Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Mkuu unafugia wapi?
 
Mkuu unafugia wapi?
 
Wabongo wanapenda kutafuniwa jaman khaaa
 
Jana kulikua na mnada mtiriangwi,minada inaenda kwa tarehe Leo ulikuwepo Gwandi Wilaya ya Chemba!
Usafiri upo kuna magari ya minada pia!Mimi nilienda majuzi nilienda majuzi nimesavei sana tu!ukiwa tayari ntafute!
Mzigo pesa yako tu!
Nakubali mkuu upp real sana nimeona effort yako since day, toka hii theard imekuja jf
 
una maana gani wanawashughulikia mkuu
 
lakini watu tunatofautiana mkuu...yawezekana wewe unaaproch faida kubwa Sana ndo sababu jamaa mwingine hapo kasema ana mtaji was laki tatu
 
Unaweza ukahisi umeandika kwa kupoteza muda ila ukweli ni kuwa kuna watu tayari umewapa wazo zuri sana la biashara na soon wataanza kulifanyia kazi. Hongera sana mkuu kwa hili wazo una roho ya kitajiri na utafanikiwa sana maishani mwako.
Mimi mmoja wapo.
 
Asante sana Mkuu, biashara hii nimekuwa naifikiria Kwa muda sasa, hivi nimewasiliana na jamaa zangu Dodoma but hawajaonyesha ushirikiano mzuri ila nadhani week ijayo nitaenda huko kuangalia ni namna gani naweza kuifanya hii, nikianza kidogo kidogo.
 
Au bora wangenunua Mbuzi kwa kuzingatia Live weight..

Waseme kwa mfano Mbuzi hai tukimpima uzito tunakulipa let say Tsh. 2000/kg kisha wanawapima wanakulipa chako wewe ukishuhudia..
 
Hakuna biashara hapo biashara ina mirorongo mingi Alafu Mimi niweke mfano laki 8 ninue mbuzi wa elfu50 wawe 16 kwenye kila mbuzi mfano awe na kilo 9 sawa na 63000 ukitoa matumizi nibaki na 6000 faida kila mbuzi kwahiyo 6000 * 16= 96000 Tsh 96000 siwezi huo ujinga biashara zenyewe na wachina sijui wahindi bado kwenye kilo wakupige
 

Mtaji wa 800,000/= faida 96,000/= Sawa na 12%. Hii biashara siyo mbaya Mkuu labda tu kila mmoja ana namna yake ya kuwaza.

800,000/= faida 96,000/= maana yake ukiwa na 8M tu faida 960,000/= approximately to 1M na mzunguko huu ni ndani ya week moja tu maana yake kwa mwezi ukifanya mizunguko 3 you’ve 3M...hii biashara hata MO anaweza kuifanya.
 
Wengine sio wafanya Biashara bro , hua wanaangalia angle ya "ni kwa namna gani hili jambo haliwezekan"
 
Wahindi wenyewe wanetupiga Sana kwenye viwanda vya samaki!
 
Wewe bwa
Wewe bwana unawezaje kutoa 800000 kwakutafuta 96000 Alafu bado umewakabizi mzigo eti utapigiwa simu au kutumiwa meseji yaani
 
Ila bro haiko simple kama unavyoilezea hapa, pipo tushaingia field tumeona mziki wake ktk kupata hao mbuzi...tumebaki kushangaa tu, mana mafanikio tuliyokuwa tunayawaza baada ya kusoma huu uzi ni magumu mno kuyafikia japo inawezekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…