Kama unaogopa hasara, baki na hela zako

Kama unaogopa hasara, baki na hela zako

Void ab initio

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2015
Posts
5,720
Reaction score
5,659
Sikia.... BAKI NA HELA ZAKO

Mzee Mengi alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Lete Raha vile vile. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk.

Akaachana nayo. Afu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.

Hivi unadhani Novida imeenda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je?

Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition.

Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa. Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Juzi tu Landmark Hotel ikawa Hostel.

Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo. Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 8 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo.

Hakuna biashara isiyolipa. Ila kuna akili zisizo za kibiashara ambazo lazima kuzibadili zijue biashara faida na hasara ni kawaida kabisa. Wanasema SOMETIMES YOU WIN AND SOMETIMES YOU LEARN.

Sasa wewe hutaki kulearn utafikaje kwenye mafanikio kibiashara?

Trump mwenyewe alifilisika kabisa. NIL. Zero. Rock bottom. Licha ya kuanza kwa mtaji mkubwa.

If you're afraid to lose money NEVER INVEST. Baki na hela zako.
 
Yaani kwa maelezo yako yalivyojitoshereza nahakika utakuwa umetugusa wengi.

Nakupa hongera sana kwa uzi mzuri.

Wataalau wanasema kitu chochote unapokianza lazima ukipe muda wa mjaribio/probation period na mara nyingi ni kati ya miezi mitatu hadi sita ndo utakuwa na uhakika wa mafanikio yake kwa maana ya walau kuona mwangaza wa unakokwenda.

Na ndo maana hata makazin waajiri hutoa probation period ya miezi mitatu au sita ili wewe pamoja na wao mutathimin kama kweli you are the right candidate for the company/post or vise versa..

Mimi nimeanza biashara ya ku process na kusambaza viungo vya chai vya asili (Organic Spice Herbal Tea) na bahati nzuri sana nina ujuzi wa muda mrefu na mambo ya usambazaji na uuzaji so wakati tunaanza brand yetu kwakweli tumegawa pakti nyingi sana mpaka mwenzangu akawa analalamika kwanini nagawa sana hahahahaha lakini hakujua kuwa hii ni bidhaa mpya na haijulikani.

So, lazima ufanye sampling kwa wadau/wateja ili waitumie, waitathimini na kuielewa, na hata baadhi ya tulio waachia kwa maana ya kuwakopesha ili baadae watulipe nao walitudhurmu na mpaka leo tunadai na labda hawatatulipa lakin kibiashara tayari sisi ni faida maana yule tuliyemwachia dukani katusaidia kutangaza brand yetu na leo ninaandika hapa tunapata oda nyingi tena kwa simu na wengine wanakuja wenyewe kiwandani mpaka walalamika tunapochelewesha kuwapelekea. Na toka tuanze ndo tunaenda mwezi wa nne sasa.

So, kama mwanzisha uzi alivyosisitiza tena kwa mifano mizuri, nadhani ndugu zanguni tusiogope kupoteza maana ni shemeu ya kujifunza na hakuna short cut kwenye hilo.

Cha msingi weka mikakati tu ya namna utaanzaje biashara yako na mteja wako ni wa aina gani, usipoteze muda kwa kudeal na kundi ambalo haliendani na bidhaa yako maana hakuna bidhaa ya kila mmoja, kila bidhaa ina watu/wateja wake.

Hongera sana Void ab initio!
 
Wataalamu wanasema kitu chochote unapokianza lazima ukipe muda wa mjaribio/probation period na mara nyingi ni kati ya miezi mitatu hadi sita ndo utakuwa na uhakika wa mafanikio yake kwa maana ya walau kuona mwangaza wa unakokwenda.
Na ndo maana hata makazin waajiri hutoa probation period ya miezi mitatu au sita ili wewe pamoja na wao mutathimin kama kweli you are the right candidate for the company/post or vise versa..

Mimi nimeanza biashara ya ku process na kusambaza viungo vya chai vya asili (Organic Spice Herbal Tea) na bahati nzuri sana nina ujuzi wa muda mrefu na mambo ya usambazaji na uuzaji so wakati tunaanza brand yetu kwakweli tumegawa pakti nyingi sana mpaka mwenzangu akawa analalamika kwanini nagawa sana hahahahaha lakini hakujua kuwa hii ni bidhaa mpya na haijulikani so lazima ufanye sampling kwa wadau/wateja ili waitumie, waitathimini na kuielewa, na hata baadhi ya tulio waachia kwa maana ya kuwakopesha ili baadae watulipe nao walitudhurmu na mpaka leo tunadai na labda hawatatulipa lakin kibiashara tayari sisi ni faida maana yule tuliyemwachia dukani katusaidia kutangaza brand yetu na leo ninaandika hapa tunapata oda nyingi tena kwa simu na wengine wanakuja wenyewe kiwandani mpaka walalamika tunapochelewesha kuwapelekea. Na toka tuanze ndo tunaenda mwezi wa nne sasa.

So, kama mwanzisha uzi alivyosisitiza tena kwa mifano mizuri, nadhani ndugu zanguni tusiogope kupoteza maana ni shemeu ya kujifunza na hakuna short cut kwenye hilo.

Cha msingi weka mikakati tu ya namna utaanzaje biashara yako na mteja wako ni wa aina gani, usipoteze muda kwa kudeal na kundi ambalo haliendani na bidhaa yako maana hakuna bidhaa ya kila mmoja, kila bidhaa ina watu/wateja wake.

Hongera sana Void ab initio!

Kumbe kuna mambo tunaweza tukaongea kwa pamoja kwa akili nzuri.Ahsante mtoa mada kwa somo zuri,shukrani wachangiaji kwa kukiri mapungufu yetu.

Tusaidiane kuelimisha na kuhamasisha watoto na wadogo zetu kusoma mada hizi tuwatengenzee kesho njema kwao.Hawajui kuwa kuanguka ni sehemu muhimu ya darasa.Hongera.
 
Nakumbuka cousin wangu alipata mafao ya kujitoa baada ya ku-move kutoka kampuni moja kwenda nyingine, akapata 25mil tsh. Sasa akawa anajiuliza afanye nini na hizo hela? Me nikamwambia tafuta kitu cha kufanya maana hizo hela ukikaa nazo utakula tu! Tafuta hata taksi basi au daladala, analalamika hizo biashara ni headache!!! Nikabaki nashangaa, wapi duniani kuna biashara isiyo na headches?

Ndio nature ya biashara, mafanikio yako yanakuja baada ya kuzishinda hizo headache. Hata machangudoa wana headache zao za kutosha tu. After one year, jamaa kabakia na milioni kama 8 hivi, alichofanya hajui.
 
Exactly..watu wanasahau kuwa it's not what you do ndio kitakutajirisha ila ni the process katika kukifanya Mara kwa Mara bila kukata tamaa
Mjasiriamali ni Marufuku kukata tamaa.
 
Mtoa mada umesema ukweli na umetoa somo. maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge.

Hapo unajifunza kama ni baridi au moto. sio mtu unaambiwa tu tikiti linalipa unakurupuka kisha ukipata hasara unakimbia na kulaumu. unapopata hasara kuna kimeenda wrong ambacho ni cha kusahihisha. ingekuwa matikiti ni hasara tu bila shaka yangepotea na tusingeyaona tena!

Muhimu kila kitu kina hasara na kina faida pia kina hasara muhimu ni kujifunza.

Asante mkuu.

Kuna mijitu inafikiri always negatively na hupenda kukatisha tamaa.

Hivi karibuni nimeanza kilimo cha bustani kule Ruvu. nikaanza na kilimo cha mahindi ya kuchoma. mtaalamu mmoja akaniambia ukilima heka moja kitaalamu unaweza kupata milioni 2.5 hadi 3. Niliishia kupata laki 8 lakini ukweli nilijifunza sana kwani kuna makaosa na changamoto. ni kweli kabisa inawezekana kupata 2.5 hadi 3 mil kwa eka lakini with knowlege and hard work.

Nimevutika sana kuwa kilimo kinalipa saanaaa lakini ukiwa na nia ya dhati. wengi wanabeza lakini mafaniko hayaji haraka. hata miongoni mwa familia watakubeza lakini unakaza buti.

With time and hard work unaweza kuzungumzia mamilioni kwenye kilimo na ajira binafsi na si katika hii mishahara!
 
Back
Top Bottom