Kama unao mtaji wa kuanzisha kilimo_biashara ila huna msimamizi/patner sahihi mimi nipo tayari, tuunganishe nguvu tusonge mbele.

Kama unao mtaji wa kuanzisha kilimo_biashara ila huna msimamizi/patner sahihi mimi nipo tayari, tuunganishe nguvu tusonge mbele.

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,922
Reaction score
3,559
Habari za jioni wakuu,
Mimi naamini katika kilimo katika kuufikia uhuru wa kipato. Nimekuwa na ndoto ya kuwa miongoni mwa wakulima mwenye mafanikio makubwa.

Changamoto pekee inayonikabili mpaka naandika uzi huu ni kutokuwa na mtaji wa kuanzisha kilimo chenye tija (ekari nyingi angalau kuanzia 20+) hivyo mchango wangu utakuwa ni muda, nguvu, maarifa na uaminifu katika mradi.

Naamini wapo wenye nia kama yangu, wenye kuamini katika kilimo kama mimi na wenye mtaji wa kutosha kuanzisha kilimo ila hawana muda wala watu sahihi wa kukisimamia. Mimi ni mtu sahihi kwakuwa ninakipenda kilimo. Sasa basi kama tunavyojua Mungu hawezi kukupa kila kitu ili unachokosa ukipate kwa wenzako, mimi muda wa kutosha ninao kuanzia mwanzo wa mchakato hadi mwisho.

Nipo Dar, nipo tayari kwenda mkoa wowote kulingana na mahitaji ya kilimo husika.

Makubaliano na mambo mengine mengi muhimu tutayajadili kwa kadri Mungu atakavyotubariki.

Kwa aliye tayari tuwasiliane tafadhali.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Nimependa ulivyojieleza na nikuhakikishie Mungu atatenda sawa na haja ya moyo wako.
Hata mimi nnahitaji partner ila tayari ninae mwaka huu ngoja nimsome kama yupo vizuri akinichanganya naachana nae tu.
Nashukuru mkuu kwa kunipa moyo.
Nami nikutakie kila la kheri, Mungu awasimamie mtimize na ikiwezekana mpitilize malengo yenu.
 
Mkuu hujaeleza ni kilimo cha mazao gani?
Mkuu nimekuwa too general kwakuwa sina kinachonifanya niwe specific, let say ningekuwa na eneo lililoko bondeni pengine ningesema linafaa kwa kilimo cha zao fulani.

Hivyo basi kilimo chochote kile ambacho kitahitaji very close supervision kama mahindi, vitunguu, mpunga, nk nk na sio mihogo au nanasi.

Ni matumaini yangu utakuwa umenielewa mkuu.
 
Ooh nmekusoma mkuu.
 
Na sense njaa kali sana ya mafanikio kwenye bandiko lako Mkuu...wanasema wenyewe kwamba what you think you become.. Hopefully utapata mshirika kibiashara soon.. Kila la heri
 
Na sense njaa kali sana ya mafanikio kwenye bandiko lako Mkuu...wanasema wenyewe kwamba what you think you become.. Hopefully utapata mshirika kibiashara soon.. Kila la heri
Hakika mkuu, ni wazo linalonipa wakati mgumu sana, na njia pekee ni kulitekeleza tu ndio maana nikaamua kuanzisha huu uzi kama njia mojawapo ya kulifikia lengo.
 
umewah jishughulisha na kilimo chchte before!
Ndio mkuu, ilikuwa ni msimu wa 2003/4 mkoani Iringa.
Nililima kienyeji kwakuwa kipindi kile nilikuwa na umri mdogo pia na mtaji mdogo sana 150, 000 ila kwakuwa nimeanza kukifikiria mda mrefu niliamua kwenda kijijini na kukomaa japo matokeo hayakuwa mazuri.
Nililima maharage, karanga na alizeti
 
sawa..kwa jinsi nilivyo na uzoefu na kilimo angalia hizo eka..ni nyingi sana...!na vile uzoefu unao mdogo mnaweza kujikuta mmerudi kwenye zero!kila la heri!
 
Vp hauna mpango na kilimo cha cash crops?
Sijawahi kukifikiria ila ikitokea mwenye mtaji yuko interested nacho niko tayari kuambatana nae kwakuwa lengo kuu ni kuufikia uhuru wa kipato.
 
sawa..kwa jinsi nilivyo na uzoefu na kilimo angalia hizo eka..ni nyingi sana...!na vile uzoefu unao mdogo mnaweza kujikuta mmerudi kwenye zero!kila la heri!
Nashukuru kwa mtazamo wako mkuu, naamini kupitia ushauri wa wataalamu wa kilimo pamoja na uzoefu wa watu kama ninyi safari haitakuwa ngumu sana.
Changamoto za hapa na pale zipo kila mahala cha msingi ni kuzijua na kuzitatua.
 
Back
Top Bottom