Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

*Jana Mtoto wa Dada yangu aliniuliza swali la kizushi, Eti Mjomba ukichanganya OMO na FOMA unaweza kupata povu??*
*Nikamjibu, Lazima upate kwa kuwa zote ni sabuni za unga.*
*Kisha nikamwambia,Siku nyingine usiwe unauliza maswali ya kipumbavu*.[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
*Akaniambia majibu yako ndio yakipumbavu. Utapataje povu bila kuweka na maji?*
*Tangu Jana najiuliza nimekosaje swali kizembe?*
*sasa namtafutia sababu afanye kosa nimtie bakora za maana kwa kunivunjia heshima.*[emoji3][emoji3]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nimeamka alfajiri nifanye jogging kidogo nikakumbuka maandiko ya biblia MITHALI 28:1 (waovu hukimbia hata wasipokimbizwa😉 nikaamua kurudi kulala.
Ninayaelewa sana maandiko niko deep kiroho.!!! Za asubuhi
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
ca7a2f3dfb3a71eb8f0f81ef88614e14.jpg

Siku zote nikiicheki muvi hii, kipande hiki ni lazima nikirudie zaidi ya mara tano[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Dumb and Dumber au..!?
 
Nipo kwenye daladala afu pembeni yngu limekaa jamaa...... bila ta aibu linasoma chats zangu zote[emoji35]
Nkaamua kuweka front camera ndo tupo tunaangaliana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
hahahahaha [emoji23][emoji28][emoji23][emoji28][emoji23] ila we jamaa...
 
Kitimoto....

Uipate ile rosti iliyorostiwa mpaka ikageuka kuwa brown, afu pembeni unawekewa pilipili za kukata zile... zimechanganywa zile za kijani na moja inayoelekea kwenye wekundu hiviii. Pemben tena kuna vipande viwili vya ndimu zile kubwakubwa pamoja na chumvi.

Hiyo uipate na dona au ndizi kama 3 hivi zilizokaangwa. Kabla hata hujamaliza kuikagua sahan kama kila ulichoagiza kimefika unaambiwa na mhudumu "naomba unawe".... unamuangalia kidogo usoni then unakinga mikono unanawa, maji vuguvugu saaafi kabisa.

Anamalizaa anaondoka unamsindikiza kidogo na jicho la kiwizi then unairudia sahan yako. Unapiga one touch moja unakamata kipande cha kitimoto kilicholowa rosti zito unakitupia mdomoni na kabla hujatafuna sana unang'ata na kipande cha pili pili. Then baada ya hapo unachukua kipande cha ndimu na kuanza kukamulia taratiiibu kwenye rosti yako huku ukiiangalia kwa madaha beer yako iliyopo pembeni na imefungwa tishu kwa juu.....


......Itaendelea[emoji39]
 
Japan Airport wameweka kioo kubwa ukisimama mbele yake inataja jina lako na nchi unayo elekea.

Mpemba mmoja alisimama mbele ya kioo akaambiwa jina lake ni Awadhi Mkufu Mbaruku na ndege yake yaelekea Zanzibar.

Awadhi alishangaa na kioo na akataka kuhakikisha kuwa ni kweli. Akaenda kuvua koti akavaa kanzu, kofia na miwani. Akarudi tena mbele ya kioo na akaambiwa tena kuwa jina lake ni Awadhi Mkufu Mbaruku na ndege yake yaelekea Zanzibar.

Awadhi akaenda tena kuvua kanzu zawadi alizokuwa amemnunulia mkewe. Akavaa night dress, akatia rangi ya mdomo na akatafuna ubani na kulegeze mwili. Akarudi tena kwenye hicho kioo na akaambiwa

"Jina lako Awadhi Mkufu Mbaruku na ndege yako ishakuacha kwa ukhanithi wako!"

- kwa hisani ya jf
 
Nipo kwenye Daladala hapa, naona kuna abiria mwenzangu anasoma meseji zangu.

Nimeongeza size ya maneno halafu nimeandika,
"BABU HUYU NYOKA NILIYEMBEBA ANASUMBUA AU NIMFUNGULIE?".

Naona abiria mwenzangu anapiga kelele. Nahisi atakuwa amepandisha mashetani.

[emoji1] [emoji1] [emoji1] Sipendagi ujinga.
 
Abiria wakiwa kwenye Daladala mmoja wao aliyekuwa kiti cha nyuma alipumua (Kujamba).

Kwa kuficha aibu wakaanza kunong'ona na baadae kwa sauti kubwa wakisema;

Wabongo: Mzungu kajamba, mzungu kajamba. Ushuzi wa mzungu unanuka.... (Wakidhani mzungu hajui Kiswahili)

Mzungu: (Alikuwa amekaa kiti cha mbele akageuka nyuma ghafla na kusema..) Pumbavu zenu imetoka huko huko nyuma.

Abiria wote kimya....
 
Back
Top Bottom