Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

huko wanakopatikana hao mbuzi ni Kondoa kijiji/mtaa gani? Au ukifika tu kondoa ukiulizia mnada wa mbuzi utapelekwa? Naomba details zaidi jinsi ya kufika huko wanakonunua mbuzi na gharama zakr za usafiri.

Na unazungumziaje uhakika wa soko huko kiwandani? Mana nisije kuchukua mbuzi wa kutosha hlf nafika kiwandani..naambiwa wanastock ya kutosha hawahitaji tena...au inabidi nifike hapo kiwandani kwnz kuona kama wanao uhitaji?
 

Uko sahihi mkuu utaratibu bado siyo mzuri, binafsi nashangaa sana kwanini serikali haiingilii kati suala hili. Kipindi cha raisi wa awamu ya tano alikuwa amepanga kuanzisha utaratibu wa kupima mbuzi kabla ya kuchinjwa na kumlipa muuzaji kadri ya uzito uliopatikana. Japo wenye kiwanda siyo Wachina lakini ni wapigaji sana kwa sababu utumbo, ngozi, kichwa, miguu na kwato hawahesabu kwenye uzito ilhali vyote wao wanauza na kupata faida. Lakini kwenye biashara mkuu unachopaswa kuangalia ni faida yako na siyo ugomvi na mnunuzi wako.
 

Mkuu ukifika Kondoa mjini ulizia madalali au wanunuzi wa mbuzi, watakupeleka minadani. Minada inakuwa vijijini kila kijiji kina siku yake na pale Kondoa mjini pia kuna siku yake.

Kuhusu soko hadi mimi nasitisha baada ya kupata ajira nje ya nchi, lilikuwa la uhakika sana na ilikuwa March mwaka huu. Hata ungepeleka lori zima wananunua, kiwanda ni kikubwa sana na hawa jamaa wanapeleka nyama ya mbuzi, nchi za kiarabu, Oman, Qatar na kwingineko kwa hiyo soko ni uhakika sana.
 
Vibali Ni mpaka office za TRA sio....

Hapana mkuu ukinunua mbuzi unakatiwa ushuru halafu unapounganisha na wanunuaji wenzako mnakata kibali kwa pamoja. Huwa siyo usumbufu sana. Narudia binafsi nilipenda sana Warangi wana roho nyeupe kama ngozi yao, hawana roho ya k….gga! Hahhahhahahaha
 
Naiona changamoto katika kupata nafasi huko viwandani kuwauzia..

Hii haina tofauti sana na kule kwa walima miwa na kuwauzia kiwanda cha sukari,wakulima wamelia sana maana wengi walilima ila kiwanda hakikununua kwa wingi..

Hapana mkuu, hii inautofauti sana, kuna competition sana ya kununua mbuzi ukizingatia kiwanda ni kikubwa sana wanauwezo wa kuchinja mbuzi wengi sana, lakini pia kumbuka kuna soko la mbuzi pale Pugu na bar pia.
 
Nilikuwa karibu nichanganye mambo kidogo hasa pale nilipoona DODOMA (Urangini) na baadaye tena nikaona KONDOA (Urangini)! Ndipo nilipokumbuka kuwa Kondoa iko mkoa wa Dodoma hivyo ni sawa ukisema Dodoma - Kondoa (Urangini). Ni elimu nzuri kwa wafanya biashara ila hizo gharama ndogo ndogo ambazo hukuziweka zingesaidia sana kutoa mwanga wa faida na hasara katika biashara hii, ambayo inaonekana haina shida ya MASOKO.
 
Mm niliwai kufanya hii biadhara ya mbuzi lkn nilikuwa nakwenda kuuza pugu. Ukiwa umezoea kufanya buashara ya nyanya ,vitunguu, mchele ,ukija kwenye buashara hii unakuta kuna changamoto nyingi sana , changamoto kuuubwa kumsafilisha mbuzi afike akiwa salama. Utakuta dari ina mbuzi 180 yaani wamebanana itabidi awepo mtu wa kuwainulia, kuna jamaaa aliuwa kondoo 5 kwa safali moja. Changamoto nyingine pale pungu vijana wa kikurya ni wezi sana wa mbuzi usipokuwa makini wakati wa kushusha unapigwa mbuzi hata 2 , ukinunua mbuzi ktk kijiji chochote kuna kibali unakata inategemea na sehemu kuna sehemu wanalipia sh 1000 kwa kila mbuzi na unapewa lisiti ya mashine. Sasa hapo unaweza ukajiongeza yule jamaa asikuandikie idadi ya mbuzi kwa hiyo kama umenunua mbuzi 50 unampa 40 eflu yeye anauandikia risiti ya 30 elfu ukiwa baada ya hapo kuna kibali kingine ambacho miaka ile tulikuwa tunalipa 1500 kwa kila mbuzi hiki ndio muhimu sana ambacho kinakufanya upite popote bila kupingwa,lkn hiki kibali cha pili huwa kinalipwa kwa gali nzima yaani anakata dalali wa gali na mara nyingi malipo hujumlishwa kwenye nauli.

Ukitaka biashara hii upate faida usinunue mnadani mm nilikuwa afikia kwa jamaa aafu tunaenda nyumba hadi nyumba pale unazungumza na muuzaji mpaka mwisho ,mnadani wateja wengi hupanda bei hii itakuganya nawe upande bei
 
Tatizo wanachinja usiku na huwa mbuzi ni wengi sana labda zaidi ya elfu 5 na wanakuwa wamechanganywa kutoka sehemu mbali mbali ni ngumu kuingia kiwandani kusubiria mbuzi wako wachinjwe na in short utaratibu wao uko hivyo, lakini they are reliable.


je kiwanda ni kimoja tu kwa dar na huko Arusha

na wanapokea Mbuzi siku gani au ni kila siku?

kiwanda kiko wapi kwa hapa dar,

kuna utaratibu gani wa kupeleka mbuzi wako.. unaandikishwa in advance ili kuwa supplier wao au unaweza tu ukaja na mbuz wakapokea..

na hizo alama mnaowaweka mbuzi mlikuwa unawaandika na nini au ndo kuwa piga chata na vyuma vya moto

Je wanapokea Aina nyingine za nyama kama vile ng'ombr au ni mbuzi tu
 
Sawa Mkuu barikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…