Kama unapenda amani chagua CCM

Kama unapenda amani chagua CCM

Watanzania tuna misingi ya amani tangu zama hizo, uhuru tuliuupata kwa mazungumzo ya mezani, ccm tafuteni vigezo vingine, maendeleo hatuyaoni ni bora mkoloni alijali maslahi ya watanzania, mnapoongelea mshikamano mna maanisha mshikamano miongoni mwa mafisadi? watanzania wekeni mbele maslahi ya taifa.
 
Na Usipochagua CCM, basi CCM watachukua madaraka kwa nguvu ya dola!

Kila uchaguzi mkuu, CCM imekuwa ikitumia propaganda za "divide and rule" (wagawe uwatawale) ambayo ni mbinu iliyokuwa ikitumiwa na WAKOLONI ili kututawala, kwani walijua kwamba umoja wetu ndio nguvu yetu dhidi ya udhalimu wao.

CCM wanatumia mbinu hii chafu kujenga hoja kwamba vyama vya upinzani vinahatarisha (au vitahatarisha) amani iwapo vitapewa fursa ya kuiongoza nchi hii. CCM inajua kutawala, si kuongoza.

Kwani ni NANI kati ya viongozi wa kambi ya upinzani aliyetamka kwamba AMANI ITATOWEKA iwapo vyama hivyo vitashinda Uchaguzi Mkuu?

Nyota mnayakumbuka yaliyotokea 1995, wakati ITV iliporusha matangazo yakionesha picha za mauaji ya kutisha yaliyotokea Burundi na Rwanda, huku wakitangaza kwamba vyama vya upinzani vya nchi hizo ndivyo vilivyohatarisha amani nchini humo. Huo ulikuwa uongo. Yale yalikuwa mauaji yaliyosababishwa na chuki za kikabila. Hivi kweli sisi tuna hulka za ubaguzi wa aina hiyo, mpaka kumwona jirani yako, Mmasai, Mmakonde, Mmakua, Mwera, Mnyakyusa, Muha, Mhaya, Mjita, na kadhalika, kuwa adui?

Hatuna ukabila wala udini Tanzania. Hizi propaganda chafu ZIACHWE!

Mfunyukuzi, unajidhalilisha na unawadhalilisha wana-CCM wenzako! Sikutarajia haya kutoka kwa mtu ninayemheshimu kama wewe. Usinipe sababu ya KUKUDHARAU na KUKUTENGA!

-> Mwana wa Haki
 
Tangu lini TZ imekuwa na amani??? Au mwandishi alikuwa anamaanisha 'utulivu'. Nchi itakuwaje na amani ambapo asilimia zaidi ya sabini wananchi wake ni maskini wa kutupwa. Hawana uwezo wa kula chakula cha uhakika, kupeleka watoto wao shuleni, kupata huduma za afya nzuri na kwa gharama ndogo, n.k. Hata huo utulivu ni hulka ya watanzania tu wala siyo kazi ya chama cha mujahidin - ccm, kama kinavyotamba bila soni.

Hiki chama kimeishiwa mbinu za kuwadanganya waTZ sasa kimeanza kutisha wananchi kwa hoja ya amani. Lakini waTZ sasa hawadanganyiki. Chadema lazima ichukue nchi na kwa taarifa yao ccm kama wanadhani watatumia dola kuiba au kufanya hujuma yoyote kwenye uchaguzi basi wajue kwamba hata dola yenyewe imechoka. Inachohitaji dola ni Rais mwenye uchungu nao ambaye kwa sasa ni Dr. Slaa. Hakika nwaka hiu, ccm imeshikwa pabaya. Ukimwino kikwete akijieleza unahisi kachoka kabisa. Yeye ameendelea na kastaili kake kakutembea na lundo la ahadi za abunuwasi. Kampeni zake zimekosa mvuto mpaka inachosha.
 
Kila uchaguzi mkuu, CCM imekuwa ikitumia propaganda za "divide and rule" (wagawe uwatawale) ambayo ni mbinu iliyokuwa ikitumiwa na WAKOLONI ili kututawala, kwani walijua kwamba umoja wetu ndio nguvu yetu dhidi ya udhalimu wao.

CCM wanatumia mbinu hii chafu kujenga hoja kwamba vyama vya upinzani vinahatarisha (au vitahatarisha) amani iwapo vitapewa fursa ya kuiongoza nchi hii. CCM inajua kutawala, si kuongoza.

Kwani ni NANI kati ya viongozi wa kambi ya upinzani aliyetamka kwamba AMANI ITATOWEKA iwapo vyama hivyo vitashinda Uchaguzi Mkuu?

Nyota mnayakumbuka yaliyotokea 1995, wakati ITV iliporusha matangazo yakionesha picha za mauaji ya kutisha yaliyotokea Burundi na Rwanda, huku wakitangaza kwamba vyama vya upinzani vya nchi hizo ndivyo vilivyohatarisha amani nchini humo. Huo ulikuwa uongo. Yale yalikuwa mauaji yaliyosababishwa na chuki za kikabila. Hivi kweli sisi tuna hulka za ubaguzi wa aina hiyo, mpaka kumwona jirani yako, Mmasai, Mmakonde, Mmakua, Mwera, Mnyakyusa, Muha, Mhaya, Mjita, na kadhalika, kuwa adui?

Hatuna ukabila wala udini Tanzania. Hizi propaganda chafu ZIACHWE!

Mfunyukuzi, unajidhalilisha na unawadhalilisha wana-CCM wenzako! Sikutarajia haya kutoka kwa mtu ninayemheshimu kama wewe. Usinipe sababu ya KUKUDHARAU na KUKUTENGA!

-> Mwana wa Haki
Mkuu mie sio mwana chama wa CCM ni kuwa nimekutana na hiyo habari picha sehemu nikaona vi vibaya kuishare hapa thus why sikuweka any comment kwenye mtundiko...twataka mabadiliko sasa
 
Period! Utadumishaje kitu ambacho hakipo? lazima kwanza amani ijengwe halafu ndio inaweza kudumishwa. Sasa hao SISIEM hata hawajui kama Tanzania hakuna amani kweli WANATUFAA HAWA JAMANI? KWELI WAKO SERIOUS?
 
eti mfunyukuzi nae ni mccm. Haingii akilini hata kidogo
 
Hiki ni kichekesho kingine... Zamani kabla hatujaelimika ilikuwa rahisi kututisha na amani, labda we mzushi uliyepost huu upuuzi hujui maana ya amani. Ukimkuta mzazi mwenye mtoto ana utapiamlo kwa sababu ya sera mbovu za ccm hawezi kukwambia nchi ina amani. Pia amani haipo kwa watanzania wenzetu wanaokufa kwa ukimwi kila siku wakati ARV zao zinauzwa kwa magendo Zambia na Malawi kutokana na sera mbovu na usimamizi mbovu wa rasirimali za nchi wa ccm. Vilevile kwa wanaokufa kwa magonjwa yanayotibika, ajali za wanaopanda malori kwenda badala ya mabasi au wanaokufa kwa ajali za mabasi yenye chesesi za malori kutokana na usimamizi mbovu wa sheria wa serikali ya ccm na Kikwete pia ni uvunjaji wa amani na damu zinamwagika. Nyie wenye upeo mdogo wa kufikiri mkachagua ccm mjue kuwa hapa Tz damu zinamwagika kila siku kutokana na sera mbovu za ccm. Sio damu ikimwagika vitani ndo ukosefu wa amani, damu ya mtanzania ni damu tu, haijalishi imemwagika vitani au kwa ARV zake kuuzwa malawi na watendaji wa Kikwete. Ndio maana ili tuwe na Everlasting peace tumchague DK Slaa aje kurekebisha uozo wote wa serikali ya Kikwete nchi iwe na discipline na damu za watanzania zisiendelee kumwagika.
 
Hii ni kauli ya vitisho ya CCM, kwamba tusipowachagua kutakucha?
 
CCM wakitumia hao askari kuwaua raia wake kwa vile hawajawachgua ; sasa wakisha waua watatawala paka? Na hizo kodi za kuendesha hiyo dola zitatoka wapi kama raia ndio wameuawa? Acheni ujinga mlipewa miaka zaidi ya hamsini kutawala na mmeshindwa ondokeni kwa amani muwapishe wenzenu nao wafanye vile wanavyowaahidi wapiga kura!
 
Tanzania bila CCM inawezekana
Ni kheri uwe kwenye machafuko na maisha mazuri bali kuwa na amani alafu washindia mlo mmoja hatiame utaja kufa kwa maradhi ambayo ni sawa tuu na anaekufa kwa mtutu wa bunduki vyote ni vifo.
Kinana amekuwa kimya sana au ndo mgomo baridi
 
Tanzania hakuna amani, labda wananchi wake tu ni watulivu. Watu wanaweza kuwa wametulia lakini haina maana kwamba wana amani.
 
Nchi yang Tanzania naipenda sana kuliko chama chochote cha siasa. Vyama vitakufa Tanzania itabaki
 
Ninapenda sana amani,lkn niliwahi kuchagua CCM ckupata amani niliyotarajia!so this tym nitachagua CHADEMA nipate ladha tofauti
 
Duh hii imetulia hata rangi zapendeza kabisa yaani
 
Back
Top Bottom