Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Safari za zamani south ilikua kisanga wallah, nakumbuka miaka hiyo ya tisini mwenetu Msafiri Mungu amrehemu aliiba tv la chogo kwao ,

Akaiba hela za hesabu ya malori ya mchanga yale ,akaingia kitaani akakodisha na baskeli kama mitaa minne hivi akaenda kuuza na safari mbele kwa mbele ,

Kumbe bhana kuna majamaa ndio yalimtia wenge Msafiri baada ya kuona kwao ana uwezo wakapanga wamtumie kupata hela kisha wamuache🤣🤣

Wazee ikumbukwe kipindi hiyo ni kuzamia meli tu hakuna cha boda la wapi wala la wapi basi haooo wakayeya mpaka dar na kuanza kupiga ramani ya meli gani itaondoka kwenda South

Nb,( wale wazamiaji kipindi kile walikua wanajua hadi meli fulani nahodha wake anaitwa fulani ,meli fulani itaondoka baada ya muda fulani au meli fulani itakuja baada ya muda fulani )

Basi walipofika "daslamu wakapata taarifa zote za meli maarufu kwa uzamiaji miaka hiyo jina limenitoka ila kama kuna wakongwe wanaweza ikumbuka hiyo meli

Basi wahuni wakampanga mwenetu Msafiri we lete hizo hela kuna jamaa hapo tumefanya nae mchongo atupitishe mpaka sehemu za ndani ndani ya meli,

Bhana bhana Msafiri akatoa kibunda akajikunyata kusubiri masela wamfuate wakapande dungu wasepe bwnaa bwana weee, alikaa mpaka siku ya tatu kwa mbali aliona mzigo unapiga honi nyingi sanaa , hapo hapo machozi yalimbubujika kama Lucas Mwamshamba akajua tayari kaingizwa king

Huku kwao habari zikaja jamaa amezamia mama yake ikawa ni kilio mwanzo mwishoo,

Ikumbukwe Msafiri hapo hakuachiwa hata mia mbovu

Akaanza kuishi kama chokoraa feri hapo ,kurudi home anaona noma ila ngoma ilivyozidi kuwa ngumu akarudi home na ubwabwa tukala wa kisomo ,

Ndipo mwana akatupa mkasa mzima🤣🤣🤣

Nimekumbuka hiki kisa cha muda kidogo
 
Hahaha hapo kwenye swala la kuzamia umenikumbusha mbali sana mkuu 🤣🤣🤣
 
Pole sana mkuu!

Bado upo SA?
 
Pole sana mkuu!

Bado upo SA?
Huyu bingwa kama sikosei kuna sehem aliandika kuwa amesharudi bongo kuendelea na maisha yake. Sema alifanya la maana kuandika ushuhuda wake kwa kile ambacho kiliwahi kumtokea katika nchi hii na kuwafungua wale wasiojua macho.
 
Sasa mkuu kama chenji imekosekana na pesa unazo unatakiwa umpatie dereva?
 
Ukiwa bado fresh panda train achana na hizo daladala wanazoziita tax.

Train zimepita location zote muhimu.
Train sawa, lkn kuna route za location nyingine ni hatari, ile route ya Philip to Kyalitsha huko wee kukabwa nnjennje, route ya usalama zaidi niya Wyneburg, Bellville to Strand na ile ya Miuzngburg, na kuna hii inayo pita Levi's town to UniBell nayo ipo kimya mchana nayo ni hataree
 
South africa South africa lazima nijeee tu...
 
Sasa mkuu kama chenji imekosekana na pesa unazo unatakiwa umpatie dereva?
Ukikosa chenji unamwambia dereva akuchenjie, ila baada ya hapo usimshirikishe. Warudishie chenji wewe mwenyewe 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…