Kama una Ndugu au Mpenzi anafanya Biashara ya Magendo ya Mkaa Mlandizi na Kibaha mwambie aache kwani Askari Maliasili wa huko sasa hawatanii

Kama una Ndugu au Mpenzi anafanya Biashara ya Magendo ya Mkaa Mlandizi na Kibaha mwambie aache kwani Askari Maliasili wa huko sasa hawatanii

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Dakika 30 zilizopita nimetoka Msibani Kumzika Mmoja wao ambaye Utumbo ulitoka Nje na ukarudishiwa kabla ya Kuzikwa.

Kesho tena kama nikipata Nauli na nikijua huko Msibani kuna Wali mzuri wa Nyama na Nazi naweza kwenda Kumzika mwingine huko huko.

Na kama kwa sasa ukiwa Unajiuliza ni kwanini ukiwa barabarani huwaoni tena Wabeba Mkaa / Mikaa katika Pikipiki zao na labda unayajua Majina yao jitahidi utembelee katika Makaburi ya Jirani unaweza ukayakuta huko yakiwa na Maua ya Kimaombolezo kwa juu.

Ikitokea una ama Ndugu yako au Mpenzi wako anayejishughulisha na Biashara hiyo ya Magendo ya Mkaa maeneo ya Mlandizi au Kibaha na kila ukimsihi asiende huko na bado analazimisha kwenda hakikisha akienda umuulize je, ikitokea Akafa huko angependelea azikwe Dar es Salaam au Kijijini Kwao Mkoani?

Askari Maliasili wa Mlandizi na Kibaha ( hasa Mkoa wa Pwani ) ambao Shughuli za Ukataji Miti holela na Biashara ya Magendo ya Mkaa inashamiri Hongereni kwa Kubeti na Roho za Watu na Mochwari wanazohifadhiwa kutokana na Utekelezaji wenu wa Kimedani.

Kinachonishangaza mno GENTAMYCINE ni jinsi Media za Tanzania zilivyo Kimya, hazijui Kunusa Taarifa Nyeti na Muhimu halafu Watu wa Kawaida mno ( tusio na mbele wala nyuma ) kama akina GENTAMYCINE tunazipata na hata Kushiriki katika Maziko au Kutembelea Wahanga ( Majeruhi ) Makwao au Mahospitalini.

Halafu Askari Maliasili wa Siku hizi je, huko Vyuoni Kwenu huwa mnafundishwa sana Somo la Kulenga / Shabaha?

Kwani Mashuhuda wa huko Mlandizi na Kibaha wasema mkiziinua tu Bunduki zenu na mkishusha Mtu Kaondoka mazima Ahera.

1678947635197.jpeg

Hatar Sana chief
Vijana Wanadondoka huko hakuna mfano. au Hawa Askari Maliasili wa siku hizi wamepitia na Kozi ya Shabaha kwa Makomandoo Wetu au hapana kwani unaambiwa Wakiziinua Mtu utaona Pikipiki inaanguka kule, Mkaa Kwingine na Dereva nae Kwingine huku Kichwa kikipasuka au Utumbo wake Kutusalimia tunaowahi / Kuwasalimia wanaowahi Kuokoa.
 
Na kweli media zimezubaa.
Kwa mfano ile habari ya yule jamaa kukatwa sikio na mgoni wake. Wale wa sokoni
Bila wewe tusingeijua.
(Though chini ya kapeti wadau wanasema ni wewe ndo walipita na sikio 🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️)
 
Unafurahia watu kuwawa.?
Ungekuwa na Akili ungenishukuru tena mno GENTAMYCINE kwa Kukuletea hapa hii Taarifa Muhimu ambayo nina uhakika hakuna Media yoyote ile iliyoripoti.

Ukiwa Mpumbavu kamwe hutoweza Kunielewa wala kuielewa pia na Sanaa yangu ya Kipekee ya Uwasilishaji wa Mada na Masuala Mtambuka hapa JamiiForums na Tanzania kwa ujumla.
 
Kuna vitu vimebaki kama kanuni na daima watu hawawezi kuviacha leo hii hata gesi iuzwe elfu tano bado kuna watu wengi tu wataendelea kupikia mkaa.
ila kuua watu hovyo nako haijakaa vzr.
je, wanatumia kifungu gani cha sheria?
Kwa Kujiamini kabisa ( kama ilivyo Kawaida yangu ) GENTAMYCINE nasisitiza kuwa Usiku huu huu nimetoka Msibani kwa Mhanga Mmoja na Kesho nikipata Nauli nitaenda tena kwa Msiba wa Mwingine kwani Askari Maliasili wa Mlandizi na Kibaha ( Mkoani Pwani ) hawana Masihara kwa Wafanyabiashara wa Mkaa wa Magendo na Kuwatumia Madereva Bodaboda wanaobeba Magunia ya Mikaa Mitatu Mitatu na Kuileta Mbezi Louis Shule, Kimara na Goba huku machache wakiyapeleka Tegeta kwa Ndevu.
 
Vijana Wanadondoka huko hakuna mfano. au Hawa Askari Maliasili wa siku hizi wamepitia na Kozi ya Shabaha kwa Makomandoo Wetu au hapana kwani unaambiwa Wakiziinua Mtu utaona Pikipiki inaanguka kule, Mkaa Kwingine na Dereva nae Kwingine huku Kichwa kikipasuka au Utumbo wake Kutusalimia tunaowahi / Kuwasalimia wanaowahi Kuokoa.
Najiuliza kwanini imekuwa kama Vita,sababu ninachojua Mimi au Kwa mtazamo wangu isingepaswa kutumika nguvu kubwa sana,kwasababu Jambo rahisi ni kuwekwa kizuizi njiani na kuwakamata kistaarabu Tu,lakini ninachokiona sasa ni kama uhasama uliopitiliza
 
Huenda kuna jinsi wakishachomoka huko ndani wakifika huku barabarani huwezi watofautisha na wachuuzi wa halali. kwahiyo ni kuwawahi huko huko.
 
Juzi kilinuka haswa ,tukashidwa kupita morogoro road,risasi kama tupo Somalia kumbe ni mlandizi
Siku hiyo ndiyo aliuwawa huyu niliyetoka Kumzika Jioni hii ya Leo ambaye Utumbo wake ulimwagika kabisa nje.

Kuna Mwingine Kauwawa Jana na kama Kesho nikipata Nauli nitaenda Kumzika ili nijue kama huyu nae Utumbo wake nae Ulitusalimia ( Ulitoka Nje ) au pengine wa safari hii Kolomero lake ndiyo limetoka.

Askari Maliasili wa Mlandizi na Kibaha ( Mkoa wa Pwani ) najua mpo Kazini ila fanyeni taratibu basi sawa?

Ila na nyie Madereva Bodaboda mnaobeba hiyo Mikaa tutashindwa sasa Kuwatetea kwani GENTAMYCINE nimeambiwa kuwa mmeshaonywa mno kuwa msiingie katika hayo Mapori na Misitu kwa Shughuli zenu za Kimagendo za Kukata Mikaa hamsikii tu.

Hamuogopi hivi mnavyopukutishwa?
 
Kuna vitu vimebaki kama kanuni na daima watu hawawezi kuviacha leo hii hata gesi iuzwe elfu tano bado kuna watu wengi tu wataendelea kupikia mkaa.
ila kuua watu hovyo nako haijakaa vzr.
je, wanatumia kifungu gani cha sheria?
Fujo zinatokea ,na polisi nao waliumizwa,ila kutumiaa risasi za Moto halikua Jambo zuri,sio la kufumbia macho
 
Back
Top Bottom