Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kwa kesi ya housegal wangu. .Wakati anaombewa aliongea mambo mengi sana yanayofanywa na wachawi duniani na kuzimu huko. .

Alisema kwa wale wanaokufa kwa kuchukuliwa kiuchawi na badae kuonekana/ kurudi kwenye Jamii inakua kwamba wengine wanashindwa vyakula vya huko kuzimu kabisa na wanakua na mizimu mikali sana yani ile too much ambayo kila kitu yahuko kuzimu haipatani nayo haiitaki yani mzukule hata apigwe vipi hata afanywe nini hali ngo'o akiambiwa afanye hiki hafanyi wee fanya ufanyavo mzukule anagoma kabisa mwisho wanaamua kumrudisha duniani. ..wanamrudishaje sasa hilo hakuongelea .... Au wale wanaoshindwa kutimiza mara nyingi wanayoagizwa na wakuu wao huko kuzimu yani wale vilazaaaaaa kama huyo binti yangu wakazi . Alionekana kuwa mzito sana kufuata maekekezo .
Alipofika kwangu tu mkuu wao wa uchawi aliona mtoto mchanga wa kiume wa mdogo wangu niliyekuwa naishi nae eti ana damu, nyota nzuri, pamoja na nguvu sana yani nguvu NYINGI SANAAAAAAAA Kumbe housegel huyo alikua duniani kama agent tu wa kuua watu kuwafanya mizukule, kuwatafutia damu na nyama za watu wakuu wao huko kuzimu. . Na alishaelekezwa mara kibao afanye nini tangu alipofika hapo kwangu kwa ajili ya kumuua huyo mtoto mchanga by that ime. Alipewa dawa za kumpa na kumuwekea ka changa hako lakini binti hakuweza kufanya hivo na alikua anamuonea imani huyo dada na roho inamuuma sana Kwani walikua wa naishi vizuri hapo nyumbani kwangu . shortly alikua kama ndugu yetu. Nayeye ndiye aliekua anashinda nyumbani akiwahudumia mama na mtoto muda mwingi mimi nikiwa kazini Sasa sijui kama ni kweli au laa but nimeshuhudia hayo na mpaka Leo naishi nao mama na mtoto

Katika uhalisia huyo mtoto wa mdogo wangu ana nguvu sijawahi ona. . Hata Ukimbeba ni mzito jamani jamani na ana akili sana. .Ni mtoto mdogo ila ukimuangalia mambo yake mwenyewe unabaki mdomo wazi.
Pia kwa matendo yake naezasema Ni wale talented ones

Ni story ndefu yenye mengi.
ThanksGod

Cc Smart911

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia mkuu nahitaji maombi make ukweni kwa dogo walitaka kumchukua mtoto kichawi na kumfundisha uchawi mama yake ili wawe wanaruka kuwanga na Kufanya mambo yao ya uchawi pamoja ila tangu yalipotokea hayo mauzauza na kujua hayo kupitia kanisani nilimpiga stop dogo kutokanyaga ukweni ila ukweni wanadai wanataka kumuona mtoto wao eti damu yao huwa haiendi mbali. .ni changamoto sana na story ndefu hapa nakatisha katisha tu
Wachawi wanajuana
Kwa kesi ya dogo wangu kuna

1. Wifi yake ambae ni mkuu wa wachawi
2.aliekuwa housegel wangu wakazi ambae nilimtafuta pindi dogo anataka kujifungua na kama bahati tu nilimwambia aje kujifungulia kwangu na si ukweni alikotaka kujifungulia huko.
Acheni mungu aitwe mungu.

Cc Smart911

Mkuu habari yako.... ninaweza kukusaidia kwa maombi (kama upo mkoa wang) au kukuelekeza jinsi ya kusali ni rahisi sana sema tu Ur Mam inabidi awe tayari kusali na kuwa na imani.....

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko insta kuna page za maombi moja inaitwa anointed-room nyingine bishopemmanuel. Angalieni kama maombi yao yatawafaa
Mimi pia mkuu nahitaji maombi make ukweni kwa dogo walitaka kumchukua mtoto kichawi na kumfundisha uchawi mama yake ili wawe wanaruka kuwanga na Kufanya mambo yao ya uchawi pamoja ila tangu yalipotokea hayo mauzauza na kujua hayo kupitia kanisani nilimpiga stop dogo kutokanyaga ukweni ila ukweni wanadai wanataka kumuona mtoto wao eti damu yao huwa haiendi mbali. .ni changamoto sana na story ndefu hapa nakatisha katisha tu
Wachawi wanajuana
Kwa kesi ya dogo wangu kuna

1. Wifi yake ambae ni mkuu wa wachawi
2.aliekuwa housegel wangu wakazi ambae nilimtafuta pindi dogo anataka kujifungua na kama bahati tu nilimwambia aje kujifungulia kwangu na si ukweni alikotaka kujifungulia huko.
Acheni mungu aitwe mungu.

Cc Smart911



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi binti yangu nkiniombea kitu kwa Mungu napata yaani mpaka huwa tunashangaa sana na mkewangu ni mdogo muaka mi nne tu ila huwa anaomba utamsikia Mungu naomba baba apate ela aweke mafuta atupeleke mikumi aisee keshoyake hata iweje lazima nipate pesa yakutosha tu ni mengi sana kanifanyia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu namimi naomba umwambie aniombee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu nisimulie hiki kisa changu...

Jumanne 23-08-2019.

Ilikuwa saa nne na nusu usiku nikiwa nimeketi sebuleni,mara gafula mzee akatoka chumbani na kuanza kunitukana matusi ya nguoni...

"Kijana gani wewe kazi kula na kujaza choo,huoni wenzio wanafanya kazi na wanategemewa na wazazi wao...ni bora ningezaa hata mbuzi ningefaidi mchuzi.."


Mara ghafula nashutuka kofi hili hapa sijakaa vizuri ngumi hii hapa,nikasimama imara na kumkazia tu macho...wadogo zangu na mama yangu wakitazama tu pasi na kusema neno.

Nikageuka taratibu na kutoka nje,chozi la uchungu likanitoka ilikuwa ni siku mbili tu toka nifukuzwe shule moja niliyokwenda kuomba ajira ya kujitolea..ati hawawezi kuajiri kiziwi!.

Nilitazama anga jeusi lililosheheni nyota nyingi,mwezi uliotoa nuru angavu nikajiuliza "Mungu upo wapi?".. Nikaingia chumbani na kuvaa viatu.. Nikatoka naenda wapi? Sijui!

Nikaambaa nisijue kama nakanyaga ardhi au ninapaa,napishana na mtu ama kisiki,ilinichukua nusu saa kuuacha mtaa wetu nikaingia mtaa wa pili,huu ulikuwa na watu wachache zaidi na nyumba zilikuwa mbalimbali kiasi.


Nikakatiza pembeni ya makaburi,nikasimama,nikayatazama na kujiuliza " kwanini nisingekuwa nimelala pale? Nipumzike!"...loooh lakini sauti nyingine ikaniambia "una uhakika ukilala pale utapumzika? Nikagutuka nikatazama huku na huko hakuna kiumbe nikaongoza njia kuliacha eneo la makaburi na kuzidi kupotelea mbali zaidi na nyumbani.


Hatimaye nikawasili sehemu pweke,barabara kubwa ya kokoto,kulia na kushoto kukiwa na msitu na vichaka vingi,kiza ni kingi kutupia macho simu yangu ni saa sita na robo usiku!

Ikafika mahali kuna njia panda na upande wa kulia kuna mti mkubwa sana aina ya mbuyu mahali pana pana joto sana bwana,pana joto kali,mapigo ya moyo yakanienda mbio " duuucha dunduncha ducha dunduncha" sasa mapigo niliyasikia hadi masikioni..

Nywele zikanisimama na vipele vya uoga vikanitoka hewa ikawa nzito na uvumilivu ukaniisha na sasa nikatimua mbio hata nilipoliacha eneo lile kwa umbali wa mita mia mbili hivi,na sasa nikaanza kutoka katika makazi ya watu.

Kufika hapa ikanipasa kujiuliza ni wapi naelekea,sikuwa napajua napoelekea kumbukumbu ya misukosuko ya kimaisha na masimango yasiyoisha zikanijia,woga wote ukabiisha donge zito la uchungu,hasira na kukata tamaa likanivaa,machozi yakanitoka,nikashika njia na kuendelea na safari,safari isiyojulikana!


Baada ya mwendo wa dakika ishirini hivi nikaingia katika barabara kubwa ya lami,nikashika uelekeo wa kushoto,ilielekea ufukweni,baada ya masaa mawili hatimaye nikawasili ufukweni,nikazitupia macho hoteli kadhaa zilizotamalaki eneo lile,nikaachana nazo na kushuka mchangani mbali kidogi na mahoteli yale,nikajikalisha kitako na kutafakari nilipotoka,nilupo na ninapoelekea,lakini mbona mbele kyna kiza kizito!


KIZAAZAA!

Hatimaye saa tisa ikawadia,nilichoka,na sasa ilikuwa ni safari ya kurudi,nikajizoa zoa na kushika njia kurudi nyumbani,bahati nzuri barabara hii ilikuwa na taa hivyo ikawa ahueni kwangu.


Baada ya mwendo wa dakika arobaini hivi nikahisi kama kwamba kulikuwa na mtu nyuma yangu,nikageuka kwa kasi, ebo! Nikaona nguo ya rangi ya khaki,aidha gauni au kanzu ikiishia na kufutika machoni kwangu....

Mshtuko uluonipata ukanifanya hata nguvu za miguu ziniishie nikajikuta nikiketi katika mfereji mfupi uliojengwa pembeni ya barabara.

"Ni nini hiki? Ni kweli au ni mawazo yangu tu?" Nikajiuliza,nukatazama huku na huko hali ni shwari,labda niliangalia vibaya bwana nikajizoazoa na kuendelea na safari..

Kiroja kingine tena! Ati nina vivuli viwili,kimoja ni changu na kimoja kimevaa kanzu kama si gauni!(mataa ya barabarani yanawaka hivyo mtu akipita kivuli chake kinaonekana kwa ufasaha kabisa) nikatetemeka kwa woga,nikageuka nyuma ati nacho kikageuka! Nikawa natembea kwa kurudi kinyume nyume,ati nacho kinarudi kinyume nyume!.

Lakini mbona kivuli changu kupo mbele yangu hiki cha nyuma ni cha nani? Na tumeachana umbali wa hatua kama tatu hivi toka kilipo hadi nilipo,nikaona huu sasa utani,nikifa si nife tu ebo! Nikakata shauri kukifuata he! Ati nacho kinageuza kila nikikifuata nacho kinaenda nyuma zaidi,ikabidi nikikimbize sasa..kikapotea.

Nikageuka na kuanza kukimbia kwa taratibu mithiri ya mbio za riadha,nikachoka nikaanza kutembea baada ya mwemdo mrefu kivuli kile kikarudi! Sikusimama nikaendelea kutembea tu.

Hata hivyo nikaanza kuhisi mwili kuchoka sana,miguu inauma na usingizi ni mwingi sana,nikajikalisha juu ya ukingo wa karavati kutafuta pumzi maana ilikuwa ni safari ya masaa mawili zaidi hadi nifike nyumbani...nikaanza kusinzia na hatinaye fahamu zikakomea hapo.


Kelele za watoto wakicheza ndizo zilizonigutusha,nikafumbua macho..afanalek! Nilikuwa nimelala chumbani kwangu..miguu ilikuwa imevimba kiasi na mwili mzima ulikuwa unaniuma...


"Lakini mimi mbona nilikuwa kule barabarani?" Nikajiuliza nisijue kilichotokea,nikaamka na kulibinua bati ninalotumia kama mlango,nikapenyeza kiubavuubavu hadi nje.

Nikawatazama nyusoni niliowakuta nje,wapo kawaida,hawana hata habari,pengine niliokotwa na wasamaria wema! Lakini mbona watu wapo kawaida kama hakuna kitu?...nikashindwa kuvumilia nikaamua kumuuliza mama ni muda gani niliingia kulala!

Akanijibu "we si uliingia kulala saa nne weww? Maswali gani hayo usinisumbue" ni nani aloyenirudisha nyumbani,na kile kivuli ni kiumbe gani? Je ndicho kilichonirudisha nyumbani? Lakini hakijanidhuru, hili ni fumbo niishilo nalo hata sasa kuna wakati natamani kukiona tena kivuli kile kilichovalia kanzu au gauni lililopauka lakini hakitokei tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mhuu interesting

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saint anne Ushawahi kuona moto unawaka kitandani na hakuna alieuwasha? ? Na kitanda hakijaungua? ? Kitanda kinatikisika hakuna alietikisa earthquake ikasome Ushawahi ona? ? Ile umekaa na Kachanga kitandani mara vuup unaona kama shoti imepiga kitandani mara tatu. Paaaa moto unawaka unazima unawaka unazima na kitanda chumba chote kama tsunami inapiga Umewahi ona????!!
It happened nyumbani kwangu ...

Ilikua hivi. .
Kachanga kalipozaliwa tu ndipo kasheshe likipoanzia. Baada ya kujifungua tu dogo usiku alikua anaota kama ndoto ambazo kumbe hazikuwa ndoto bali ni uhalisia alikua anaota kama kuna mtu anakuja usiku anakua anamziba pua hivi na kumfanyia vitu ambayo wakati huo yeye anaona kabisa kama anafanyiwa ila akitaka kupiga kelele kuomba msaada hakuna anayemsikia yani sauti haitoki. .taka kupiga kelele za msaada wapi. .hata akitaka kumwita anaelala nae chumba kimoja hawezi.
Akiamka asubuhi ananihadithia kuwa dada tangu nilipojifungua usiku usiku natokewa nahivi na vile. .Mi nikawa namwambia kuna nguvu za giza zinakufatilia. .inaonekana zilikutafuta sana tangu ukiwa mjamzito lakini hazikufanikiwa stil zinakufatilia. Sali sana dogo dunia ina mambo mengi. (Nina imani kali sana mimi yani moyo wangu ukikataa kitu lazima kinakua hovyo au cha majanga yani ninachodoubt mara nyingi huwa hivo hivo kama nilivohisi )
Ikaendaa Ikaendaaa muvi yenyewe ilikua siku mtoto ametimiza mwezi mmoja kamili yani the same tarehe amezaliwa mwezi uliopita wakuuuuu. .omba yasikukute kumbe Tarehe 15 kuamkia 16 ndipo wifi mtu( mkuu wa wachawi na team yake walikuja kumchukua mtoto na hapo nyuma housegal alikua ameshampa dawa mtoto nyingine alishamnywesha na kuwafanyia vitu kadhaa kwa kulazimishwa nahuyo wifimtu . Walijuanaje mimi mwenyewe nilishangaa sana.)Kwani baada ya wiki kadhaa ndiye aliyekua anawahudumia mama na mtoto
Mtoto alizaliwa tarehe 16 sasa Ile tarehe 15 usiku wakati tumelala dogo aliona kama kuna mtu ambae alikua ni mdada alikuja na kuwa kama anachukua mkono wa dogo ( mamamtu) na kuupeleka shingoni kwa Kachanga dizain kama anamlazimisha mamamtu amkabe mtoto..dogo akawa anatoa mkono ile ya kukataa huyo dada anamlazimisha kumkaba mtoto dogo anagoma vutana vutana dogo anaishiwa nguvu badae akashtuka na kumuangalia mwanae mtoto alikua analia sanaaaaaaaa. . Akasali na kulala asubuhi akaja kuniambia tena dada usiku nimetokewa na hivi. .
Ile kunisimulia nami nikakumbuka usiku huo huo wa tarehe 15 kuamkia 16 niliota ndoto kuwa mtoto( Kachanga ) gafla amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha na mama yake yupo ukweni ila amekondaaaaa ngozi imekua kama mzee. .Hapo ukweni ndugu zake tumeenda kumuona ndugu yetu ila tunaona wanapitisha sahani zenye mapaja ya nyama za watu yaliyochomwa paja jekunduuuuu mara mikono ya watu lakini kama nyama ambazo watu wanakula. The same night kuna dada yetu mwingine yeye aliota mtoto wa dogo amefariki ila anaonekana yupo dirishani kwenye chumba fulani.
Niliposikia hayo ya dogo nikaunganisha ile ndoto yangu nilishtuka sana nikamwambia dogo jiandae leo mchana tunaenda kwa mchungaji hii hali si ya kawaida.
Ukapita mchana wote jioni imefika usiku saa 2 kasoro ndio nikashtuka OMG mbona hatukwenda kanisani kwa mchungaji? ? Nikamwambia dogo sasahivi vaa muache mtoto twende kanisani mara moja Kwani alijifungua kwa oparesheni. .na ndokwanza alikua anatimiza mwezi mmoja. Dogo akawa anasema aaahhh dada bwana usiku umeingia tutaenda kesho. .mimi roho ilikataa kabisa nikamlazimisha vaa twende anasema tutaenda kesho asubuhi dada roho iligoma kabisa nilisema hapana moyo wangu umegoma kulala leo bila kwenda kwa mchungaji huwezi jua .usiku mkubwa na roho haikubali kabisa kuacha kwenda
Akavaa tukaenda hapo saa mbili usiku..tukaenda hatukumkuta mchungaji tukamsubiri
Dada akamuhadithia kwa ufupi tu mchungaji akasema kwakua ni usiku wacha nimuombee kidogo ili awahi mtoto si akaanza kuomba troooobaaaa....
Dogo alikua kama wale wenye mapepo

NITAENDELEA KESHO NIKIPATA MUDA

Cc Smart911



Sent using Jamii Forums mobile app
 

kumbe ndiomana watu wengi wakianguka chooni wengi sijui wanakuaje hata. .Wengine wanakufa.
Yani huyo houseg alisema mengi sana na wakati dogo anaombewa kule kanisani nguvu yamungu ikifanya kazi hadi moto kuwaka kitandani alipokuwa amelala mtoto binti wakazi alikua ameenda chooni kuwasiliana na mkuu wao Kwani tayari reaction walishaipata kupitia yale maombezi ..hizi ajali nyingine ni Shetani yuko kazini. . Mnaona ajali kumbe mkuu keshapuliza tu puuu dakika sifuri midamu hioo barabarani anatuma watu wake wengine waje kuchukua damu wengine wabebe miili huku huko kuzimu wengine wanakua wanachemsha maji ya kupika hizo nyama zinazoletwa kutoka kwenye ajali endapo huyo hao mlengwa atakuwa ni wa kuliwa nyama kwani Wengine wanafanywa mizukule tu yakufanya kazi zao.

MY GOD IS LIVING AND HE LOVES ME AND MY FAMILY

Cc Smart911
 
hizi ni mambo za kiwaki dadeq zenu mnatulisha matango pori inamaana mnataka kusema kuwa hivyo vitu haviwezekan bila kuvihusisha na hizo nguvu zenu za uchawi/';`1
 
Mimi binti yangu nkiniombea kitu kwa Mungu napata yaani mpaka huwa tunashangaa sana na mkewangu ni mdogo muaka mi nne tu ila huwa anaomba utamsikia Mungu naomba baba apate ela aweke mafuta atupeleke mikumi aisee keshoyake hata iweje lazima nipate pesa yakutosha tu ni mengi sana kanifanyia.

Sent using Jamii Forums mobile app
hii chai naona majani yamezid kidgo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bibi yangu ni mchawi, anamtesa sana Mama yangu, anataka kumuua. Ni muda sasa mama anateseka na maradhi yasiyo pona. Tumezunguka sana... ila basi tu
Mpelekeni kwenye maombi hafu naye aamini kwamba anapokea uponyaji.......Na atenge muda wa kusoma vitabu vitakatifu kulingana na iman aliyonayo mkristo au muislam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi binti yangu nkiniombea kitu kwa Mungu napata yaani mpaka huwa tunashangaa sana na mkewangu ni mdogo muaka mi nne tu ila huwa anaomba utamsikia Mungu naomba baba apate ela aweke mafuta atupeleke mikumi aisee keshoyake hata iweje lazima nipate pesa yakutosha tu ni mengi sana kanifanyia.

Sent using Jamii Forums mobile app
True servant of God.......The choosen one....Mlee kidini mhamasishe ili akue akimpendeza Mungu aje kuwa mtumishi wa Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom