ngulukizi
JF-Expert Member
- Oct 10, 2018
- 619
- 1,749
Biashala ina mambo mengi ndugu uchawi ktk biashala upo nakupa kisa kimoja hivi miaka ya nyuma nilifanya biashala ya duka maeneo ya kwa mkandawile huko nikawa nikiweka mtaji biashala nauza vizuri ila hela jioni siioni nikajiongeza mana pale kulikuwa na waha wanauza hao mpk basi basi nikaenda sehemu kwa mzee mmoja kule Kunduchi yy ni marehemu kwa sasa akaniangalia nyota akasema inabidi kazi yako tuifanye siku ya j5 kulingana na ulivyo ila apatikane kuku mweupe ambaye tutatoa damu yake kweli nikaacha hela ya kuku pale nikaondoka siku nimefika akafanya mambo yake na akanichanja chale kadhaa mwilini yule mzee ni mha akaniambia nakupa hii azima kaiweke dukani kwako huyo ni jini atakuwa anakujazia bidhaa pale dukani na ndio wafanyabiashala wakubwa wanamtumia akanipa na masharti kadhaa basi nakumbuka nilikimbiza pale ila nilikuja kukosea sharti moja kila kitu kikafa ila tangu hapo hakuna ninachofanya kikaenda sawa tena mpk sasaKutoboa biashara.
1. Kuwa mbunifu kuja na idea ya biashara unayoipenda na yenye uhitaji, acha ujinga wa kufuata mkumbo kufanya biashara fulani kisa umesikia inalipa.
2. Usiwe na akili mgando kusubiri wateja waje uwauzie tu kisa wewe mwamba una mtaji na bidhaa zipo dukani, jifunze sales and marketing.
3. Usiwe na akili mgando kupata faida bila kufanya saving yoyote. Jifunze elimu ya fedha na siyo ujuzi wa kuuza tu bidhaa na kurudisha chenchi.
4. Usiwe na akili mgando kufanya biashara moja na kutegemeana kwa asilimia mia moja kiasi kwamba huna back-up yoyote in case biashara hiyo ikiyumba, hapa ndo dhana ya ndumba inapoanzia na kuwa na akili kama za mtoa mada.
5. Acha kuwa na akili mgando kufuata kila ushauri wa kibiashara au kimaisha unaotolewa Jf, wengine humu wana matatizo kuanzia ukoo wa babu zao hivyo matatizo hayo yanaama ukoo hadi ukoo.
Wenye akili za mkumbo wote huwa fursa kwa wanaojielewa. Chunguza utagundua.
Sent using Jamii Forums mobile app