Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Mengine yote upo sahihi isipokuwa namba 2 umedanganya. South africa hakuna kazi kwa foreigners hata kama umesoma. Hao wazimbabwe wanapata kazi za hovyo tu na wanakuwa exploited as cheap labor. Dzonga kupata kazi rasmi ya kuajiriwa kihalali lazima uwe na critical skills ambazo raia hawana. Kuna sheria kabisa inayokataza waajiri kuajiri foreigners wasiokuwa na critical skills ambazo ziko in short supply. Kupata work permit ni ngumu hatari na hakuna mwajiri atakayekuajiri bila work permit. Wazimbabwe na foreigners wanaojiriwa as cheap labor wana karatasi za ukimbizi ambazo zinawaruhusu kuajiriwa. Kuwa na documents halali za kuingia SA hazikufanyi upate kazi.
 
Uko sahihi kabisa na umeeleza kwa ufasaha
Namba Moja ilinifanya niombe mkate ndani ya train nikitoa Musina kuelekea cape town maana hela iliishia beit bridge the rest is history ila SA iliniacha na experience Moja kubwa sana
Hii kwa sisi wazoefu wa mambo huwa tunaiita South teacher (sauzi ticha) badala ya South Africa. Maana ukiishi hapa mwaka mmoja tu ni elimu tosha 🀣🀣🀣
 
umesomeka baba Khumbu! Uko poa?
 
Siku hizi South sio ile ya enzi zile vijana wakirudi kusalimia wanarudi well of tofauti na sasa vijana wanaenda alafu hawarudi na wakirudi mateja tena kwa kurudishwa
Maisha yamebadilika. Enzi zile South ilikuwa na watu wachache sana ukilinganisha na sasa hivi. Kila biashara iwe ya halali au haram ilikuwa inalipa na fedha zina thamani.

Leo hii watu ni wengi mno, kila mtu anafanya biashara halali na haram, upatikanaji wa hela umekuwa sio easy kivile, thamani ya fedha yao imeshuka sana. So kwa wale wasiojielewa vizuri na wanaosahau kilichowaleta lazima wawe mateja au machizi.
 
Asante sana kwa ufafanuzi mzuri mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…