Kama unajijua hauko vizuri Kichwani usipende sana kuvalia Suti kwani unaidhalilisha

Kama unajijua hauko vizuri Kichwani usipende sana kuvalia Suti kwani unaidhalilisha

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Lijitu zima kabisa linatoka kwake Mkewe na Watoto wake wanamuona kabisa jinsi alivyounyuka / alivyopendeza na Vazi lenye ' heshima ' kubwa duniani na nahisi hata huko Mbinguni pia la ' Suti ' halafu anatuaminisha kwa ' ujumbe ' wake ambao pengine alikuwa nao mwezi mzima halafu hapo hapo hata Saa 24 hazijapia ' Jitu ' hilo hilo hata ' aibu ' halina linakuja kutuomba radhi kwa ' ujumbe ' wake wa Kitango Pori ( Uwongo ) huku ' likiwa ' limevaa ' Suti ' nyingine.

Ombi kama unajijua hauna ' akili ' sawa sawa acha kulidhalilisha ' Vazi ' linaloheshimika la Suti. Halafu tujitahidi pia na kunyoa ndevu zetu au kuzifanyia ' ukarabati ' kidogo ili ziendane na ' hadhi ' zetu.

Naomba niishie hapa tafadhali.

Nawasilisha.
 
Nikinyoa fresh tu na ndevu zikakaa sawa si ntakuwa vzr kichwani!!
 
Hayo ni Moja kati ya mapungufu ya mwanadamu, Mungu ameclick kitufe wamepoteana, wameona waombe radhi kupunguza pressure ya baadae
 
Kumbe suti ni vazi la heshima sana? Sijui kwanini waheshimiwa sana Yesu na Muhammad hawakuliendekeza....

Anyways... maadam linavaliwa na watu wenye heshima zao usukumani kama mzee wa kipande cha Dar na mzee wa kuombewa... mi acha niendelee kutinga matisheti na majinsi ili nisifanane nao. Siku maalum ntakuwa natinga kanzu kama waheshimiwa viongozi wa kiroho...
 
Hayo ni Moja kati ya mapungufu ya mwanadamu, Mungu ameclick kitufe wamepoteana, wameona waombe radhi kupunguza pressure ya baadae

Basi bora hata hayo yangefanyika huku akiwa kavalia Bukta tu au Kaptura tungejua moja ila kinachoniuma kavaa ' Vazi ' la ' Suti ' ambalo Mimi tokea nazaliwa miongo mitatu na miaka kadhaa nimelikuta bado likiwa na ' hadhi ' yake duniani.
 
😀😀😀😀😀😀😀 Jamaa alitaka kumvisha paka kengele, matokeo yake kaishia kudhalilika!...

Watu wanalidhalilisha sana Vazi lenye ' hadhi ' yake duniani la Suti. Inakera na inaudhi mno!
 
yule kaniudhi sana. wakuelewa watuelewe hali ni mbaya na dira kiuchumi ni mbaya sana.
 
No anti kutoka juu, happy ndipo ninashindwa kuelewa thamani ya elimuvya wasomi wetu kama hawawezi kusimamia wananachokiamini.
Prof ssingekosa mkate wa kula kama angejiuzuru kutetea alichotamka

Dada yangu mbona uandishi wako wa leo una makosa makosa mengi na kama vile huyu siyo Sky Eclat ninayemfahamu Mimi? Vipi ID yako imekuwa hacked Dada? au ndiyo umetoka ' usingizini ' sasa hivi baada ya safari ndefu ya ' Kibaiolojia ' kutoka kwa Shemela letu la ukweli Mumeo?
 
Lijitu zima kabisa linatoka kwake Mkewe na Watoto wake wanamuona kabisa jinsi alivyounyuka / alivyopendeza na Vazi lenye ' heshima ' kubwa duniani na nahisi hata huko Mbinguni pia la ' Suti ' halafu anatuaminisha kwa ' ujumbe ' wake ambao pengine alikuwa nao mwezi mzima halafu hapo hapo hata Saa 24 hazijapia ' Jitu ' hilo hilo hata ' aibu ' halina linakuja kutuomba radhi kwa ' ujumbe ' wake wa Kitango Pori ( Uwongo ) huku ' likiwa ' limevaa ' Suti ' nyingine.

Ombi kama unajijua hauna ' akili ' sawa sawa acha kulidhalilisha ' Vazi ' linaloheshimika la Suti. Halafu tujitahidi pia na kunyoa ndevu zetu au kuzifanyia ' ukarabati ' kidogo ili ziendane na ' hadhi ' zetu.

Naomba niishie hapa tafadhali.

Nawasilisha.
Ha ha ha,, kichwa cha "jitu" kwenye paji la uso kuna doa jeusi.
 
Dada yangu mbona uandishi wako wa leo una makosa makosa mengi na kama vile huyu siyo Sky Eclat ninayemfahamu Mimi? Vipi ID yako imekuwa hacked Dada? au ndiyo umetoka ' usingizini ' sasa hivi baada ya safari ndefu ya ' Kibaiolojia ' kutoka kwa Shemela letu la ukweli Mumeo?
Nimerekebisha jana Asprin ameniletea simu mpya zawadi ya Easter. Inaanza kuzoea Kiswahili
 
Kwa muonekano ni muumini mzuri wa dini .

Hakuna ' Muumin ' mzuri wa Dini aliye ' bogus ' wa Kiwango kile. Na Mimi ' Kilio ' changu ni kutuvalia ' Suti ' leo kisha kutuaminisha jambo fulani halafu hata Saa 24 hazijapita unakuja tena na ' Suti ' nyingine kutuomba radhi na ' midevu ' iliyosimama vibaya utafikiri mchicha mbichi.
 
Back
Top Bottom