Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

kagombe, Yeah hiki ulichokisema ni sahihi...kina chiddy mapenzi walianzia huko
 
Hiyo ni challange kubwa sana
Nimesoma comment zote kikubwa nilichogundua ambacho inaweza kuwa ni changamoto ni hii kauli kuwa " wew mwenyewe ndo uwe unafanya hyo kazi" yaani isiwe umeajiri mtu. Sasa kwa wanaokaa maofisin na wanamtaji wao watafanyaje
 
Biashara ya kukausha matunda ni nzuri SEMA inategemeana na maeneo pamoja na msimu wenyewe hivyo biashara hii unaweza fanikiwa iwapo utapata eneo zuri na kwa muda ambao unawlkuta kunauhaba wa matunda eneo Hilo hivyo hayo matunda yatakupa faida
 
Sawa! Basi unaish kama malaika wewe[emoji2][emoji2]
Hahaha.....

Mkuu haya mambo yanawezekana, ni kuweka nia thabiti na kupambana tu. na ukipata kuwa na biashara moja inakupa hamasa ya kuwa na biashara nyingine. Safari moja huanzisha nyingine.

Nilianza na banda moja ila nililidizaini kimuonekano mzuri. Navyoanzisha nilikuwa nipo likizo ya kazi ambayo nilikuwa nalipwa take home 500k.

Nilipambana mwenyewe ili nijue muelekeo wa biashara hii ndio nimuweke mtu. Nakumbuka mwisho wa mwezi nilipata kama 900k. Baadae nikamuweka mtu wa kazi mimi nikarudi job, ila kamisheni hakuwa anapata nyingi, alikuwa anapata arround 700k hv. Nikapata wazo la kuacha kazi ya kuajiriwa

Baada ya miezi kadhaa nilifungua goli la pili na nikaacha kazi ya kuajiriwa ili nisimamie mwenyewe na nikaajiri wadada wawili , kila mmoja sehemu yake. Maendeleo nikayaona nikaongeza goli lingine tena

hizo kamisheni zote nilizorusha hapo zote washazitoa sasa, jumla kwa mwezi mzima wa November

tigopesa 717500
m pesa 522,616
Airtel money 302,580
na halopesa 143,825

Jumla ya kamisheni zote kwa goli moja pekee ni 1,686,521
 
Kuna jamii fulani iliwah sikika kuwa kipindi hiki cha Magu hakuna biashara unayomake profit ya 200k!..labda ww unatokea Mars mkuu!hongera zako
Hakuna sehemu kasema profit ya 200K na biashara ya kuuza vitu vya kula ili upate hiyo unahitaji mtaji wa zaidi ya 50mil kumbuka faida yake ni 1000 kwa mfuko au ndoo ya mafuta
Amesema mauzo
 
[emoji16][emoji16][emoji16]SEMA ladha huwa inapotea ukisema unaunda juice unakuaga Kama umesaga mswaki wa mtii
Kuna mama hapa moro ana hotel na maeka mengi ya maembe..huwa anakausha maembe then kipindi cha kiangzi anaanza kusaga juice ya embe..ila huwa mbayaaa!ladhaless! Ila anauza coz anauzia wasafiri hasa wa dar-dom!
 
Mzunguko mtu mkuu, tena hapo nilikuwaga wateja wa voda nawakataa wanaoutuma mbali. Ila mwezi huu sichague muamala yesterday night niliacha above hizo figure na hata tigo ziko over 500k karibu katika ofisi zangu zote. Tunapeana hamasa ili muamasike na mchukue hatua.View attachment 1248914
Mkuu umeelezea biashara hii kule mwanzo na kuweka attachment ya karatasi ya kuandikwa kwa mkono. Zile namba ni hela ya mtaji au ndio faida kwa mwezi. Naomba unifafanulie, nimehamasika sana na wewe.
 
Hio hela 1M anaingiza kwa muda gani, mwezi au siku? Fafanua tuelewe ambao hatuifahamu hio biashara.
mchawi location mkuu, mimi kuna naemfahamu anaingiza tigopesa pekee hadi M, na yupo kwenye banda tu
 
Back
Top Bottom