Hii imetokea wiki iliyopita jumatano..
Nilienda kumtembelea rafiki angu fulani tumeanza nae lakwanza ila alipofika form four alifukuzwa shule, sababu kuu alipiga ofisi nzima ya walimu akiwa mwenyewe. Walimu walikua wanatumia kumpiga na viti ila hakutoka hata nundu ila walimu wote wa kiume aliwachakaza vibaya..
Je aliwezaje kuwapiga mwenyewe.?
Huyu rafiki angu alichanjwa dawa fulani inaitwa Vidono ambavyo vinamuongezea nguvu pia ukimpiga kwa siraha yoyote ile haumii wala kuvimba. Siraha inayoweza kumuumiza mtu mwenye vidono ni wembe tu kwakua wenyewe ndio ulio mchanja dawa.
Sasa siku hiyo jumatano tukawa tunakumbushia tukio hilo la kupiga walimu nikamwambia wale walimu wangejua wangechukua nyembe wangekuweza..Akasema kwake hata wembe haufanyi kazi maana kidono alichokula ni extra ordinary wembe haushiki. Nikabisha.
Alinieleza kua yeye ukimchana na wembe unaweza kumchana ila damu hazitoki kama mimi na wewe zinavyotoka..ukimchana zinaganda hapo hapo. Nikabisa.
Alienda chumbani akachukua wembe akajichana kwenye msuli wa mkono damu zilitoka kweli lakini hazikutiririka kwa maajabu kabisa baada ya dk tano kile kidonda kilikua kimeshapona kabisa kama hakuna kitu kilichotokea.. Nilishangaa sana hili tukio.
Nafahamu aina nyingi za vidono na nishawahi kuwa navyo siku za nyuma ila cha huyu jamaa ni kiboko akanieleza jinsi alivyochanjwa weeee na madawa yakiyotumika nikabaki nimeduwaa..
Hua twaona tu kwenye muvi za X men wolverine anachanwa kisu hapo hapo anapona ila hiyo siku nilithibitisha kua things are real in this world.
Niliharibu vidono makusudi kabisa maana mm sio mgomvi wala sijichanganyi kwenye makundi ya watu ila hua nikifikiria wale wahuni wa Kigigo,gongolamboto,Karakata,Sombetini,Ngarenaro, mianzini,Matejo,Sinoni,ungalimited No way itabidi nivitafute asee