Nilirudi na kuungana na familia huku tumeshaanza kutawaliwa na hali ya hofu lakini haikuwa hofu kubwa sana sababu naweza kukiri kwenda kwa mganga ile ndo ilikuwa mara yetu ya kwanza toka nizaliwe hivyo tulikwenda lakini hatukua tunaamini sana kwenye uwepo wa uchawi japo kwa sasa kidogo tulikuwa tumeanza kuingiwa na imani kuwa mambo tuliyoyasikia kwa yaliyowapata wenzetu wakiotufanyia ule ushenzi sasa na sisi tutayapata soon kivitendo.
Tulikaa macho mpaka usiku wa saa 5 tukiwa tunasoma sana dua mpka tunalia kabisa, then kila mmoja akaingia kwake kulala,naweza kusema kuwa lile dude ni kama lilikuwa linatusikiliza tumalize kuomba dua then tukiingia ndani lianze kazi yake, ile tumejifunika tu shuka tukasikia kishindo kikubwa mno juu ya bati.
Hakuna aliyeongea zaidi ya kila mtu kujifunika shuka yake zaidi palikuwa kimya,basi kishindo kilidumu zaidi ya masaa matatu mazima then ikafata sauti ya ngombe kupika kelele ndani ya dakika tano tu tukasikia kimya.mpka asubuhi ilivyofika asubuhi tukatoka nje,tukakuta uwani kote kumejaa nyama tupu za ngombe hakukuwa na ngombe hata mmoja mzima kati ya wale waliobakia,nyumba yetu ilikuwa ina fens hvyo ile kufungua tu geti,tukakuta majirani kibao wako getini wanauliza kulikoni.
Hapa nikiri mzee alijaribu kuficha akasema tu kuwa mtaani kuna mtu anamfanyia husuda na anamfanyia ushenzi ote huo mzee alilalamika sana,kisha majirani wakatusaidia kusafisha pale uani zile damu pamoja na zika zile nyama wakati huo pia polisi walikuja wakachukua vielelezo,na tukaenda polisi pia kutoa taarifa,wakasema watafatilia huyo mshenzi aliofanya huo ushenzi na ndani ya saa 48 watakuwa walishampata.
Mzee alirejea jioni kutoka polisi akalakiwa na majirani na pole kutoka kila sehemu,ulivyofika usiku hatukuwa hata na hamu ya kula ulinunuliwa tu mkate na chai lakini hata nusu haikufika,naweza kusema mungu tulimsahau maana hakuna aliyeomba dua tena ote tulilala barazani,
mzee alivyotoka polisi mda ule mkuu wa kituo alioanga team yake bila kumwambia mzee kuwa watafanya kitu gani,basi aliteua askari wake watano ilivyofika usiku wa saa tano wakaja mpka nyumbani na gari yao wakawa umbali kama wa mita 10 au 20 wanaiangalia nyumba yetu kwa mbali huku wengine wanaizunguka kwa mbali,sasa wakiwa wanaizunguka wakamuona mtu mweusi tiii,anakimbia juu ya bati kuanzia mwanzo wa bati mpka mwisho wa bati akiwa juu,
walivyomuona wale wa kwenye gari wakachukua silaha zao then kwa pamoja wakazunguka nyumba kumuwinda,baada ya muda wakawa wanaskia kuku kama vile wanachinjwa wao target yao kubwa ilikuwa wanasubiria atoke tu nje ya geti wamkamate mchezo uishie hapo,na kweli baada ya mda aliruka ukuta,ile anatua tu chini wakamuweka chini ya ulinzi lakini mdomoni alikuwa na damu nyingi sana ya kuku aliofyonza damu,lakini hakusimama akawa anakimbia wakapiga risasi moja juu lakini hakusimama kuna askari mwengine alisogea na yeye akampiga ya mgongo,baada ya kupigwa ya mgongo aligeuka na kuwarudia kwa uoga wakawa wanapiga risasi nyingine nyingi lakini linawafata tu,askari mmoja alipigwa kofi kali sana mpka akazimia,yule wa pili aliyekuwa anakuja akampiga risasi mgongoni akawa anakimbilia gari kule walipo wenzake,walivyomuona anakuja wakawasha gari na lenyewe likarukia ile gari na kuanza kuwachapa makofi walipiga sana risasi kulipiga na nyingine kwenda hovyo kwa hasira lilitoboa toboa mpka mataili ya magari kisha likapotelea kwenye shamba lililokuwa mbele yetu,
Wakati yote yanatokea sisi tulikuwa tuko barazani,tulivyosikia kelele za juu ya bati tulijua ni lile dubwana na hata tulivyokuwa tunasikia kelele za kuku tukawa tunaelewa nini kinaendelea lakini tuliingiwa na butwaa zaidi baada ya kusikia risasi maana ilikuwa ni kitu kigeni na kwa wakati huo ilikuwa ukisikia basi unajua ni majambazi ambao walikjwaga wengi ni majambazi kutoka burundi,
Ghafla tukawa tunasikia tunagongewa hodi na majirani ambao kwa sauti tuliwajua,ile tumetoka nje tukakuta geti limetobolewa tobolewa na risasi mbele tunaiona difenda ya polisi imegonga mti wa umeme,lakini tyre zikiwa zimechanwa chanwa,ndani walikuwepo polisi wawili hawana fahamu lakini wanatoka damu,na mbele kuna mwengine amelala chini lakini mguu umeparuliwa tukamsikia mwengine nyuma ya ukuta ndo anazinduka lakini kama amechanganyikiwa.
mzee alitoka haraka akawasha gari akawapakia tukaingia mimi broo na wale askari gari ikawashwa wakati huo tunawakimbiza hospitali kuna askari mmoja hakuonekana kati ya wale watano,hivyo wale majeruhi wakaomba wananchi wamtafute mwenzao na pia wakatoe taarifa kituoni kule ujiji sisi hao tukawasha gari tukaondoka
Tumetembea na gari mpka sehemu moja inaitwa buzeba zeba kwa mbele kuna sehemu moja inaitwa bimala kuna bohari kubwa ya dawa ya msd sijui kama ipo mpka leo kwa mbele kuna mwembe mkubwa kwa mbele tukamuona nyoka mrefu sana anavuka bara bara ikabidi mzee asimamishe gari apite cha ajabu yule nyoka alivyotuona alisimama kichwa kikiwa kwenye kichaka,yule askari ambaye ndo alikuwa mzima aliyekuwa amezimia akawa anabishana na mzee,mzee anataka kumsubiri mpka apite yeye anataka mzee amkanyage
mwisho wa ubishi mzee akamwachia sterlimg aendeshe yeye basi akawasha tena gari akairudisha nyuma then akatoka spidi kali mno akamkanyaga yule nyoka,tuliona nyuma baada ya kumkanyaga kama aliruka juu kisha kwa mbali tukaona kama kwenye lami kwa pembeni kwenye majani kama kuna kitu kinatukimbiza kwa kasi mno lakini kwa spidi tuliyokuwa nayo hatukujali sana ila tuliskia tu gari kama imegonga kama tuseme jiwe then ikawa sawa,
baada kama ya dakika tano tukawa tumefika hospitali ya maweni wagonjwa wakashushwa,wakaenda kutibiwa,baada ya mda mkuu wa kituo akawa alishafika pale na baadhi ya askari sasa yule askari ambae alikuwa anaendesha gari yetu akaomba funguo ili achukue radio call yake mzee akampa funguo,alivyofika ile anafungua tu mlango tukasikia ukelel mkali mno mamaaa nyokaaaa,kufika pale tunakuta ndo nyoka analallizia mkia porini, tukamfunga kitambaa lile eneo tukamuwahisha haraka hospitali.
kuona hivyo mkuu wa kituo akapaniki akawa anamfata mzee amwelezee kulikoni wakati huo mzee alikuwa kama amedata fulani,basi gari zikawashwa mpka nyumbani tulivyofika pale tulikuta askari wengine ambao walifika mda mrefu,mkuu wa kituo alivyofika pale akawa anaendelea kuulizia askari wake mmoja kama alishapatikana ninachokumbuka alipatikana na wala hakuwa mbali na pale bali alikuwa ameingia kwenye shimo la taka akiwa amejifunika na gunia la mkaa juu akiwa na silaha yake mkononi,na aliyegundua yumo mle ni mzee jirani yetu ndo alienda kumwaga maji ya kahawa sasa kwenye kumwaga akaona kiatu kukivuta hivi akashangaa kuna mtu ndo akampliz na kumtoa presha akaja nae mpka pale nyumbani ambapi mtaa mzima ulihamia hapo.
Baada ya kupatikana ndo akaingizwa ndani na baadhi ya wazee pamoja na askari wengine akaelezea mwanzo mpka mwisho walichokutana nacho,hapo mzee nae akaelezea mwanzo mwsho wakafikia muafaka baba na sisi ote pamoja na baadhi ya wazee twende kwa mzee juma njemba japo alikuwa hayupo lakini walikuwa wanataka kuongea na mkewe
Tukafika tukamkuta yule mama anatwanga unga wa muhogo kwenye kinu,hapa nikiri wazi yule mama na familia yake walikuwa wanaishi maisha duni mno lakini walikuwa wanaheshimiwa mno nasema mno nimiwa namaanisha hata askari walivyoingia mle ndani walikuwa wanamsalimia yani mpka ile adabu unaona hii sasa huyu anaweza kupiga hata magoti,tulikaribishwa vizuri.
mama yule aliwaeleza kosa tulilolifanya na mtihani wa mzee kwenda DRC,kumtibu kuna mteja wake,lakini kuna kauli ambayo aliitoa kuwa kama dubwana hilo halijarudishwa/kudhibitiwa basi litatuua sisi sote na likitumaliza sisi litahama kwa yoyote maana chakula chake ni damu
basi baada ya kile kikao ikaamuliwa kuwa siku hiyo hiyo familia nzima twende huko huko congo nakumbuka kulikuwa kunaitwa kalemi wenyeji mtanisahihisha na kwenda ilikuwa ni kwa njia ya boti na mwenyeji ambae ilibidi atupeleke alikuwa ni mjukuu wa mganga maana ndo alikuwa anakujua kipindi hicho nakumbuka simu zilimuwa siyo sana na barua pia zilikuwa zinatumika,na safari tuliianza ote nakumbuka tulipewa askari wawili wenye silaha na hatukuwa na pasport wala chochote zaidi tu ya barua kutoka polisi
naomba niweke nukta hapa then ntamalizia baadae hasa kwenye kunusurika kutekwa na majambazi ya burundi na kuponene a chupu chupu kuliwa nyama na jinsi tulivyolimaliza lile dubwana
Sent using
Jamii Forums mobile app