Kila uchaguzi mkuu, CCM imekuwa ikitumia propaganda za "divide and rule" (wagawe uwatawale) ambayo ni mbinu iliyokuwa ikitumiwa na WAKOLONI ili kututawala, kwani walijua kwamba umoja wetu ndio nguvu yetu dhidi ya udhalimu wao.
CCM wanatumia mbinu hii chafu kujenga hoja kwamba vyama vya upinzani vinahatarisha (au vitahatarisha) amani iwapo vitapewa fursa ya kuiongoza nchi hii. CCM inajua kutawala, si kuongoza.
Kwani ni NANI kati ya viongozi wa kambi ya upinzani aliyetamka kwamba AMANI ITATOWEKA iwapo vyama hivyo vitashinda Uchaguzi Mkuu?
Nyota mnayakumbuka yaliyotokea 1995, wakati ITV iliporusha matangazo yakionesha picha za mauaji ya kutisha yaliyotokea Burundi na Rwanda, huku wakitangaza kwamba vyama vya upinzani vya nchi hizo ndivyo vilivyohatarisha amani nchini humo. Huo ulikuwa uongo. Yale yalikuwa mauaji yaliyosababishwa na chuki za kikabila. Hivi kweli sisi tuna hulka za ubaguzi wa aina hiyo, mpaka kumwona jirani yako, Mmasai, Mmakonde, Mmakua, Mwera, Mnyakyusa, Muha, Mhaya, Mjita, na kadhalika, kuwa adui?
Hatuna ukabila wala udini Tanzania. Hizi propaganda chafu ZIACHWE!
Mfunyukuzi, unajidhalilisha na unawadhalilisha wana-CCM wenzako! Sikutarajia haya kutoka kwa mtu ninayemheshimu kama wewe. Usinipe sababu ya KUKUDHARAU na KUKUTENGA!
-> Mwana wa Haki