Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

[emoji115] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
huyu ndo yule muhuni aliyekufa na maviagra juzijuzi hapa au mimi ndo sijaelewa
 
Nimefika muhimbili nikakuta watu kibao kwenye foleni.....nikapokea simu nikaongea kwa sauti kubwa "Ndio mweshimiwa Rais ndio tumefika hapa bado atujapata huduma tumekaa kwenye mabenchi"" manesi waliposikia wamenikimbilia kama sita sasa hivi ndio namalizia vipimo...mmoja akaniuliza mh. Rais ni nani yako nikamjibu "Rais wa kamisheni ya ngumi Tanzania Emmanuel Mlundwa ni shemeji yangu amemuoa dada yangu....sasa hivi wote wameninunia
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] du hatari
 
Mwaka 1978 timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars kulikuwa kuna mchezaji anaitwa Otieno Mboo.
walifanikiwa kufika Fainali ila huyo mchezaji aliumia mechi ya Nusu fainali,
Magazeti ya Kenya yaliandika vichwa vya habari "WAKENYA KUCHEZA BILA MBOO", Raisi akazuia magazeti yote na kusema warekebishe hiyo sentensi....
Walibadilisha na kesho yake kuandika "WAKENYA KUCHEZA MBOO NJE"
Siku ya mechi Wanawake walifurika Uwanjani
 
Mshkaji nimempigia simu inaita wimbo wa gigy money nikamuuliza huu wimbo umeweka weye au haya mambo ya mtandao?
Akanijibu ni yeye kaweka tena anaupenda sana basi kwa unyonge nikamshauri abadilishe pale penye papa iimbe tigo cha ajabu kakata simu na kila nikipiga inaiita tu nadhani analifanyia kazi.
 
Katikati ya usiku nakatiza kitaa mara paap mbwa kama nane hivi wakaniibukia kwa mbele wanabweka si mchezo mara nikakumbuka mbinu ya mzee wa lugumi Dr Shika basi nikapeleka mikono yote penye makende huku nikijiamini. Duh hapa nakatiza mtaa wa tatu nina boxer tu sina jeans wala tshirt sijui mbwa wa kienyeji hawaheshimu sheria ya kushika korodani!
 
Sikujua kama mabinti wa kitanga wataalam hivi.
Wapendwa siku mbili zilizopita nilikwenda Tanga kutembea, kufika kule si nikachepuka[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Unaambiwa wakati naoga nimewekewa maji ya kuoga mixer viungo kibao.
Siku ya tatu leo sijaingia nyumbani maana nanukia pilau[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Kuanzia juzi sijatoka nyumbani kwa sababu jirani yangu kagombana na mke wake kisa alifumaniwa na mchepuko. Nikasikia mke akimwambia mumewe ili kukukomesha na mimi natembea na jirani zangu wooote.
Nahisi zamu yangu imekaribia bado nasubiria..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…