Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Asante kwa taarifa zenye kujitosheleza..umeeleza vizuri Sana.
Naomba nikuulize swali..lingine..wateja uliwapataje wa kununua nguruwe wengi kwa wakati mmoja..?
Mkuu,
Mimi niliunganishwa na mtu mmoja aliyekuwa anafanya hiyo biashara zamani (kwasasa nimepoteza mawasiliano naye)

Soko kubwa lilikuwa Mwanza (uwanja wa fisi) pale kuna jamaa ana mabanda, ukifika na nguruwe usiku mnawahesabu anaigiza kwenye banda, asubuhi mnapatana bei ( unawauza wazima) halafu yeye anachinja na kuwauzia jumla wale wanaokaanga na kuuza rejareja ( wanunuzi wadogo na wenye mabucha wanafata nyama pale)
 
tunaokaa huku mara muwoma tunaenda kuuza wap sasa kwane kiwanda cha nyama mkuu
 
Na sie tunataka hiyo ya kujikimu kwanza, maana mengine huja baadae safari moja huanzisha nyingine usichoke pengine babu wa huyo tajiri wa kiwanda alikuwa kama wewe
 
Mkuu unajua nini cha kufanya, mwenye dhiki hana haya, huu ni msemo wa waswahili walisema.
 
Asante sana
 
Kijana una upeo mkubwa, nimefurahishwa sana na comment yako hii. Ni ufafanuzi unaothibitisha Uwezo wako mkubwa wa kufikiri na kupambanua mambo kwa weledi.

Huyo sio kijana ni mwalimu mstaafu
 
Bila shaka jamaa anahamia phase nyingine,Top level ya food chain.
Watakaoingia kwenye hii biashara sa hivi atawauzia mbuzi na kuwapiga udalali.anatafuta mbuzi wa kumuingizia pesa .
Sio katika kila jambo unaweka dhana mbya tu..jifunze kuyaona mazuri ktk kila jambo. Kuna mtu alisema "matajiri wako bize kutafuta fursa, huku maskini wako bize wakidhani kila fursa nni utapeli"
 
Mkuu umenipa somo kubwa

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Katika Biashara yapasa ufanye
1. Mnyororo wote wa Biashara kuanzia malighali hadi soko

2. Faida na Hasara za Biashara

3. Fursa na Changamoto

4. Vitu gani vikitokea vinaweza kuharibu biashara yako

5. Upatikanaji wa Mtaji na RASLIMALI za kuendesha hiyo biashara

6. N.k
 
HESABU lako halikakaa fresh
 
Nataka fanya utafiti nikijiridhisha nianze mchakato japo kwa udogo wake. Nataka ikibidi niwapigie simu nione kama bado wananunua na terms zao zipoje? Nitakapowasikia na nikajiridhisha na mchakato basi niende kondoa machakani huko nako nikajifunze. Wadau mm ni msakatonge tuu nipo morogoro mjini hapa. Tushirikiane kutafiti hili alilotupa mwezetu. Ikishindikana kupata simu zao itabidi niende physically.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…