Don't pay for getting a job!!!those guys are a hoax! You should send your CV to reputable recruiters who charge their clients and not u the candidate! Such as radar, e goli, epic etc
samahani mbona wewe unaonekana kuitetea kwa uchungu na kujua details nyingi za hii kampuni kuliko wenye kampuni waliotuma post? tetea ya huyo himo one haina uchungu kama wewe.
Anyways kuna walakini katika hili clarification zitolewe na muwe na ofisi
No more comment from me coz' i was abt to question about the same thing!!!!! by the way, why should i pay money in advance while am looking for money?! If they're charging 20% for my first salary, then am ready to be charged up to 50% of my firts three salalries BUT AM NOT READY FOR THAT TZS 50,000!
fungua ubongo wako fikiria zaidi ndugu, elf hamsini sio kitu kabisa sisi walevi tunasema ni round moja tuu imekwisha hata michemsho na supu za mikia na ulimi hazijaja mezani .
Mimi nimepata kazi through this ba ra na nitamshauri mutu yeyote ajiunge nao atafanikiwa,acha mawazo ya kufikirika utazeeka ukisaga soli kwenye recruitment agencies zinazojiita za bure kumbe wanataka rushwa yako ili wakupe kazi panua mawazo na jiulize kati ya watu unaowajua i wangapi wanatafuta kazi na ni wangapi hawana kazi na ni wangapi wana kazi na ni wangapi wamepata kazi kutokana na recruitment agency unayoijua,then ujiulize ni kwa nini na ni hatua gani muhimu ya kuichukua.
njaa tu!amaridong,congs. Mbona mi nilituma cv zaidi ya wiki imepita wapo kimya?
TaaHIRA;;njaa tu!
Hii ni scam bila mashaka. Reply nyingi saana zinafana namna ya uandishi wake. Karibu zote na hata za waliopata kazi zipo bolded. Si hivyo tu, wengi kati ya watafuta kazi kasoro mmoja tu wamejoin November na December. Kwahiyo wanajua wanachotaka. People watch out the step of this group
Ndugu wadau na watanzania wote kwa ujumla,napenda kuwatangazia kuwa mkombozi wa ajira sasa amekuja Tanzania.Kampuni mpya ya kutafuta kazi imeanzishwa hapa Dar-es-Salaam,inaitwa BA Recruitment Agency.Japo kutakuwa na gharama kiasi kwa ajili ya kuchangia huduma hii,napenda kuwahakikishia kuwa tuna uzoefu wa muda mrefu na tutajitahidi kukufikia na kukusaidia kwa wakati,Kazi tulizonazo kwa sasa ni kama ifuatavyo;
-Wahasibu
-Masoko
-Maafisa/Mameneja Utumishi
-Wanasheria
-Madereva
-Maafisa Uhusiano
-Masecretari
-Watafsiri
-Waalimu
Kazi hizi zipo hapa Dar-Es-Salaam na nyingine ziko nje ya Dar kama Morogoro,Arusha,Manyara na Mbeya.
Tafadhali wahi sasa tuma CV yako patakazi1981@gmail.com ,tutawasiliana na wewe mara moja kukujulisha gharama za huduma na taratibu nyingine.
AHSANTENI SANA NA KARIBUNI WOTE.
naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru sana waanzilishi na wamiliki wa jamii forum,wana jamii forum na wadau wote.
mimi ni mmoja wa wamiliki na wa ba ra na niliamua kuweka tangazo letu hapa kama wiki sasa imepita na kwa kweli tumekuwa tukifuatilia michango ya watu juu ya kazi na kampuni yetu hapa kwa kipindi chote ,inafurahisha sana na ninapenda kuwapongeza sana kwa michango mizuri inayojenga na kusaidia sana.nawashukuru jf kwa kuliacha tangazo letu hapa kwa muda wote bila hata malipo,ukweli ni kuwa watu zaidi ya hamsini wametutumia cv zao hivi karibuni na ukiwauliza wamesoma wapi kuhusu sisi wanasema wameona tangazo letu jamii forum,ahsanteni sana.
la muhimu ambalo nimeamua kuja tena kuwaeleza waungwana ni kusisitiza kuwa kampuni yetu ipo ,inafanya kazi kwa bidii na kwa haraka sana,gharama zetu ziko wazi kabisa na hakuna rushwa wala dhuluma,na watu wote tuliopokea fedha zao kwa kipindi cha mwezi mzima sasa wamepata kazi na wengi wengine wako kwenye pending list na watapata kazi hivi karibuni.
ninapoandika ujumbe huu wapo watanzania 24 kwenye makampuni mbali mbali dsm,morogoro na arusha wakifanya interview zao leo tuu na wamepata nafasi hiyo kutoka hapa kwetu.
kuna watanzania 32 wako kazini sasa na wanafurahia kazi zao wakiwa wamesaidiwa na kampuni yetu.wako watanzania 52 watakaoanza kazi tarehe 2 /1/ 2011 ambao ni juhudi zetu na wote hao wamesaidiwa na bara
with due respect i berg to present
""lets all make the tanzania we dream of""
Mambo mawili hapa.
Inwezekana ni kweli mnasaidia lakini Marekerting Officer wenu ni bomu,kama manfanya hivyo biashara ambayo kwa kiasi kikubwa ni msaada mkubvwa kwa watanzania kjwa nini mjifiche? Hili kwa nini linashinda watu,onesha jina lako,kampuni yako,namba za simu,nk.
Wewe unadhani utafanya biashara(kama ni halali) kwa kificho namna hii,Mfano mimi natumia ID ya jina langu na wakati wa kujisajili nilieleza sababu,iwapo naitaji kitu nataja jina langu,kampuni yangu,simu yangu nk.
Hii inasaidia kuondoa utata
"Hivyo hata kama nyie siyo matapeli lakini mnatumia njia za kitapeli kufanya kazi halali"
Tofauti na hilo,fafanua jina lako,cheo,namba ya simu,kampuni zilizowahi kunufaika na kupelekwa wafanyakazi nk
Byabato
Kiresua unakichaa lazima,hiyo si ni mistake ya kawaida tuu au una bifu na hawa jamaa nini aua unawajua?tueleze mkuu maana unahasira sana wkila mbuzi anakula usawa wa kamba yake ndugu yangu au?
Kampuni mpya, uzoefu wa muda mrefu!?Ndugu wadau na watanzania wote kwa ujumla,napenda kuwatangazia kuwa mkombozi wa ajira sasa amekuja Tanzania.Kampuni mpya ya kutafuta kazi imeanzishwa hapa Dar-es-Salaam,inaitwa BA Recruitment Agency.Japo kutakuwa na gharama kiasi kwa ajili ya kuchangia huduma hii,napenda kuwahakikishia kuwa tuna uzoefu wa muda mrefu na tutajitahidi kukufikia na kukusaidia kwa wakati...
Kuweni makini wadau,ulizeni wale jamaa wa Erolink wanaofanya kazi za customer care voda.
MATANGAZO YA KAZI YANATOKA KILA SIKU, USIWE MVIVU KUWEKA KWA MUUZA MAGAZETI TSH 20,000 YA KUSOMA THE GUARDIAN NA DAILY NEWS KILA SIKU, UTABAHATISHA TU SIKU MOJA,NA PIA KUWA MVUMILIVU NA INTERVIEW RESULTS MAANA NDO UNAJENGA UWEZO WAKO WA KUJIELEZA. SOMA MAGAZETI HAYO,TUMA MAOMBA HATA MARA 1000,JIANDAE VIZURI KWA INTERVIEW NA IPO SIKU ITAKUWA ZAMU YAKO KUPATA KAZI.
THANKS.