Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Kumbe na wewe umemuona? [emoji23][emoji23][emoji23] huyo jamaa amenifurahisha sana
Ni kama wale husoma biashara kwenye vitabu wanakuwa na nadharia zao vichwani
Hao watu ambao hawajawah kutafuta pesa ni shida tupu , wanaonaga kama watu wengine akili hawana, subiri tu life liwafundishe
 
Fursa vp mbona umefunga DM.....nimekuchek
 
Nimeenda mpk huko vijijini kabisa...kufatilia hii kitu!
Minada inafanyika daily wewe tu pesa yako kununua na kujua wataka was Aina gani ili usipigwe bei..
Napenda kusema hivi kama mtumishi wa Umma yakupasa ufanye wikiendi tu la sivyo itakugharimu maana kuna kulala huko huko km mzigo haujatosha na ni vzr pia ufanye mwenyewe Ili kuepusha lawama au muandikishane
Kaka ameelezea kila kitu na kwa uwazi kabisa hajaficha kitu!
Ila Nilichopenda Kondoa warangi watu wazuri sana hongera zao!
 

Aise mimi mwenyewe warangi niliwapenda sana mrangi Asanteni sana.
 
Kaka ningeomba unitajie vijiji ulivyotembelea na ufikaji wake huko, na kama unapata mzigo unawasafirishaje mpaka kiwandani? Mana nna mpango wa kufanya ziara na mimi huko vijijini kbl cjaingia rasmi ktk huo mchongo..ili nijue km naweza kupata bidhaa ya kutosha ili nione tija ya hii biashara.
 
Jana kulikua na mnada mtiriangwi,minada inaenda kwa tarehe Leo ulikuwepo Gwandi Wilaya ya Chemba!
Usafiri upo kuna magari ya minada pia!Mimi nilienda majuzi nilienda majuzi nimesavei sana tu!ukiwa tayari ntafute!
Mzigo pesa yako tu!
 
Kwa kuanzia ni mtaji kiasi gani mtu anaweza kuanza nao?
 
Mkuu vipi ulishaanza mchakato?
 
Jana kulikua na mnada mtiriangwi,minada inaenda kwa tarehe Leo ulikuwepo Gwandi Wilaya ya Chemba!
Usafiri upo kuna magari ya minada pia!Mimi nilienda majuzi nilienda majuzi nimesavei sana tu!ukiwa tayari ntafute!
Mzigo pesa yako tu!
shukrani, haina shida tutatafutana kwa infor zaidi...ila usalama upo huko watu wasijegundua una pesa hlf ukaviziwa ukapigwa robber.😅
 
Mkuu vipi ulishaanza mchakato?
Nimefanya upekuzi wa mazingira ya kondoa mpaka kiwandani . Ni hivi kwa sasa wakulima wamepata hela ya mbaazikwahiyo mbuzi wana bei kidogo . Kwa mujibu wa ushauri wa mwenyeji wangu alishauri nianze mwezi wa 11. Hata hivyo tar 15 Oct naanza mdogo mdogo. Kiwandani soko lipo wazi kabisa na bei ni 8500/kg. Karibu tupambane
 
kwa uzoefu kidogo hiko hiv, mvua zikinyesha za kutosha na mipaka kufungwa1.nchi inapata neema ya mazao ya nafaka na bei kushuka. 2.maumivu yanakwenda kwny unga wa mahindi sbb watu upendelea kula wali kwsbb bei ya mchele inakua chini wkt mwengine karibu sawa na bei ya unga wa mahindi. 3.pumba za mahindi bei upanda sana sbb watu hatuli tena ugali. 4.sbb nafaka ipo ya kutosha wafugaji nao hawaoni sbb ya kuuza mifugo yao sbb nao ni wakulima siku hizi lkn pia akiuza hata mbuz mmoja tu anaweza kununua chakula kingi hivyo mifugo upanda bei sana. 5.kwa vile mvua zilikua za kutosha hivyo nyasi kwaajili ya mifugo yao pia zinakua nyingi hivyo mfugaji halazimishwi na kitu chochote kuuza mifugo yake na kwanza sio utamaduni wa mfugaji kuuza mifugo yake ile ni pride tu wanapenda kuona wanamifugo mingi bila kujali kama inawafaidisha au la!
 
Solution hapa ninayoiona ni mtu kuingia chimbo na kuanza kufuga mwenyewe huko usingidani au popote. Labda sasa aje mtu mwenye uzoefu na ufugaji atuelezee changamoto zake. Kwasababu kwa mtizamo wangu ukiweza kufuga ukauza mbuzi hapo kiwandani na ukawa na uwezo wa kusupply consistently basi unaweza kumaximize faida mara dufu.
 
Jana kulikua na mnada mtiriangwi,minada inaenda kwa tarehe Leo ulikuwepo Gwandi Wilaya ya Chemba!
Usafiri upo kuna magari ya minada pia!Mimi nilienda majuzi nilienda majuzi nimesavei sana tu!ukiwa tayari ntafute!
Mzigo pesa yako tu!
Mkuu ninapenda kukupongeza sana na nimependa sana spirit yako!! Tangu huu mjadala umeanzishwa nimekuwa nikiufuatilia na nimeona una nia dhabiti na umeenda physically kiwandani na Ukaenda Kondoa pia, Big up!!! Nilichogundua watu wengi hasa wanaume hap JF ni lele mama wanapenda kutafuniwa hadi kumezeshwa imagine mchongo wameshapewa wanaingia kwenye simu zao na kuomba simu, hawa ndio hufuga na kulima kwa simu wakiwa kitandani (watoto wa mama, vijana walaini na nyororo, vijana wa kushinda mlimani city).

Njoo inbox tupange namna ya kushirikiana.
 
Hili la watumishi ni kweli toka Mkuu Jebel alivyoanza kuelezea huu mchongo niliona kabisa mtumishi ukifanya hii ni lazima kazini ulege lege au kwenye business ulege lege. Hivyo nilikata shauri kuifanya lakini na partiner ambaye hajaajiriwa. Pia naona kama mtu upo serious ba uwezo upo ni vyema kuestablish eneo na kuanza kufuga kwa wingi.
 
Upo sahihi Mkuu, nitakuwa ninakucheck. Ngoja nianze na utafiti. Leo ninaelekea Kibaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…