Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 11,640
- 24,066
Sawaaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha uchawi mkuuSawaaa
Ni Mapenzi Yake MUNGU mpaka leo hii upo, kuna nguvu ya MUNGU ilikukinga dhidi ya nguvu za giza ulipopita hapo... Oyaa hawa masela huwa hawakopeshi ukiwaona live au wakigundua umewaona au kuona mambo yao na ww sio mhusika.. au probably na ww una kinga za kijadi za huko kwenu ulisha chanjwa mkuu [emoji2][emoji2]Siku flani za Mwezi Nov mwaka wa 2023 ilikuwa siku ya kushangaza kwelikweli. Kwa umri wangu wa 27 kipindi hicho sikuwahi Kuona miujiza yoyote yenye chembechembe za uchawi na ushirikina. Sikuwa home Kwa miaka kadhaa hivyo siku hizi nilikuwa nimewatokea kuwacheki hali zao.
Njia ya kuelekea home huwa Kuna miti mikubwa minne iitwayo MIKUYU. Hii miti bwana husemwa na wanakijiji kama miti yenye kuwa makazi ya majini. Na stori hizi nikizisikia toka utotoni.
Sasa basi siku hiyo naelekea home mida ya saa 1:30 hivi usiku nilipofika karibu na miti ile ghafla kulitokea upepo jirani na nilipokuwa nilipocheki ghafla nikaona kiumbe flani nguo nyeusi mfano wa mtu kinakimbia Kwa Kasi kubwa bila kugusa chini Kwa umbali wa karibu MITA 70 hivi then kikapotea. Ghafla nikahisi kichwa kinavimba na nywele zinacheza.
Nikakimbia kuelekea home Kwa mbio ndefu. Nilipofika home nikamwambia Maza. Maza alishtuka sana akisema eneo Lile limepoteza watu wawili mpaka Leo Kwa kifo kwani yasemekana walikumbana na majini. Dah hofu nami ikanshika nisije kuwa watatu.
Bahati nzuri mpaka Leo Nipo.
Labda kama nilichanjwa bila kuambiwa.Ni Mapenzi Yake MUNGU mpaka leo hii upo, kuna nguvu ya MUNGU ilikukinga dhidi ya nguvu za giza ulipopita hapo... Oyaa hawa masela huwa hawakopeshi ukiwaona live au wakigundua umewaona au kuona mambo yao na ww sio mhusika.. au probably na ww una kinga za kijadi za huko kwenu ulisha chanjwa mkuu [emoji2][emoji2]
maidha magumu mqjini yamejichimbia chimbo hayaji dunianiwatu waliishiwa visa
Unahisi malori ndio shida ama mlikua haunted na jini mahaba2010 nipo ndani ya fuso, natokea Ifakara kwenda dsm. Kufika Maseyu mida kama saa 8 usiku dereva akapaki, akasema amechoka anapumzika kidogo. Akatuambia saa 10 tumwamshe tuanze safari.
Sijui kama ni uchawi au ni nini, tulipitiwa na usingizi mzito, na wote, tulikuwa watatu tuliota ndoto ya aina moja. TUNAPIGA MECHI. tumejipiga mabao wote, kuangali saa ni dk 20 tu zimepita. Nilichowaeleza wenzangu ndio walichoota. Mwanamke niloyeota namgonga ndio huyo huyo wenzangu walikuwa wakiota wanamgona.
Niliota vipele vya baridi kwa uoga. Tukaondoka kuendelea na safari. Tangu siku hiyo sipandi tena malori ya mzigo yanayosafiri usiku.
Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Unatofautisha vipi usichokijua na nguvu za giza..., nadhani hii inapelekea uvivu wa fikra na kurahisisha mambo; Mababu zetu wangekuwa hivyo huenda mpaka leo tungekuwa tunakula chakula kibichi kwa kuogopa moto kwamba ni Uchawi au Mungu...Ujue watu wengi husema hakuna ushirikina,but utasena hivyo ikiwa hsujawahi kushuhudia .ila in short nguvu za Giza zipo sana tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Poleni sana mkuu ndiyo hivyo hii Dunia ina watu wabaya sanaMi nilimpata ajali kijijini na GARI ya mzigo kuitoa ikashindikana tukalala baada ya kunywa sana mpaka SAA Saba usiku kukawasha gari kucharge betri Isiishe Kama dka 10...tukazima tukalama...usiku nastuka taa zimewaswa full light nkazima fasta nikasema charge ishanyonywa yote...uzuri ilikuwa jino moja tu kupiga ikakubali tukaachrhe palee Ila mpango kuanzia siku hio ukawa haufungi Tena emajini tulifunga kwa ndani mbugani hapo Isaka Jana shy...ogopa NI hatari
malizia stori mbili za mwisho mkuuWakuu, mimi huwa nawashangaa sana watu wanaokana uwepo wa nguvu za giza (uchawi na ushirikina). Nadhani ni kwavile hawajawahi kukumbana na ushirikina. Na Mshana Jr huwa anapata wakati mgumu sana kuwaelewesha watu kuhusu mambo hayo.
Si ajabu hata comments tuzopandisha kwenye uzi huu wengine watafikiri ni story za kunogeshea baraza, la hasha! Mimi nina visa kadhaa nilivyoshuhudia:
1.Wakati nikiishi mkoani Mwanza, alikokuwa anafanyia kazi Mzee wangu, na nikiwa na miaka 11 tu, kuna siku wazazi wangu wakiwa wamelala huku wamefunga milango na madirisha yote, walikuja kugutuka kutoka usingizini mishale ya saa 9 usiku na kukuta madirisha yote ya chumbani kwao na mlango yamefunguliwa. Na kwavile kulikuwa na mbalamwezi, waliweza kuwaona bundi 4 wamesimama katika madirisha 2 ya chumbani huku wakiwatazama wazazi wangu waliolala kitandani. Baba alivaa ujasiri wa kuwatimua, ila baada ya kuamka watu 4 ndani ya familia tuliamka tukiwa tumechanjwa chale mwili mzima. Ilibidi familia iingie 'gereji' ndo mambo yakawa shwari.
2.Mwaka 1993 tukiwa tulipanga nyumba moja kule Tandika Mabatini, Dar es Salaam. Mwenye nyumba alitupa masharti kadhaa, kubwa kabisa likiwa ni katazo la kuingia nyumbani baada ya saa 6 usiku, au kwenda chooni/bafuni baada ya masaa hayo. Tulijitahidi kutii! Siku moja, mpangaji mwenzetu mmoja alikiuka masharti akaenda msalani saa 6 na ushee, tulisikia kelele za kuomba msaada, lakini hakuna aliyethubutu kwenda kutoa msaada. Kesho yake alfajiri tulimkuta jamaa bado ameanguka chooni. Mwenye nyumba alimfokea kwa 'kuyataka mwenyewe'. Ilibidi jamaa ahame nyumba baada ya siku 4. Ilikuja kubainika kuwa, Mwenye nyumba alikuwa anafuga majini na huwa anayafungulia masaa hayo yanaingia kazini, hivyo jamaa alikumbana nayo yakamshughulikia. Sisi nasi kwa uoga ilibidi tuhame kabla kodi yetu haijaisha.
3.Muda haunitoshi kusimulia nilivyokutana na wachawi ' live' mara mbili, wakati nikiishi huko Kanda ya Ziwa.
Ndugu yangu, shida watu hawaamini haya mambo kama yapo hata kama nitasimuliaje.malizia stori mbili za mwisho mkuu
Mimi naamini 100%...Ndugu yangu, shida watu hawaamini haya mambo kama yapo hata kama nitasimuliaje.
Ila wasioamini wote wajaribu kwenda kuishi vijijini huko, na majibu watakuja kutupa hapa. Mimi nimeishi Uswahilini Dar, na nikaishi Kijijini, Usukumani huko. Kote huko niliyaona hayo mambo.
Mwaka 2023 nilitoka nje nikamuona chura karibu ya ukuta. Nilikuwa na mwanangu wa miaka 2. nikaona anaweza aogope, nikainama kuchukua kizibo cha chupa nimrushie aondoke. Kitendo cha kuinama, kuokota kizibo ni sekunde kama 2, nainuka chura hayupo, hakuna sehemu ya kujificha chura na kuna smenti kote. juu ya alipokiwepo kuna dirisha limefungwa halina upenyo. Nilibaki nimeduwaa. Ametowekaje? Namuuliza mtoto chura yuko wapi? Chijuiii. Hadi leo sielewiMimi naamini 100%...
Nataka nijionee zaidi, usukumani maeneo ya vijiji vipi nikafanye nijionee zaidi?
Ningependa kujua ulimkosea nini hadi aseme amekusamehe? Baba alikuwa wapi kipindi hicho? Kwa nini unadhani uliwaona hao wachawi? Nguvu ya kukimbia na akakubeba unadhani aliitoa wapi? Kuna kitu ningependa kujua ambacho hujakisema na kukiweka wazi.ngoja tu nimalizie kisa changu kingine,but huwa nikimsikia mtu anasema uchawi hakuna namwangalia na kutikisa kichwa tu.
Nimezaliwa na mama ambae ni mgonjwa wa sicle cell hali iliyokuwa inamfanya mama yangu kuumwa mara kwa mara hasa mifupa na hata kuishiwa damu mara kwa mara naweza kusema mama yangu haikuwahi kupita week bila ya kuumwa au kulazwa hospitali,hali iliyopelekea kuwa anatumia mara kwa mara dawa za valium na hata wakati mwengine kuwa anajichoma mwenyewe sindano za valium ili apunguze maumivu apate usingizi,ilikuwa ni usiku wa saa 8 usiku nimelala na bimkubwa naskia anaugulia maumivu makali mno ya mifupa,nikaanza kutafuta dawa hakuna sindano wala vidonge na nyumba tulikuwa mimi na yeye tu wakati huo simu ni anasa na usafiri huu wa boda boda hakuna na gari ilikuwa saa 4 mwisho, basi kila akiugulia maumivu akili yangu inahangaika mwisho wa siku nikamchukua nikamuweka mgongoni kulikuwa kuna dispensari fulani hvi ipo kigoma ujiji na sisi wakati huo tunakaa bimala kwa wenyeji wa kigoma wanakujua ni umbali wa kama dakika 10 kwa gari,basi nikamuweka mama yangu mgongoni safari ikaanza wakati huo nina umri wa miaka 12 tu,tembea sana kila nikiskia anazidi kuugumia na mm ndo naongeza spidi,basi tukafika sehemu moja inaitwa shine cinema ni ukumbi fulani hivi walikuwa wanaonyesha movies na pembeni kuna shule ya msingi ujiji, baada ya kufika pale ile shule tuliona imegeuka treni watu wanashuka na kupanda wakati huo upande wa pili kwenye ule ukumbi kwa nje tukaona watu wengi mno wapo nje wanapiga kelele mno wanasherehekea wako uchi wa mnyama wanauza vichwa vya watu ulimi na viungo vingne vya binadamu na kulikuwa kunanuka damu kweli kweli cha ajabu ajabu kufika pale nikashikwa na bumbuwazi kiasi cha kanga kulegea bimkubwa akaanguka lakini kwa kusimama sasa alivyofungua macho kuona kilichopo mbele yetu nilishangaa tu amenibeba juu alitoka mbio za ajabu huku akiwa amenibeba mgongoni mpaka ujiji kwenye ile dispensary alivyofika tu akazimia pale pale nakumbuka alikuja kuzinduka siku ya tatu na mtu wa kwanza kuniita alivyoamka tu nilikuwa mimi alinikumbatia na kuanza kulia sana(kisha akanitamkia nimekusamehe leo na siku zote za maisha yako) kauli hii aliirudia akiwa anafariki ndani ya mikono yangu mwaka 2007 kwa kunambia(nakufa mwanangu nakupenda sana na nakufa nikiwa radhi nawe uishi maisha ya kumpendeza mungu na uwapenda nduguzo kama ulivyokuwa unanipenda mama yako)
R.I.P my beloved mom
Sent using Jamii Forums mobile app