Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Boer wangu na Galla sio kwa ajili ya kiwandani my dear hizi nataka kuzaliza kwa wingi cause ni adimu then soko lake lipo! nimeeleza wazi kuwa nakusanya local kwa ajili ya kiwandani,,ila ukipata majike local ukapandisha na Galla au boer utapata vitu amazing wacha tuendelee kupambana
Mkuu unafugia wapi?
 
Kaka ningeomba unitajie vijiji ulivyotembelea na ufikaji wake huko, na kama unapata mzigo unawasafirishaje mpaka kiwandani? Mana nna mpango wa kufanya ziara na mimi huko vijijini kbl cjaingia rasmi ktk huo mchongo..ili nijue km naweza kupata bidhaa ya kutosha ili nione tija ya hii biashara.
Wabongo wanapenda kutafuniwa jaman khaaa
 
Jana kulikua na mnada mtiriangwi,minada inaenda kwa tarehe Leo ulikuwepo Gwandi Wilaya ya Chemba!
Usafiri upo kuna magari ya minada pia!Mimi nilienda majuzi nilienda majuzi nimesavei sana tu!ukiwa tayari ntafute!
Mzigo pesa yako tu!
Nakubali mkuu upp real sana nimeona effort yako since day, toka hii theard imekuja jf
 
Kusafirisha mbuzi na kondoo umbali mrefu inawezekana kabisa cha msingi zingatia haya;
Moja; jitahidi sana kuwasafirisha usiku au wakati ambao joto/jua siyo kali sana
Pili; Jitahidi kumpata kijana atakayekuwa anawaamsha pale wanapolaliana. Kuna vijana wanafahamu vema shughuli hii japo ikifika usiku wanawashughulikia pia mbuzi na hasa kondoo[emoji851][emoji851][emoji851].

Tatu; Zingatia kipengele A na B hapo juu.
una maana gani wanawashughulikia mkuu
 
Fala Sana wewe. Umeongea kama vile wewe ni wale fai waka mnaofanya Kazi hapo kiwanda.

Kama biashara inaweza kukupa Faida ya 10k alafu wewe ukawa unapata 3k ukaona poa kisa unapata Faida nasi wewe utakuwa mjinga wa mwisho.

Anyway nisamaraizi kwa kusema nimadamu tumatofautiana.binafsi huwa naangalia gaida na mfa niliotumia pamoja na kapital niliyoweka.

Kwa mfano niweke eti niwe na mtaji wa mbuzi 60 alafu gaida yake iwe 360k kwa mda wa wiki mbili hata kwa wiki sifanyi.

Kama nilivyosema tunatogautiana kimtazamo na mipango. Bila kusahau uwezo pia.

Siku nyingine uwe na adabu huwezi jua nani atakupa fursa.

Na kukuthibitishia ninacho kuambia kuna biashara nimeamua kutuma M7 Kati ya hizo M7; 1.3M ni tiketi ya ndege; 500k kula na kulala lakini Faida yake ambayo iko projected ni 6M. Nitaleta ushuhuda suni
lakini watu tunatofautiana mkuu...yawezekana wewe unaaproch faida kubwa Sana ndo sababu jamaa mwingine hapo kasema ana mtaji was laki tatu
 
Unaweza ukahisi umeandika kwa kupoteza muda ila ukweli ni kuwa kuna watu tayari umewapa wazo zuri sana la biashara na soon wataanza kulifanyia kazi. Hongera sana mkuu kwa hili wazo una roho ya kitajiri na utafanikiwa sana maishani mwako.
Mimi mmoja wapo.
 
Habarini Waungwana!

Leo nimeona nitoe mchongo wa biashara ambayo binafsi nimewahifanya kabla sijapata ajira na natarajia kuendelea kufanya baada ya ajira kuisha.

Uzuri wa biashara hii, pamoja na kuwa na faida nzuri, soko lake ni la uhakika sana na changamoto zake ni chache sana na zinakabilika kwa mtu ambaye ameamua kwa dhati kutafuta.

BIASHARA YENYEWE NI KUNUNUA MBUZI NA KWENDA KUUZA KIWANDANI.

A. Upatikanaji wake
Upatikanaji wa mbuzi. Pamoja na mambo mengine ambayo Tanzania tumejaliwa ni mifugo hasa mbuzi. Kuna upatikanaji wa uhakika wa mbuzi na kondoo katika mikoa ya Dodoma (Urangini), Singida, Tanga na Tabora. Kwa kule KONDOA kuna Warangi wazuri sana madalali ambao ni waaminifu sana tofauti na madalali ambao tumewazoea katika jiji la Dar.

Kwa ushauri wangu, sehemu nzuri zaidi ya kununua mbuzi kwa bei nzuri, wenye ubora (Uzito) na faida nzuri, urahisi wa upatikanaji wake na hata urahisi wa usafirishaji ni KONDOA (Urangini). Huku kuna minada ya mbuzi kila siku na hivyo kwa siku unaweza kununua hadi mbuzi 50 na zaidi kama una mwenyeji mzuri.

B. Soko lake
Binafsi ningependekeza kupeleka kiwandani hasa kiwanda cha TanChoice kilichopo Soga, wilani Kibaha mkoa wa Pwani. Hapa utaweza kuuza idadi yoyote ya mbuzi japo huwa wanapenda walau uwe na mbuzi kuanzia 20 (hii ni idadi wakati mimi napeleka inawezekana kukawa na mabadiliko kwa sasa).
Sehemu nyingine ni Longido-Arusha katika kiwanda cha Eliya Food Ltd japo kwa Arusha kuna wanunuzi wengi hasa Wakenya wanatoa bei nzuri sana.

C. Bei ya mbuzi
Kwa kuwa mbuzi hununuliwa vijijini bei yake siyo kubwa kwani ina range kati ya 30-70 elfu. Mbuzi wa 30 elfu anaweza kukadiriwa kuwa na uzito wa kilo 7 au 6.5. Mbuzi wa 70 elfu anaweza kufikisha hadi 12Kg au 13Kg. Kiwandani hawapendelei sana mbuzi wakubwa sana kwa hiyo ni vema kuwa makini katika selection ya mbuzi wa size ya kati ili upate faida nzuri na soko la uhakika.

D. Bei ya nyama kiwandani
Wakati mimi napeleka mbuzi katika kiwanda cha TanChoice, walikuwa wakinunu kwa Tsh 7000/Kg kwa mbuzi na Tsh6800/Kg. Kwa Arusha inasemekana bei iko juu kidogo ila Arusha niseme ukweli sana information za kutosheleza kwani nilienda trip moja tu.

E. Kadirio la faida
Kama mbuzi amenunuliwa kwa kwa Tsh 50,000/= halafu akatoa Kg 9 za nyama ambazo ni sawa na Tsh 63,000/= faida yake itakuwa karibu 6,000Tsh hadi 7,000Tsh kwa mbuzi mmoja. Hapa unakuwa umetoa Gharama zote kuanzia usafiri kutoka Dar nimetumia kwa wakazi wa Dar hadi Kondoa, kulala guest, usafiri kwenda minadani, kuwasafirisha kutoka minadani hadi Kondoa mjini, ushuru wake na vibali, usafiri kwenda Dar kiwandani, chakula na mengineyo.

F. Changamoto zake
Kusema ukweli kila kazi ina changamoto zake na hasa inapokuja suala la biashara, basi changamoto haziepukiki. Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine ina makandokando yake kama ifuatavyo;
  • Kuna wakati kunakuwa na wanunuzi wengi wa mbuzi kwa hiyo competition inakuwa kubwa sana na kupelekea wauzaji kupandisha bei na hivyo faida kukuachia kidogo sana
  • Usipokuwa makini madalali ambao wameshawahi kufika Dar basi lazima watakulalia katika ununuzi wa mbuzi. Binafsi kwa mara ya kwanza nilijikuta kwa kila mbuzi mmoja napigwa 2000-3000Tsh. Yaani mbuzi anamununua 40,000Tsh halafu ananiambia amemchukulia 43,000Tsh.
  • Kuna wakati upatikanaji unakuwa mgumu hata kama wanunuzi siyo wengi. Baadhi ya siku unakuta wanaoleta mbuzi minadani ni wachache sana na hivyo unaweza kutumia siku nyingi kupata mzigo mzuri.
  • Uwezekano wa kuibiwa mbuzi. Kumbuka munapowanunua mbuzi kutoka mnadani basi munawahesabu na kila mnunuaji anaweza label ya kwake kwenye mbuzi kwa kutumia mkazi. Mimi ilikuwa nachora herufi K ambayo ni herufi ya kwanza ya jina la wife. I love her and she knows that. Baada ya hapo munawaweka mbuzi pamoja na kumkabidhi kijana anayewaswaga kutoka mnadani(minada ipo maporini sijui kwanini) hadi kuwafikisha mjini. Baada ya hapo mbuzi wote wanawekwa kwenye gari na kupelekwa kiwandani. Wakati mwingine mnaweza kupata gari linaloishia Dodoma na kulazimika kuunganisha na wanunuzi wengine wanaofikishia mzigo wao Dom mjini na kisha kutumia gari moja kupeleka kiwandani. Sasa inaweza kutokea au kijana anayewaswaga kutoka mnadani akapiga pande mbuzi mmoja au vijana wanaowaangalia na kuwapeleka malishoni kama unanunua mzigo mkubwa kwa siku kama tatu au zaidi.
-Mbuzi kukosa uzito wa kutosha. Hapa ndo sehemu ya kuwa makini sana. Mbuzi wanaotoka Tabora kwa mfano, uzito wake ni mdogo sana wanapochinjwa tofauti na mbuzi wa Kondoa. Kwa hiyo ukinunua mzigo Tabora kwa bei kubwa kuna uwezekano ukaingia loss na kurudi hapa kunitukana na kunilaumu. Naomba kwa atakayekuwa interested aulize maswali ya kutosha na ikiwezekana afike Kondoa kufanya preliminary investigation and research. I do recommend Kondoa kwa warangi.
G. Malipo

Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma. Hapa kwenye malipo mara nyingi hakuna usumbufu japo binafsi nilifikiria sana reliability yake yaani wanakwambia umepata KG 500, kwa mfano, inakuwa ni hiyo hiyo au inawekana ilikuwa zaidi?

Hitimisho
Kila biashara ina changamoto kama nilivyosema mwanzoni lakini biashara ambayo soko lake ni la uhakika na mzunguko wake ni wa uhakika basi daima huwa ni biashara nzuri. Kwa yeyote anayependa kujaribu biashara hii, nashauri afanye utafiti wa kutosha na kisha aanze na mzigo kidogo hata wa 1M kwanza aone faida yake, changamoto zake n.k.

ASANTENI KWA MDA WAKO NAKUTAKIENI MAFANIKIO KWA KAZI UFANYAYO.

Asante sana Mkuu, biashara hii nimekuwa naifikiria Kwa muda sasa, hivi nimewasiliana na jamaa zangu Dodoma but hawajaonyesha ushirikiano mzuri ila nadhani week ijayo nitaenda huko kuangalia ni namna gani naweza kuifanya hii, nikianza kidogo kidogo.
 
Kama hao wamiliki wa kiwanda ni wa China, narudia tena ni waChina mimi siwaamini hata kidogo maana hawa ni wahalifu sana hivyo nahisi kwa asilimia kubwa ninyi mnaowauzia mbuzi mnapigwa sana.Ki utaratibu ilitakiwa waweke utaratibu wa kila muuza mbuzi ashuhudie yeye mwenyewe au mtu aliyemteua uzito wa nyama tena kwenye mizani iliyo hakikiwa na watu wa vipimo (WMA).
Au bora wangenunua Mbuzi kwa kuzingatia Live weight..

Waseme kwa mfano Mbuzi hai tukimpima uzito tunakulipa let say Tsh. 2000/kg kisha wanawapima wanakulipa chako wewe ukishuhudia..
 
Hakuna biashara hapo biashara ina mirorongo mingi Alafu Mimi niweke mfano laki 8 ninue mbuzi wa elfu50 wawe 16 kwenye kila mbuzi mfano awe na kilo 9 sawa na 63000 ukitoa matumizi nibaki na 6000 faida kila mbuzi kwahiyo 6000 * 16= 96000 Tsh 96000 siwezi huo ujinga biashara zenyewe na wachina sijui wahindi bado kwenye kilo wakupige
 
Mtaji wa 800,000/= faida 96,000/= Sawa na 12%. Hii biashara siyo mbaya Mkuu labda tu kila mmoja ana namna yake ya kuwaza.

800,000/= faida 96,000/= maana yake ukiwa na 8M tu faida 960,000/= approximately to 1M na mzunguko huu ni ndani ya week moja tu maana yake kwa mwezi ukifanya mizunguko 3 you’ve 3M...hii biashara hata MO anaweza kuifanya.
 
Wengine sio wafanya Biashara bro , hua wanaangalia angle ya "ni kwa namna gani hili jambo haliwezekan"
 
Kama hao wamiliki wa kiwanda ni wa China, narudia tena ni waChina mimi siwaamini hata kidogo maana hawa ni wahalifu sana hivyo nahisi kwa asilimia kubwa ninyi mnaowauzia mbuzi mnapigwa sana.Ki utaratibu ilitakiwa waweke utaratibu wa kila muuza mbuzi ashuhudie yeye mwenyewe au mtu aliyemteua uzito wa nyama tena kwenye mizani iliyo hakikiwa na watu wa vipimo (WMA).
Wahindi wenyewe wanetupiga Sana kwenye viwanda vya samaki!
 
Wewe bwa
Mtaji wa 800,000/= faida 96,000/= Sawa na 12%. Hii biashara siyo mbaya Mkuu labda tu kila mmoja ana namna yake ya kuwaza.

800,000/= faida 96,000/= maana yake ukiwa na 8M tu faida 960,000/= approximately to 1M na mzunguko huu ni ndani ya week moja tu maana yake kwa mwezi ukifanya mizunguko 3 you’ve 3M...hii biashara hata MO anaweza kuifanya.
Wewe bwana unawezaje kutoa 800000 kwakutafuta 96000 Alafu bado umewakabizi mzigo eti utapigiwa simu au kutumiwa meseji yaani
 
Mtaji wa 800,000/= faida 96,000/= Sawa na 12%. Hii biashara siyo mbaya Mkuu labda tu kila mmoja ana namna yake ya kuwaza.

800,000/= faida 96,000/= maana yake ukiwa na 8M tu faida 960,000/= approximately to 1M na mzunguko huu ni ndani ya week moja tu maana yake kwa mwezi ukifanya mizunguko 3 you’ve 3M...hii biashara hata MO anaweza kuifanya.
Ila bro haiko simple kama unavyoilezea hapa, pipo tushaingia field tumeona mziki wake ktk kupata hao mbuzi...tumebaki kushangaa tu, mana mafanikio tuliyokuwa tunayawaza baada ya kusoma huu uzi ni magumu mno kuyafikia japo inawezekana.
 
Back
Top Bottom