Kinyonyoke
JF-Expert Member
- Oct 4, 2016
- 3,498
- 13,138
Leo kutakukuwa na game ya kukata na wembe kati ya watetezi wa nchi dhidi ya wageni Zesco United pale katika dimba la mkapa.
Young Africans ndio timu pekee inayowakilisha nchi katika michuano hii mikubwa kabisa barani Africa hasa baada ya wadau mikia kuangukia pua kwa aibu ya mwaka kwa kusuuziwa rungu na UD Songo jina ambalo ukilitaja kwa shabiki yeyote wa mkia jicho atakalokuangalia kama ingalikuwa ni silaha basi ni AK47.
Kinachonishangaza ni hawa Mashabiki wa MIKIA kupumbazwa na kupofushwa kwa kiwango cha juu na kipigo cha suprise walichokipata dhidi ya watoto wa mujini UD Songo mpaka kufikia hatua ya kukubali kuolewa bila mahari na Zesco United.
Sasa ninyi na mlioamua kuwapa 071... wote mtaabika vibaya mno pale taifa halafu mnanishangaza sana hivi hamjui Dar Es Salaam Young Africans ndio wakombozi wenu?
Njooni kwa wingi mumuone CR7 Molinga straika Mbavu akifanya yake Taifa na mshuhudie namna mme wenu Zesco anavyofanyiwa matusi leo.
Jambo moja la msingi kwanini mnateseka?
Yanga akifungwa au kutolewa katika michuano hii anatua zake Shirikisho hana la kupoteza nyinyi mikia kwani mnashindania kombe gani msimu huu?
😀
#msimuhuumtapatataabusana
#napendasoka
#utaniwajadi
#chiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii