Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Rafiki yangu alipata eneo la nusu heka, aliamua kujenga nyumba ya nyuma ya vyumba vitatu na kimoja ni en-suite. Kwa kweli sikumuelewa, ingawa vyumba viwili aliwapa dada na kaka wa kazi na ensuite aliiweka kwaajili ya wageni.
Uchaguzi uliopita baba yake alikua mmoja wa wazee wa chama kimoja. Walizunguka na mgombea wao wa u Rais mikoani. Kwakua Chama si Chama tawala, kila msaada unahitajika katika Chama. Walipofika mkoa anaoishi rafiki yangu mzee alikwenda na wenzake watano kuishi pale kwa siku tatu.
Wakati huo huo mke wake alikua amejifungua na mama mkwe pamoja na mashemeji walikuwepo. Ile nyumba ya nyuma ilimsaidia kwa kiasi kikubwa.
Kama una uwezo nyumba ya nyuma ni muhimu.