Kama una Ndugu au Mpenzi anafanya Biashara ya Magendo ya Mkaa Mlandizi na Kibaha mwambie aache kwani Askari Maliasili wa huko sasa hawatanii

Kama una Ndugu au Mpenzi anafanya Biashara ya Magendo ya Mkaa Mlandizi na Kibaha mwambie aache kwani Askari Maliasili wa huko sasa hawatanii

Huenda kuna jinsi wakishachomoka huko ndani wakifika huku barabarani huwezi watofautisha na wachuuzi wa halali. kwahiyo ni kuwawahi huko huko.
Bado sio stahiki ya kuwaua, wachukue hatua nyingine.
 
Mkuu hii operation ya kuwaua wauza mkaa mbona wameianza muda tu takribani miezi3 sasa walimuua jirani yetu mmoja almaarufu kunguru jamaa alikuwa mwendesha boza ya mkaa.

Tulipigiwa simu na wasamalia wema kuwa kuna mwendesha pikipiki kapata ajali pande za msoga ila tumefika eneo la tukio pikipiki na mkaa vyote vipo salama ila mwili wa marehemu ulikuwa umepigwa na kitu kizito utosini.
Duuuh
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Ungekuwa na Akili ungenishukuru tena mno GENTAMYCINE kwa Kukuletea hapa hii Taarifa Muhimu ambayo nina uhakika hakuna Media yoyote ile iliyoripoti.

Ukiwa Mpumbavu kamwe hutoweza Kunielewa wala kuielewa pia na Sanaa yangu ya Kipekee ya Uwasilishaji wa Mada na Masuala Mtambuka hapa JamiiForums na Tanzania kwa ujumla.
Hivi kwa mini gesi isipungue bei hadi sh 8000 tu kilimo sasa sh 26 mtungi mdogo Roxy
 
Dakika 30 zilizopita nimetoka Msibani Kumzika Mmoja wao ambaye Utumbo ulitoka Nje na ukarudishiwa kabla ya Kuzikwa.

Kesho tena kama nikipata Nauli na nikijua huko Msibani kuna Wali mzuri wa Nyama na Nazi naweza kwenda Kumzika mwingine huko huko.

Na kama kwa sasa ukiwa Unajiuliza ni kwanini ukiwa barabarani huwaoni tena Wabeba Mkaa / Mikaa katika Pikipiki zao na labda unayajua Majina yao jitahidi utembelee katika Makaburi ya Jirani unaweza ukayakuta huko yakiwa na Maua ya Kimaombolezo kwa juu.

Ikitokea una ama Ndugu yako au Mpenzi wako anayejishughulisha na Biashara hiyo ya Magendo ya Mkaa maeneo ya Mlandizi au Kibaha na kila ukimsihi asiende huko na bado analazimisha kwenda hakikisha akienda umuulize je, ikitokea Akafa huko angependelea azikwe Dar es Salaam au Kijijini Kwao Mkoani?

Askari Maliasili wa Mlandizi na Kibaha ( hasa Mkoa wa Pwani ) ambao Shughuli za Ukataji Miti holela na Biashara ya Magendo ya Mkaa inashamiri Hongereni kwa Kubeti na Roho za Watu na Mochwari wanazohifadhiwa kutokana na Utekelezaji wenu wa Kimedani.

Kinachonishangaza mno GENTAMYCINE ni jinsi Media za Tanzania zilivyo Kimya, hazijui Kunusa Taarifa Nyeti na Muhimu halafu Watu wa Kawaida mno ( tusio na mbele wala nyuma ) kama akina GENTAMYCINE tunazipata na hata Kushiriki katika Maziko au Kutembelea Wahanga ( Majeruhi ) Makwao au Mahospitalini.

Halafu Askari Maliasili wa Siku hizi je, huko Vyuoni Kwenu huwa mnafundishwa sana Somo la Kulenga / Shabaha?

Kwani Mashuhuda wa huko Mlandizi na Kibaha wasema mkiziinua tu Bunduki zenu na mkishusha Mtu Kaondoka mazima Ahera.

Mkuu wewe utakuwa ni wale wastaafu wa ikulu nazisoma code zako ni kama unajaa kwenye ramani zangu.. bado naendelea na intelligence yangu
 
Mkuu wewe utakuwa ni wale wastaafu wa ikulu nazisoma code zako ni kama unajaa kwenye ramani zangu.. bado naendelea na intelligence yangu
Nimecheka sana na mno Mkuu wangu.
 
Fujo zinatokea ,na polisi nao waliumizwa,ila kutumiaa risasi za Moto halikua Jambo zuri,sio la kufumbia macho
Kwahyo uko mlandizi ad wauza mkaa wamtaani yaan wale wamajumban wanaouza mkaa wakupima wamakopo wanahitaji wawe na vbali ?
Ama wenyewe mambo n shwari tu wanauza bla usumbufu
Kwan Mimi pia natamani nifanye Io biashara ya mkaa ya Kwa kopo nasyo Kwa jumla huko mlandizi.Je na hyo pia inahtaj vbali
 
Siku hizi ni hatari kuingia ingia bila taarifa kwenye hifadhi za wanyama na misitu utapoza maisha. Wanyama na miti vinathaminiwa zaidi kuliko binadamu
 
Back
Top Bottom