Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Dakika 10 zilizopita nimepiga simu polisi nikawaambia kuna watu 130 ambao siwafahamu wananifuata...
Polisi akaniambia uko wapi tutume msaada
Nikawajibu ni huku instagram
Ni wachochezi?
Basi polisi watawafuata hata huko Instagram kwa makosa ya kimtandao.
 
Na jumapili Madenge amekaa barazani anajisomea kwa ajili ya mtihani watakoufanya jumatatu. Baba yake akaingia;

Baba ; Hakikisha kwamba unafaulu mtihani wa kesho, usipofaulu sahau kuwa mimi ni baba yako.
Madenge; Sawa baba nitajitahidi

Kesho mchana Madende anarudi kutoka shuleni;

Baba; Mwanangu umefaulu mtihani?
Madenge; Samahani kwani wewe ni nani? nimekusahau
 
Jana nilikodi taxi kwenda town nikiwa najua kabisa kwamba sina hata shilingi mfukoni. Taxi niliyopanda ilikuwa na abiria mwingine ambaye ni polisi. Tulipofika karibu na town tukakutana na foleni hivyo dereva akapunguza mwendo. Kuona hivyo nikachomoka fasta na kuanza kukimbia.
Yule abiria mwenzangu Polisi naye akatoka akaanza kunikimbiza huku akifoka simama au nikusambaratishe ubongo. Nilikimbia kama mita kumi nikaona nitafumuliwa bure nikasimama na kunyoosha mikono juu. Yule polisi aliponifikia akaninong'oneza "ENDELEA KUKIMBIA MIMI MWENYEWE SINA NAULI"
 
Juzi nilienda kwenye mkutano wa injili, wakati nasikiliza mahubiri jamaa moja akitokea nyuma akaja kwangu akanishika bega akasema "utatembea", mi nikampuuza nikaendelea kusikiliza mahubiri. Mkutano ulipoisha kucheki mfuko wa nyuma wallet yangu haipo. Ikabidi nitembee kwa miguu toka Mwenge hadi Mbagala...!
 
POWERFULL QUOTE OF THE DAY
"Wakati mwingine hautapewa nafasi lazima uitafute mwenyewe"
- Ziane Ndolla -
Ziane Ndolla ni nani? Huyu ni kondakta wa mabasi ya UDA. Sasa rudia na uisome upya......
 
Aaah hii sasa haiwezekani wakenya wanatutafuta ubaya eti wanasambaza khabari Dr luis shika ni wa kwao.
Na wamchukue tu wakamuoneshe majumba ya lang'ata huenda akayapenda akanunua.Jamani mkulu si alisema akihamia Dom jumba jeupe atalipiga mnada?Mnunuzi kishapatikana tunachelewa nini tumuoneshe aanze kuhamia taratibu taratibu akianza na sandals
 
Pilli alikuwa anamnyonyesha mwanaye. Rafiki ake Kipenzi (Halima) alikuwa amekaa pembeni anaangalia mtoto anavyonyonya.....
Halima akasema,
"kananyonya kama babake"
...Sasa hivi tunajaza PF3 hapa kituo cha Polisi, Kuelekea Hospitali..
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Siku zote ukweli unauma
 
Mkimuona ROMA popote alipo mwambieni huu ndio muda muafaka wa kwenda ZIMBABWE[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Haya wadada wa kibongo changamkieni fursa, maana mke wa mugabe alivyo mbaya kataka kuhongwa nchi[emoji23] [emoji23] nahisi mkienda nyiw Mugabe atawahonga Afrika nzima[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 

Giggy money akitoa remix ya wimbo wake asimkose kumweka huyu kwenye video[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…