Kama umewahi kutumia haya majani ya chai na bado upo kwenu unagombea rimoti ya tv na wadogo zako jitafakari

Kama umewahi kutumia haya majani ya chai na bado upo kwenu unagombea rimoti ya tv na wadogo zako jitafakari

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Maisha yana safari ndefu sana usipofunga mkanda haswa unaweza zeekea nyumbani hasa kwa sisi tuliotoka kwenye familia masikini.

Nakumbuka wakati nimepata ajira kampuni Fulani ujira ulikuwa mdogo sana licha ya elimu niliyo nayo ilinibidi nifanye hivyo hivyo mshahara ulikuwa 200k kwa mwezi.

Kipindi hicho bado nipo home, nyumbani kila kitu nilikuwa napata licha ya kupata kila nitakacho sikuridhika kukaa pale maana niliona nampa mzigo mkubwa mzazi wangu Mama baba alisha tangulia mbele za haki ( RIP)

Nikamwambia bi mkubwa mimi nataka nikajitegemee, akagoma akasena wewe bado sana kwanza tu kazi umeanza juzi hakuna kwenda kokote.

Baadae nilifanya maamuzi ya kuondoka nyumbani kwa nguvu japo bi mkubwa hakunipa baraka maana hakukubaliana na hatua niliyochukua.

Maisha ya kigheto gheto yakaanza bi mkubwa hakuta kuja hata kujua ninapo ishi 🤣🤣🤣 kasusa.

Aiseeh, nilikuwa najimeki siyo masihara ndani ya muda mfupi gheto likapendeza, Mungu siyo Athumani nikapata kazi sehemu nyingine kidogo masilahi mazuri mambo yakanoga, sasa Nina mke na mtoto mmoja, 🤣🤣🤣 sasaivi bi mkubwa anakuja home anacheza tu na mjuu wake asusi tena 🤣🤣🤣

FB_IMG_1645442700038.jpg
 
Kumiliki gheto, mke na mtoto tayari unajiona una maendeleo! ....kuna jamaa aliwahi kuniambia bwana mwizukulu mgikuru ukiwa mpanda katavi unatafuta dili la laki tano wakati huohuo yupo mwenzio mwanza anatafuta dili la milioni tano...usiridhike na ulipo leo .
 
kumiliki gheto, mke na mtoto tayari unajiona una maendeleo! ....kuna jamaa aliwahi kuniambia bwana mwizukulu mgikuru ukiwa mpanda katavi unatafuta dili la laki tano wakati huohuo yupo mwenzio mwanza anatafuta dili la milioni tano...usiridhike na ulipo leo .
Nilimiliki enzi hizo mkuu wakati naanza maisha.
 
Pole mkuu ondoka nyumbani, ukaishi kwako.
sasa nipo kwenye ujenzi wa nyumba yangu ya pili nishapaua kila kitu ndo namalizia baadhi ya madirisha yalopelea. Ofkozi nyumba zangu zote ni kwaajili ya biashara ikiwemo kulaza wageni, kupangisha watu na fremu za maduka.

na nipo kwetu maisha yanaendelea. Pia hivi karibuni ninafanya kaukarabati kadogo hapa kwetu kasichopungua milioni 17.6, baada ya kukamilisha nyumba yangu hii mpya ya pili.
 
Ongera mkuu, sasa niwakati wa kwenda kuishi kwako.
 
Kuondoka nyumbani ndio maendeleo?
What if mtu unakaa nyumbani na bado unamiliki majumba?
 
Back
Top Bottom