Dakika 30 zilizopita nimetoka Msibani Kumzika Mmoja wao ambaye Utumbo ulitoka Nje na ukarudishiwa kabla ya Kuzikwa.
Kesho tena kama nikipata Nauli na nikijua huko Msibani kuna Wali mzuri wa Nyama na Nazi naweza kwenda Kumzika mwingine huko huko.
Na kama kwa sasa ukiwa Unajiuliza ni kwanini ukiwa barabarani huwaoni tena Wabeba Mkaa / Mikaa katika Pikipiki zao na labda unayajua Majina yao jitahidi utembelee katika Makaburi ya Jirani unaweza ukayakuta huko yakiwa na Maua ya Kimaombolezo kwa juu.
Ikitokea una ama Ndugu yako au Mpenzi wako anayejishughulisha na Biashara hiyo ya Magendo ya Mkaa maeneo ya Mlandizi au Kibaha na kila ukimsihi asiende huko na bado analazimisha kwenda hakikisha akienda umuulize je, ikitokea Akafa huko angependelea azikwe Dar es Salaam au Kijijini Kwao Mkoani?
Askari Maliasili wa Mlandizi na Kibaha ( hasa Mkoa wa Pwani ) ambao Shughuli za Ukataji Miti holela na Biashara ya Magendo ya Mkaa inashamiri Hongereni kwa Kubeti na Roho za Watu na Mochwari wanazohifadhiwa kutokana na Utekelezaji wenu wa Kimedani.
Kinachonishangaza mno GENTAMYCINE ni jinsi Media za Tanzania zilivyo Kimya, hazijui Kunusa Taarifa Nyeti na Muhimu halafu Watu wa Kawaida mno ( tusio na mbele wala nyuma ) kama akina GENTAMYCINE tunazipata na hata Kushiriki katika Maziko au Kutembelea Wahanga ( Majeruhi ) Makwao au Mahospitalini.
Halafu Askari Maliasili wa Siku hizi je, huko Vyuoni Kwenu huwa mnafundishwa sana Somo la Kulenga / Shabaha?
Kwani Mashuhuda wa huko Mlandizi na Kibaha wasema mkiziinua tu Bunduki zenu na mkishusha Mtu Kaondoka mazima Ahera.