Kama unatafuta kazi suluhisho lako lipo hapa-ba recruitment agency



good news

mimi nimewatumia cv yangu,wamenitumia application form nimejaza na nimeshawatumia,wamenipigia simu jana wameniambia tukutane kesho saa nne pale holiday inn,swimming pool side,ila aliyenipigia mimi ni mwanamke ana jina la kikenya wangui janice,naamini mambo yataenda vizuri ila hiyo elf hamsini naipigia hesabu.
 
wizi mtupu, hivi huu utapeli utaisha LINII?
 

mkuu kuwa makini inawezekana na ww ukawa mtu wa 290 kutapeliwa na hata wliokuita sasa kuwa nao makin wanaweza wakakutapeli!
 
Na hawa nao wasipotoa maelezo ya kina kujieleza wanatakiwa kula BAN! Tusiintatein wevi humu wakuu, ama vp wakuu?
 
Biashara ni ushindani lakini kwa nini usitume CV kwa agents ambao wana weka CV yako ktk data bank zao bila gharama zo zote.
Ushauri wa bure: usilipe pesa hata senti tano mpaka upate kazi. Na kama kulipa wambie wakachukue kutoka katika mshahara wako kupitia kwa mwajiri wako mpya. La itakula kwako.
 

mi kama wapo tayari wanitafutie kazi then nikishaajiriwa wachukue hata mshahara wote.

Naona kama haijakaa sawa hii kitu.
 
website for reference? geographical address?
 

Mkuu nasubiri jibu, utakuja uniambie.......kuna kitu kinaendelea hapo na nahisi hili ni genge la matapeli
Kwanini hawana permanent offices mpaka sasa na umesema wewe ni mtu wa 290.....inamaana wameshapata application fee pamoja na commission yakutosha kulipia pango pamoja na gharama nyinginezo. Lakini interview zao wanafanyia mahotelini tena kwa kumfuata mteja...mara blue pearl, mara holiday inn. Matapeli wengi ndio zao wakitaka kukuingiza kweenye trap, ili waweze kukupumbaza kwamba wao sio watu wa kubabaisha na wamwshazoea maisha fulani classic.

Wewe test kwa kuwaambia huna hata shilingi......ila ukisha sign contract ndio utawalipa hiyo pesa. Hawatakubali kwa sababu watajua hakuna kitu watapata na interest yao ni hiyo 50,000.
 

Bado sijashawishika na ninahisi wewe ni sehemu ya hao jamaa na unajaribu ku-win confidence za jamaa walioshtukia mchezo.
 

mhhhh !!!
 
Jamani kuweni waangalifu oohhhh! Hiyo 50,000/= ungeipeleka kwenye magazeti hakika mwisho wake ungepata kazi msikimbilie kutuma pesa ovyo ovyo hao ni matapeli tena wa mchana kweupeeeeeeee!!!!! Wamekosa kazi nao wameamua kuanzisha ajira yao mpya Chunga sana!!!!!!!
 

Eti kuna Mkenya humo ndani? Kwishney! Kama hamuwajui Wakenya poleni sana wale wako dakika kadhaa mbele katika mambo ya utapeli hatuwawezi! Wangu utaibiwa wewe!!!!!!!
 

Thanks for your ushauri, hata mimi nimeshtukia wanaweza wakawa matapeli tu!!!
 

Unaweza kuwa ndo wewe tapeli mwenyewe ama mwenzao........... Kwa nini wasikubaliane na hao employers wawalipe kama ilivyo kwa recruiters wengine badala ya kuchukuwa hela kwa employee? Halafu kwa nini wanachukua hela kabla? Maana hata kwa recruiters wengine wanalipwa baada ya kupata candidate anayetakiwa na employer.

Nasema huu ni utapeli na hainiingii akilini kamwe.
 
wadu msidanganyane na msitumie uzoefu wenu wa kuingizwa mjini kuwadanganya watu na kuwakatisha tamaa watu wanaotafuta kazi,

ba recruitment agency ni wa kweli na wanafanya kazi zao kwa uhakika na haraka,mimi nimfano wa watu waliohudumiwa nao na nimepata kazi kwa haraka kuliko nilivyodhani,

binafsi nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita nimefanya vitample hapa na pale bila uhakika na wakati wote huo nilikuwa nafanya application kila recruitment agency unayoijua hapa dar-es-salaam kuna application yangu na hata wafanyakazi wa hizo agency wengi wao ni marafiki zangu lakini nataka niwaambie ukweli hao wanaosema wanatoa kazi bure ni uongo wanachukua rushwa kwa baadhi ya watu na ndio wanawapatia kazi tena rushwa yenyewe ni zaidi ya hiyo elfu hamsini ya ba ra,mimi nimewahi toa hela kwenye hizo recruitment agency zaidi ya laki saba lakini sijawahi pata kazi kila mara wanakupigia simu njoo kwa interview wanakuuliza maswali lakini no job; no what; wanakuwambia watakupigia hawakupigii ng'oo.

ba ra ni kampuni ya muda mrefu na ni ya kimataifa sema walikuwa wanatumia jina lingine na walikuwa wanafanya biashara nyingine wamebadilisha jina mwezi uliopita na wapo hapa dar Mbezi beach ila hawajafungua ofisi rasmi hili ni jambo la kawaida ulimwenguni kote watu wanataka contact na efficiency sio address zisizona mafanikio,wamebadilisha jina mwezi uliopita kutokana na matatizo ya share zao.

ukweli ndio huo ba ra wamenisaidia kwa shilingi elfu hamsini tuu; nimepata kazi lem and len tabata na nitaanza january 2 na watachukua 20% ya mshahara wangu mmoja tuu wa kwanza,kama unataka ushauri zaidi njoo pale tabata january nione mimi finance manager mpya nitakuhakikishia jinsi gani ba ra wanaaminika.

acheni kusikiliza maneno ya wafa maji wewe k=unaetafuta kazi ndio unajua adha ya kukaa bila kazi wengi hapa jf ni mabwanyenye wako ofisini hawana kazi wanachat tuu na kukatisha watu tamaa.elfu hamsini sio kitu ni hela ndogo sana we have to take risk hata kama ingekuwa laki tano,
 
No comenti,
Wajinga ndio waliwa.
By ze wei nimependa kareji yako, najua mida hii mtakuwa mmeisha make kiasi cha kutosha.
 
No comenti,
Wajinga ndio waliwa.
By ze wei nimependa kareji yako, najua mida hii mtakuwa mmeisha make kiasi cha kutosha.


HAKUNA WAJINGA WALA WALIWAO HAPA KAMA MTU ANATAFUTA KAZI NA KWELI AMESHAONJA ADHA YA KUKAA BILA KAZI KWA MUDA HAWEZI JIULIZA MARA MBILI WHEN OPPORTUNITY RISE HII NI CHANCE HAWA JAMAA WANA DATABASE YA WATANZANIA KAMA MIA TATU SASA NA BADO WATU WENGI WANAMIMINIKA KKWAO NA WANAFANIKIWA WEWE KAMA UNASHIDA YA KAZI ELF HAMSIMNI SIO KITU

ILA KAMA UNASIKILIZA MANENO YA WAUNGWANA WA HUMU WALIOKAA KWENYE MAOFISI MAKUBWA NA KUCHAT THE WHOLE DAY HAYA KAZI KWENU.NAOMBA NISISITIZE MIMI SIO MFANYAKAZI WA BA RA MIM NI MTEJA WAO TUU NA NIMEPATA KAZI HARAKA SANA WITHIN A WEEK,HATA WIKI HAIJAISHA KWELI KWANGU NIMUUJIZA
TUMENI CV patakazi1981@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…