Kama una umbo kubwa, jifunze kuwa mtulivu

Kama una umbo kubwa, jifunze kuwa mtulivu

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
First time.....
Huyu jamaa alikuwa anavuka barabara mitaa flani kwenye alama za "zebra", sasa gari hazikia zimesimama uzuri mara ghafla yeye akajiona ana haraaaaka akawa anavuka huku anakimbia.
Basi si akajikwaa mazee, msela alianguka kama gunia...😂

Second time.....
Huyu jamaa alikuwa bonge, sasa tupo ndani ya bus tunatokea huku tunaenda jijini Dodoma.
Sasa lile bus lilikuwa lina vidada vidogodogo kibao aiseee, mshkaji kwa mbwembwe mara ainuke mara akae, mara akaanza kutoa pc kwenye kibegi juu ya keria wakati bus linatembea mwendo uliochangamka.
Ghafla dereva akakanyaga break ghafla kitu kilishuka kama kilivyo🤣 akaanguka makalio hadi suruali ikabast..😜 mama mmoja akampa kikoi ajihifadhi.

Third time.........
Kuna kibonge mmoja halafu kijeba hapa kitaa, huyu jamaa ni mtu wa kwenye shughuli tu na milo ya kusaza.
Sasa kuna siku alikuja kwenye sherehe fulani mtaani kwetu hapa, akafukua ubeche wa maana then ghafla watoto wakaangusha hema lililokuwa limekinga raia kwa kivuli, sasa wakati kila mmoja anatoka akimbie huyu biggie akashindwa kunyanyuka kwa shibe ile..😝 aiseee ilikuwa fedhea sana kwake na familia yake alooooo.

Wakuu, hatukatai kunenepa lakini jitahidini msinenepe sana.😜
 
20240102_081212.jpg

Picha ambayo wat vibonge wanapaswa kuiona, nyama nyingi skeleton ile ile 😂
 
Back
Top Bottom