HEBU CHEKA UNENEPE!
Binti mmoja wa kitanzania alikuwa anasomea masomo ya kisayansi huko China muda wa miaka 20!
Alipofuzu na akaweza kugundua dawa ya kutozeeka, akawatumia wazazi wake kichupa cha dawa hiyo, wanywe tone moja moja wasizeeke!!
Baada ya miaka 10, akarudi Tanzania. akamkuta mama yake kawa binti, huku kabeba kitoto cha kiume mgongoni. Akafurahi sana kumkuta mama yake kawa binti!
Akamuuliza mama yake "baba yuko wapi"?
Mama akajibu "mwanangu, baba yako alipoona nimekunywa dawa, nimekuwa binti, yeye akanywa kichupa chote! Ndio huyu niliyembeba mgongoni!!.
Binti akazimia pale pale...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]