Muwe macho kuna duka fulani liko maeneo ya mnazi mmoja hilo duka ni jembamba ila ni refu kwa ndani kama mita 35 hivi urefu, ukiingia upande wa kushoto kuna mashelfu halafu njia, katikati kuna meza ndefu mwanzo mwisho, upande mwingine wa meza hakuna kuingia ni eneo la kupita na kukaa wenye duka. Kwa mbele mwisho ni kama kuna vyumba. Piga picha ya korido moja pana kiasi refu. Nimeeingia natafuta spana ndogo namba 10. Nilipoingia ndani nikakaribishwa na kijana wa kazi mbantu mwenzangu katikati alikaa mtu wa miaka 40s hivi amekalia hiyo meza ndefu kumwelekea mkewe ambae alikaa kwenye kiti na ana vitabu vya duka risiti n.k. Wao ni asili ya waarabu ila sio wale weupe sana. Binti alikuwa na sura nzuri ya mviringo uso mpole, alivaa nguo ya rangi ya njano njano mix light brown imefunika mpaka nywele,ila uso unaonekana wote.
Nilipoingia yule mfanyakazi akatafuta spana pale mwanzoni mwa duka zile shelfu za kushoto ikaonekana ameikosa, akasogea mbele kuingia ndani zaidi na mimi nikamfuata akaanza kupekua box jingine anatafuta hiyo spana ndogo akaikosa tena, akazidi kuzama mbele ndani ya duka mimi nikamwacha aende akipata hiyo spana aniletee, yule mfanyakazi alipoona simfuati akasema njoo nikasogea kumfuata
Ina maana sasa mlango mdogo wa kuingilia umefunga hii milango ya kioo. Ndani tuko wanne. Wakati ana pekua au anazuga kupekua box nyingine kutafuta spana ghafla nikaona kama niko sehemu ya hatari kwani upepo sijui ulitoka wapi sababu duka halina madirisha ila mwanga wa kutosha upo. Yaani paa liko juu sana hata sehemu nyingine kutoa bidhaa inabidi ngazi.
Ule upepo ukanizunguka kama kimbunga kinavyozunguka ila wenyewe ulinizunguka mimi tu wala hakuna karatasi iliyotimuliwa. Sekunde mbili tatu nne nikasahau hata kama nafanya nini mle hata yule kijana nikamsahau, ile kitu iliyokuja na upepo ilikuja na roho au hali fulani hivi, hii hali mara nyingi watu wana ihisi wakipita makaburini hasa usiku, mimi ni mlokole.
Palepale nikajua niko kwenye mapambano na majini, nikajikaza kuikataa "panic" na hofu ambayo ilinianza kwa kasi, nikatulia ndani ya nafsi, nikaikemea kwa Jina la Yesu ile roho au hicho kitu kimoyo moyo kitokomee mbali
Ile hali ikaondoka ghafla kama ilivyokuja.
Ila nilipata mtikisiko na mapigo ya moyo yalizidi.
Pale pale nikasema Asante Yesu kimoyo moyo.
Ilipoondoka tu ile hali yule mfanyakazi nikasikia ana niita akanipa ile spana na 10 chrome. Inaelekea alijua kilichotokea, na mimi sikumwambia kitu na kwa nje nilikuwa niko fresh kabisa nimetulia, sikuonesha kama nimepats mtafaruku fulani.
Ikabidi niende kulipa kwa yule dada aliyekaa pale mezani.
Nilitembea taratibu kwa kujiamini baada ya kuona kumbe Yesu amenitetea na hawa wafuga majini hawana lolote na hawawezi kunifanya kitu, hawana
hiyo power na power yangu katika Yesu imewashinda na nimeshinda vita kubwa.
Nilichoshangaa alianza kuniangalia toka napewa spana mpaka nafika kwake kwa mshangao na alikuwa hapepesi macho kabisa. Akanipa risiti akaendelea kunikazia macho natoka nageuka nyuma kumtazama nakuta yuko na mimi tu mpaka nikahisi huenda huyu binti sio binadamu wa kawaida sio rahisi kumkazia mtu macho muda wote ule bila kope kucheza, nikampotezea.
Mme wake alikuwa anamtazama mke wake kwa tabasamu fulani hivi hana habari na mimi.
Toka nimeingia na kutoka niliongea na mfanyakazi tu.
Picha niliyiopata pale ni kwamba lile duka watu wanatolewa kafara, na yule mfanyakazi anashirikiana na wale watu mwanzo mwisho. Ni neema tu ya Mungu iliniponya, ingawa huwa siondoki nyumbani bila kuomba full ulinzi wa Majeshi ya Mungu.
Na walengwa naona ni mtu anayeingia peke yake, sababu akipotea humo hakuna atakaejua. Nimeacha vielelezo vingi ambavyo nikitaja hapa kila mtu aliyepita uhuru rd ataliju hilo duka.
Sijapita tena pale ila namshukuru Mungu kwa kunipa kuniokoa. Bila Yesu pale ningeliwa nyama najiona huyu anakata paja huyu kidole, damu yangu wangekunywa juice.
Nataka niende tena pale pale kucheki kama yule jamaa pale mlangoni atanikumbuka, nitaulizia spana tena. Ila safari hii nitajipanga wakileta majini yao tena, kunidaka maana majini hayakati tamaa. nitawasambaratisha wao na majini yao,itakuwa mwisho wa biashara za majini. Itakuwa bonge la showdown.
Thank you Jesus
Matukio:2023
Ushuhuda namba. 2
Kule shambani ninakolima ni kijiji hakuna umeme na network taabu sana. Sasa nilikuwa nafuatilia kwa bidii simbank ya TCB nivute hela nilete halotel nikaitoe. Mchana kutwa napata msg server down.
Nikaamua kuamka saa nane usiku, nilifikiri muda huo server itakuwa haina jam kama mchana, nikatoka nje mita kama 60 hivi nje ya kambi yangu. Kule nyumba ziko mbalimbali sana, giza nene. Nikawasha simu janja yangu nifanye muamala ghafla mtu ambae haonekani akanigusa begani kushoto kama ananistua kitu.
Kugeuka nyuma hakuna mtu. Nikadharau nikaendelea na muamala. Hii ni Mwezi march, mwaka 2024