku zote za maisha yako) kauli hii aliirudia akiwa anafariki ndani ya mikono yangu mwaka 2007 kwa kunambia(nakufa mwanangu nakupenda sana na nakufa nikiwa radhi nawe uishi maisha ya kumpendeza mungu na uwapenda nduguzo kama ulivyokuwa unanipenda mama yako)
R.I.P my beloved mom

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana kamanda.......!!! daaah!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguvu za Giza zipo aisee.

Nilikuwa nasoma chuo some where sehemu ambayo tunaishi kulikuwa kuna shida ya maji na maranyingi yanatoka usiku.

Siku hiyo yakaanza kutoka wanachuo wenzangu wakatoka njee maana bomba lilikuwa njee wakaanza kuchota maji ilikuwa SAA nane usiku nikatoka na Mimi

Sasa ile hostel ilikuwa karibu kabisa na main road nikaona mfano wa gari lakini linawaka likapita kwa road baadae kidogo nikaona kitu mfano wa kisicho naumbo maalum kinawaka mfano wa nyota kimebeba mkuki kinazunguka ile nyumba nawaangalia washkaji hawana habari kila nikitumia njia zakuwazuia jamaa wasiendelee kuchota maji wao wanaendelea kuchota Mimi nikaamua kurudi ndani ilipofika asubuhi nikaawambia wanafunzi wenzangu ikawa ndo mwisho wa kuchota maji usiku nakuishia kunipongeza kutowaambia usiku ule maana ingekuwa balaa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kitu hapa ni uongo tena uongo wa hali ya juu.

Tunasafari ndefu sana na hivi visa vyenu vya kufikirika

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Mungu anathibisha uchawi upo kwenye maandiko, wewe ni nani nikuamini kuwa uchawi hakuna?? Mimi nimeshuhudiwa mambo mengi sana kwa macho ya Damu na Nyama mkuu.. Mungu akusaidie husije ukaangukia kwa hao watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna kitu ni chai tu hizo na magonjwa ya akili.... maandiko gani bana wewe,vile ni vitabu vya hadithi za kale tu hamna cha maana mule
Kama Mungu anathibisha uchawi upo kwenye maandiko, wewe ni nani nikuamini kuwa uchawi hakuna?? Mimi nimeshuhudiwa mambo mengi sana kwa macho ya Damu na Nyama mkuu.. Mungu akusaidie husije ukaangukia kwa hao watu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom