Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Mhh, Mkuu mbona povu. Mi sijaona ubaya hapo. Maana wameconnect hayo makanisa na nguvu za giza walizofanyiwa. sasa tatizo lipo wapi. si wanatoa na solution. Au ulitaka salution iwe kwamba walienda kwa waganga wa kienyeji. ukiona unachukia sana mambo ya MUNGU au unakereka sana ukisikia habari za MUNGU basi ujue kuna tatizo mahali
Shangaa na wewe ndugu yangu, huko juu kuna watu wamesimulia walipopatwa na maswahibu walienda kwa waganga wakapona na sijaona watu wakitoa povu.... sasa kuna ubaya gani mtu akisema aliponea kanisani maana povu linalotolewa sio la hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi tz ingetoa mabingwa wa ndondi duniani,UFC nk kama kweli hiyo dawa inafanya kazi.
Hii imetokea wiki iliyopita jumatano..
Nilienda kumtembelea rafiki angu fulani tumeanza nae lakwanza ila alipofika form four alifukuzwa shule, sababu kuu alipiga ofisi nzima ya walimu akiwa mwenyewe. Walimu walikua wanatumia kumpiga na viti ila hakutoka hata nundu ila walimu wote wa kiume aliwachakaza vibaya..

Je aliwezaje kuwapiga mwenyewe.?
Huyu rafiki angu alichanjwa dawa fulani inaitwa Vidono ambavyo vinamuongezea nguvu pia ukimpiga kwa siraha yoyote ile haumii wala kuvimba. Siraha inayoweza kumuumiza mtu mwenye vidono ni wembe tu kwakua wenyewe ndio ulio mchanja dawa.

Sasa siku hiyo jumatano tukawa tunakumbushia tukio hilo la kupiga walimu nikamwambia wale walimu wangejua wangechukua nyembe wangekuweza..Akasema kwake hata wembe haufanyi kazi maana kidono alichokula ni extra ordinary wembe haushiki. Nikabisha.

Alinieleza kua yeye ukimchana na wembe unaweza kumchana ila damu hazitoki kama mimi na wewe zinavyotoka..ukimchana zinaganda hapo hapo. Nikabisa.
Alienda chumbani akachukua wembe akajichana kwenye msuli wa mkono damu zilitoka kweli lakini hazikutiririka kwa maajabu kabisa baada ya dk tano kile kidonda kilikua kimeshapona kabisa kama hakuna kitu kilichotokea.. Nilishangaa sana hili tukio.

Nafahamu aina nyingi za vidono na nishawahi kuwa navyo siku za nyuma ila cha huyu jamaa ni kiboko akanieleza jinsi alivyochanjwa weeee na madawa yakiyotumika nikabaki nimeduwaa..
Hua twaona tu kwenye muvi za X men wolverine anachanwa kisu hapo hapo anapona ila hiyo siku nilithibitisha kua things are real in this world.

Niliharibu vidono makusudi kabisa maana mm sio mgomvi wala sijichanganyi kwenye makundi ya watu ila hua nikifikiria wale wahuni wa Kigigo,gongolamboto,Karakata,Sombetini,Ngarenaro, mianzini,Matejo,Sinoni,ungalimited No way itabidi nivitafute asee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakuwa mchawi huyo maana kutajwa kwa makanisa kunamuumiza Sana nafsi yake.
Wote wanaotokwa na povu wapuuzieni tu,
mahondaw, Tanayzer endeleeni kutiririka tuendelee kujifunza..
Shangaa na wewe ndugu yangu, huko juu kuna watu wamesimulia walipopatwa na maswahibu walienda kwa waganga wakapona na sijaona watu wakitoa povu.... sasa kuna ubaya gani mtu akisema aliponea kanisani maana povu linalotolewa sio la hapa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kipindi nilikua natumia Misukule mno,kulimia ila roho inanisuta mpaka nimewakimbia washkaji
ambao walikua wananiuzia

Machache usiyoyajua Gamboshi zipo mbili Kuna moja ipo Mwanza na nyingne Zanzibar eneo la Bumbwini.hata hivyo nimezoea kwenda hasa Gamboshi ya Mwanza kununua vifaa,misukule pamoja na Dawa mbalimbali kibiashara.

All in All sipo huko tena na sirudi tena



Sent using Jamii Forums mobile app
Muhhh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli uchawi Upo tena uhakika

Mimi Nina visa 3 mwenyewe kwenye maisha yangu.

Cha kwanza kilinitokea nikiwa na miaka 6 mwaka 92 na cha pili kilinitokea mwaka 2008 nikiwa mkubwa na elimu yangu kwa hakika uchawi Upo tena sana

Mwisho nilipanga nyumba mtaa wa mecco Mwanza nyumba nzuri ipo katikati ya nyumba nyingi sana nikalipa zangu kodi 1.5m kipindi hiko nimehamia mwanza kikazi Niko zangu single

Usiku nilichapwa viboko sijawahi Ona ananichapa simuoni kesho yake nikasema labda ndoto,saa 2 tu usiku bakora za kutosha,nikaamua kwenda kulala guest asee

Baada ya siku nikahama

Hii nyumba mpaka leo ipo pale mecco kwa ambao hamuamini uchawi nenda kashuhudie mwaka wa 6 haina mpangaji wala binadamu anaishi pale

Waganga na waombaji hawajafua dafu

Inasemekana walimuua mwenye nayo wakaidhurumu malipo ndio hayo.

= wakaidhulumu
 
Back
Top Bottom