Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Maisha haya daah

Sent using Jamii Forums mobile app
wachawi noma,unaweza kuta wewe ni mrembo sana,ukaliwa kimasihara kichawi na mwanaume mbaya kuliko wanaume wote,tena mzee halafu kikongwe asiekua na familia na wala hakuwahi kuwa nayo kabisa maishani,bila wewe kupenda.
ndio maana kwetu sisi wanawauaga wachawi ujue.
 
Sihusudu Ushirikina ujue.. Ila madame wahuni wakikuotea na Kukutoboa ndio utakumbuka.
Sifuatilii yoyote yanayohusu vitu hvi ila Nina mkosi wa kusingiziwa mambo mimi acha tu..
Ngoja nijifikirie..ikinipendeza nitaweka.
Pole sana kwa hayo mambo ya kusingiziwa.Mimi huwa nafuatilia mada zako vizuri sana humu ndani,ni nzuri,na unaonekana ni mtu mwenye akili na muungwana sana.Nakuomba uanzishe thread inayohusu hayo matatizo yako ya kusingiziwa vitu,watu watapata elimu, na utapata mawazo mazuri ya kusolve hiyo mambo.
Mwisho kuna mdau kaomba umwandikie mpango wa kuanzisha mradi,kajuaje kama wewe ni mtaalamu wa mambo hayo? kuna mawili, moja,unaweza kuwa unavutwa na mtu wa mfumo kwa nia mbaya ama njema,mbili au kweli kaona uwezo wako .
Fungua macho yako.kuna namna nyingi za kumnasa mtu.Niliwahi kukutana na mtego kama huo ,niligundua kua ni mtengo.
 
Hizi story nazifananisha na zile za zimwi, vibwengo, shetani ana mguu mmoja wenye kwato, mumiani (nyonya damu), chunusi, ukimuona albino tema mate mara 7 kwenye kifua chako, mtu amechukuliwa msekule n.k.... all of these are storytelling and myth.

Alafu ukichunguza story hizo ni za maskini tu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini sasa upo hapa ??


You have mysterious mind max.
Hizi story nazifananisha na zile za zimwi, vibwengo, shetani ana mguu mmoja wenye kwato, mumiani (nyonya damu), chunusi, ukimuona albino tema mate mara 7 kwenye kifua chako, mtu amechukuliwa msekule n.k.... all of these are storytelling and myth.

Alafu ukichunguza story hizo ni za maskini tu....

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna namna ya ku deactivate kidono halafu baadae ukakirudisha tena?
Nafahamu side effects zake.
Maana kama huyu rafiki yeye ukimchoma kisu hakiingii ila panatoka kanundu kadogo tu ila baadae kanapotea.
Halafu dawa aliyopewa imechanganywa na Mifupa ya mbwa mwitu so ukifika mwezi mpevu anapata shida sana. Si ushaona muvi za Teen wolf au Twilight saga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha! Hakuna namna ya ku recharge kwani MM?
Maana haya mambo haya si mchezo unashangaa tu unampenda mtu hata hujui mmeanzaje kumbe ni power bank zinafanya kazi
Mi naskiaga tu almaarufu kwa jina la ndere ila naskiaga ikiisha makali unakataliwa hadi na kuku utakuwa na gundu balaa baada ya kuenjoy kwa mda hiyo ndo inaitwa price hapo ndo unalipia [emoji3]

All magic comes with a price..

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee!
Hii kitu inakupa kumbe ina nguvu sana?
Kuna mdau mmoja hapa kitaa yeye alikuwa anadai ana kizizi, masafa yake ni kwenda chuo pale SAUT anajibebea madem.
Mdau pesa zake za kubangaiza tu na elimu ya kulenga kwa manati
Anaweza kua na kitu mfukoni ,akachanjiwa au akaweka mdomoni.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mysterious ni suala la kuhusiana na maajabu, lisilojulikana vizuri.

We unatafuta Gambosh Google wakati huko ni kijiji cha jirani kwao Nyani Ngabu na yeye ana habari zote za huko.

Na anasema hakuna uchawi kama inavyodaiwa na watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini Gambosh iwe mysterious place wakati ni eneo lipo kama maeneo mengine?

Mambo yake yapi?

Kwanini uyaweke siri?

Nyani Nyabu ana habari gani hizo ambazo mnazijua? Bila shaka na wewe unaabudu mysterious things za Gamboshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2016 nimeenda kufanya kazi mkoa flani, ikafika usiku tukatafuta guest. Tukapata room moja tu ila ina vitanda viwili na sisi tulikuwa wawili wote wanawake kwhy tukaamua kuchukua hiyo room.
Bhana weee usiku wa manane acha tuanze kuvutiwa shuka yaan tukawa tunanyang'anyana. Mwenzangu akashindwa kuvumilia akapiga mayowe, kwenda kuwasha taa, shuka zimerushwa mbali na vitanda.

Tukaendelea kulala ila taa tukawa hatujazima, mara mlango ukawa unalia km unafungwa na kufunguliwa, hiyo siku kwakweli sitaisahau. Palivyokucha tulijitahidi kumaliza kazi haraka na kurudi makwetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku nyingine huko mkoa wa Mara, nimelala na wanangu mara usiku wa manane nastuka nakuta taa zote zinawaka na mziki mnene sebuleni.
Bahati nzuri mdada wangu alikuwaga sio muoga, akajitosa kwenda kuzima taa na redio. Tukarudi kulala.
Muda kidogo tukamwagiwa mchele kitandani hatujakaa sawa tukaanza kusikia mlio wa high heel zinatembea ndani.

Kulivyokucha asb na mapema nilienda kuita mchungaji akapiga maombi hapo nyumbani na ndio ikawa mwisho wa hizo seleka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi

Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri

Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma

Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma

Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea

Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge

si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.

wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.

Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele

Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
🤣🤣
 
Back
Top Bottom