Kama unampango wa kujenga chukua huu ushauri

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
21,600
Reaction score
35,158
Kama una uwezo hakikisha umewekeza kwenye haya maeneo.

1. Chimba kisima uwe una uhakika wa maji.

2. Funga umeme wa solar uwe na uhakika wa umeme na sio huu wa TANESCO unaokatika katika kila saa.

Ukiweza wekeza hayo maeneo mawili maisha yako yatakua na amani.

NB: TANESCO wamenikatia umeme chakula kikiwa jikoni na jiko linatumia umeme nikajikuta nawaza hivyo.
 
Ushauri Mzuri ila inahitaji uwe na Mzigo wa Kutosha.

-Kuchimba kisima chenye urefu wa mita 100 na kuendelea lazima uwe na atleast 8m kwa mfuko.
-Kupata umeme mwingi wa solar nayo atleast uwe na 3m.(Backup kubwa za Ritar , Panel Nzuri Mono za Sundar ,atleast ukiwa na 600N ,1000W Pannel na Inverter ya 1000W si mbaya)
 
Mkuu niconection tu yupo mtu anakuchimbia kisima kwa million 2 na maji unayapata hyo 8 m ni ya wale wa machine kawachimbia watu wengi sana wanaenjoy tu full kumwaga maji yasiyo na bill unafunga waterpumb ya 1.5horse power
 
Sasa mfano Kwa majiko ya umeme na fridge plus Tv ukiachana na taa inahitajika kama bei gani?
 
Ndio anachimba local na kira akifika tabaka fulan la udongo anapumb maji yanatoka nje anaendelea kuongeza kina had apate mkondo mkali wa maji na yakiyo clear
Huyu atakuwa Wa kuweka ring bila shaka tofauti ns huyo anaechimba kwa 8 million aliesema mdau King Kong III ambae kimsingi gharama ni kuchimba, mabomba pamoja na "water quality testing" toka ofisi ya bonde

BTW, anapatikana wapi kwa sie wa uchumi wa Mtanzania mnyonge anatufaa
 
1. Panda Miti Mizuri kuzunguka nyumba,
2. Chimba chemba/Shimo refu la Choo,
3. Usjinge katikati ya Kiwanja,
4. Usibanie Material ya ujenzi,
5. Usitumie material duni hasa katika kupaua,
6. Usimwamini fundi, na yeyote katika hio safari, fuatilia kila kitu,
7. Usifanye makosa kwenye milango(imara na mizuri),
8. Usijenge kwa Mawazo eti utajenga vizuri baadae,
9. Vyumba vikubwa ni bora zaidi ya vidogo vingi,
10. Usifanye Choo na Bafu kua vyakumalizia bajeti,
11. Weka mfumo wa Maji kila Unapohisi patakua na uhitaji hata kama huna uhakika wa Maji kipindi unajenga,
12. Kua na mfumo mzuri wa majitaka, taka za nje na za ndani,
13. Usikose eneo hata dogo la kupumzika na michezo kwa watoto,
14. Kujenga Kuna hitaji mda na hatua, usikimbize nyumba isimame haraka hata kama Pesa inaruhusu,
15. Mwisho, uoto mzuri(bustani, maua, Nyasi fupi n.k) kuzunguka nyumba utakufanya ufurahie Makazi yako.
 
Huduma yake ni ya uhakika kawachimbia maboss wengi hapa mbeya anaemfahamu Kisangani yule mwenye anapangisha mabenk nyumba zake yeye ndo anamchimbiaga zile bank zinatumia maji ya mfumo huo kuanzia Kisangani ya Soweto walipopanga bima ,kabwe nmb ya mwanjelwa ,century plaza city pub
 
Mikoani anaenda?
 
Mkuu niconection tu yupo mtu anakuchimbia kisima kwa million 2 na maji unayapata hyo 8 m ni ya wale wa machine kawachimbia watu wengi sana wanaenjoy tu full kumwaga maji yasiyo na bill unafunga waterpumb ya 1.5horse power
Lakini si inasemwa kwamba gharama huoengezeka kutegemea na umbali maji yalipo?(sina uhakika sana na hili)

Namaanisha hicho kiasi cha pesa hapo,yupo atakaechimba kwa mill 8 yupo wa 13mill still yupo atakaechimba kwa 4mill.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…