Kama unatafuta nyumba ya kupanga DSM, kuna vitu vya kuzingatia usivichukulie poa!

wee namba moja NO and YES, nakumbuka nilipanga kihonda manyuki moro kwa mama mmoja mstaafu raha sana...nilikuwa nakaa naye, bill zote tuna share. umeme ukiisha ananiambia mwanangu umeme umeisha ulete hela kama huna tafuta siku mbili tatu ulete, tulikuwa wapangaji wawili tu na geti alikuwa ananiachia wazi..mimi peke yangu nilikuwa na usafiri, narudi usiku najua namna ya kufungua geti then nafunga hakuna wa kutoka wala kuingia tena, maji kama kawaida...mwanangu leta hela uliyonayo najua wewe bachela hutumii sana😛. kodi ikikaribia ananikumbusha kama hukumbuki anza kujipanga kodi..siku ikifika mwanangu huna mbona hujaja kuniambia maisha ndivyo yalivyo utapata utaileta tu. Namkumbuka sana yaani. mwengine nilikuta wapangaji wanne na kausafiri kangu hakuwa na shida hata nikirudi saa 5 geti wamefunga nampigia simu anamka anafungua...ila hawa nilikuwa nawahisha kodi😎...msimu wa mvua nilisafiri nikarudi usiku saa nne duuu..naiona nyumba ila siwezi kuifikia maji yameziba njia...nikarudi kwa mtendaji mazimbu road nikapaki usafiri kwa kulipia..nikaenda kwa miguu..viatu mkononi nikaloana hadi kiunoni...tangu hapo kodi ilipoisha nikajiondokea ila hadi kesho tunaheshimiana sana na mwenye nyumba yule😀😀
 
Yote uliyoanisha ni ya msingi sana
Nilipanga sehem jirani akaninyima penzi halafu akaanza kuweka nyimbo za majigambo namna ye na jamaa yake wanapendana dah ilibidi nihame
Alafu usiombee nyimbo iwe Ile Taarabu 🤣🤣🤣🤣 ya Mzee Yusuph

Yarabii iweee Salaamaa!! Salama Usaliminii
Wasipate Yakusemaa Roho zao ziwaumee
Walopaaangaa Tuachanee Roho zaoo Ziwaumee😝😝😝😝🤣🤣😄

Na Mimi yalinikuta mkuu baada ya Kukosa Penzi la demu mmoja wa Kitwangaa toto lilofundwa nikapigiwa huu utenzi
Nyumba za Kupanga hizi Astaghafirulaaah laana tunlaah!!😆😆😆😆😆
 
Kuna watu hawataki kuacha alama ya kujenga nyumba hapa duniani. Nina rafiki mkaka, angeweza kujenga hata nyumba 3 ikiwemo ghorofa.
Ila hataki kusikia neno kujenga! Yeye anapanga nyumba nzuri za bei sehemu nzuri. Akichoka anakaa hotelini ndiyo maisha yake mwenyewe kayachagua.
hao tuko wengi tunasema dunia njia na hatuwezi kujenga njiani,...🤒🤒
 
Nilikua kwenye nyumba ya kupanga, nzuri tu. Tatizo mwenye nyumba akapandisha bei kwa asilimia zaidi ya 25, bila taarifa mapema.

Nikaona sio shida, nikahama mkataba ulivyoisha. Sasa katika harakati za kutafuta nyumba, kuna vitu nimejifunza na vingine nimeshachelewa nimejikuta najuta tayari niko ndani.

Baadhi yake:

1. Usikae na mwenye nyumba.

Nilipokua zamani nilikua sikai na mwenye nyumba. Anakuja mara chache sana. Ila sahivi nimeyatimba.

Hafu mwenye nyumba ana shughuli kila siku, mazingira yapo ovyo wala sio masafi kwasababu yeye tu ana ndugu zaidi ya 8 na watoto, ukijumlisha mnashare uwanja, aisee.

2. Jitahidi msiwe mna-share bili/matumizi ya maji au umeme.

Iwe na wapangaji wenzako au mwenye nyumba, jitahidi sana ulipie bili mwenyewe.

Ikitokea umebanwa sana bdsi angalau muwe wawili mwisho. Sub-meater hazitasaidia kitu. Mtatoa kila mtu 20,000/= ya umeme kwa mwezi wewe unashinda kazini ukirudi unawasha feni tu, kuna sista duu anachemsha maharage kwa presha cooker.

Lazima mtagombana tu.

3. Hakikisha nyumba imekamilika ujenzi, asikudanganye lipia tu namalizia wiki ili kuweka madirisha sijui.

Unavyoenda kukagua eti nyumba haijakamilika choo au dirisha, akasema lipia namalizia mtego huo.

Ukishalipia tu imeisha. Utakuta jikoni hakuna sink, feni ya sebuleni haweki, na ata maji unaweza kuta akachelewa kuyaingiza.

Jitahidi uende nyumba iliokamilika kila kitu.

4. Kama una gari, angalia upatikanaji wa funguo za geti.

Otherwise utajikuta unawahi kurudi kuogopa kufungiwa geti kama mtoto. Zamani nilikua ata saa 8 usiku naweza kutoka sahivi nawahi home saa 4 wasije funga geti. Nishalalamika ila ndio ivo, kila siku ahadi hewa.

5. Zingatia idadi ya wapangaji wenzako.
Kama unaweza, jitahidi wapangaji muwe wachache. Mkiwa kikosi kuna faida na challenge zake. Faida moja wapo unaweza pata mke hapo hapo. Ila hasara unakuta challenge hadi kwenye kamba za kuanika mfano weekend mkifua wengi kwa pamoja, makelele kila mtu akiweka singeli nk.

6. Uliza kuhusu utaratibu wa bili za maji taka, takataka/usafi na ulinzi shirikishi.

Hii michango haiwagi mikubwa ila nayo ni kero.
Kuna hii ya maji taka kuyatoa kwasababu shimo limejaa, michango ya wale wazoa takataka na ulinxi shirikishi.

7. Zingatia msimu wa mvua kunapitika? Mafuriko na nyumba kuvuja?

Kuna nyumba msimu wa mvua hazifikiki sio kwa gari wala kutembea, pia kuna uwezekano mvua ikinyesha nyumba ikawa inavuja.

8. Kelele/mishemishe za majirani.

Unaweza ukawa umeenda kucheki nyumba ukakuta pako cool, kumbe jioni kuna bar uchwara inapiga music usiku kucha.

Au ukakuta weekend au jioni ni nyumba za ibada wanatumia maspika ww unasema unapumzika wao wakakiwasha.

Edit:

9. Uchumi ukiruhusu tafuta chumba chenye choo ndani.

Kama uchumia na mazingira yanaruhusu, epuka nyumba zenye vyoo vya kushare. Kuna watu ustaarabu mdogo sana .

Kwa sasa nimeyatimba, ila kutaka kuforce kukaa Makongo Juu kumeniponza. Nikimaliza Kodi yangu naamsha.

Hapo nimekuelewa mkuu
 
Kuna chumba nlipanga aiseee kajukuu ka mwenye nyumba ka kike around 3 yrs kakaweka mazoea ya kunivamia geto kakikuta nakaanga dagaa kanatoka kanamwambia bibi anko anakaanga nyama nataka nyama.basi kiki8va nakapea
Mama mwenye nyumba nyingine akawa na mtindo wa kukaa karibu na mlango wangu nkipika anakuja anasema ana ugali mboga hama nimpee.yaani ni shidaa tupu
 
Nilikua kwenye nyumba ya kupanga, nzuri tu. Tatizo mwenye nyumba akapandisha bei kwa asilimia zaidi ya 25, bila taarifa mapema.

Nikaona sio shida, nikahama mkataba ulivyoisha. Sasa katika harakati za kutafuta nyumba, kuna vitu nimejifunza na vingine nimeshachelewa nimejikuta najuta tayari niko ndani.

Baadhi yake:

1. Usikae na mwenye nyumba.

Nilipokua zamani nilikua sikai na mwenye nyumba. Anakuja mara chache sana. Ila sahivi nimeyatimba.

Hafu mwenye nyumba ana shughuli kila siku, mazingira yapo ovyo wala sio masafi kwasababu yeye tu ana ndugu zaidi ya 8 na watoto, ukijumlisha mnashare uwanja, aisee.

2. Jitahidi msiwe mna-share bili/matumizi ya maji au umeme.

Iwe na wapangaji wenzako au mwenye nyumba, jitahidi sana ulipie bili mwenyewe.

Ikitokea umebanwa sana bdsi angalau muwe wawili mwisho. Sub-meater hazitasaidia kitu. Mtatoa kila mtu 20,000/= ya umeme kwa mwezi wewe unashinda kazini ukirudi unawasha feni tu, kuna sista duu anachemsha maharage kwa presha cooker.

Lazima mtagombana tu.

3. Hakikisha nyumba imekamilika ujenzi, asikudanganye lipia tu namalizia wiki ili kuweka madirisha sijui.

Unavyoenda kukagua eti nyumba haijakamilika choo au dirisha, akasema lipia namalizia mtego huo.

Ukishalipia tu imeisha. Utakuta jikoni hakuna sink, feni ya sebuleni haweki, na ata maji unaweza kuta akachelewa kuyaingiza.

Jitahidi uende nyumba iliokamilika kila kitu.

4. Kama una gari, angalia upatikanaji wa funguo za geti.

Otherwise utajikuta unawahi kurudi kuogopa kufungiwa geti kama mtoto. Zamani nilikua ata saa 8 usiku naweza kutoka sahivi nawahi home saa 4 wasije funga geti. Nishalalamika ila ndio ivo, kila siku ahadi hewa.

5. Zingatia idadi ya wapangaji wenzako.
Kama unaweza, jitahidi wapangaji muwe wachache. Mkiwa kikosi kuna faida na challenge zake. Faida moja wapo unaweza pata mke hapo hapo. Ila hasara unakuta challenge hadi kwenye kamba za kuanika mfano weekend mkifua wengi kwa pamoja, makelele kila mtu akiweka singeli nk.

6. Uliza kuhusu utaratibu wa bili za maji taka, takataka/usafi na ulinzi shirikishi.

Hii michango haiwagi mikubwa ila nayo ni kero.
Kuna hii ya maji taka kuyatoa kwasababu shimo limejaa, michango ya wale wazoa takataka na ulinxi shirikishi.

7. Zingatia msimu wa mvua kunapitika? Mafuriko na nyumba kuvuja?

Kuna nyumba msimu wa mvua hazifikiki sio kwa gari wala kutembea, pia kuna uwezekano mvua ikinyesha nyumba ikawa inavuja.

8. Kelele/mishemishe za majirani.

Unaweza ukawa umeenda kucheki nyumba ukakuta pako cool, kumbe jioni kuna bar uchwara inapiga music usiku kucha.

Au ukakuta weekend au jioni ni nyumba za ibada wanatumia maspika ww unasema unapumzika wao wakakiwasha.

Edit:

9. Uchumi ukiruhusu tafuta chumba chenye choo ndani.

Kama uchumia na mazingira yanaruhusu, epuka nyumba zenye vyoo vya kushare. Kuna watu ustaarabu mdogo sana .

Kwa sasa nimeyatimba, ila kutaka kuforce kukaa Makongo Juu kumeniponza. Nikimaliza Kodi yangu naamsha.
Kuna tatizo gani kuishi na mwenye nyumba?

Nifafanulie mapungufu hayo ili nami nijifunze kitu.

Halafu kufunga mageti mapema ni kero isiyomithilika, kwa nini asichongeshe funguo za geti kila mpangaji akakaa na nakala yake ili kuwe na uhuru wa mtu kurudi muda anaoutaka?
 
Hakuna kitu kinatia hasira kama una jirani ambae kila siku anaingiza wanawake na wanawake wanatoa milio kwa sauti kubwa mida ya kulana. Pia milio ya kitanda, milio ya pwa pwa pwa pwa pwa pwa na milio mingine mbalimbali tena kila siku na ni usiku mzima.
Hahaha
 
Rafiki Mad Max natamani nikuambie njoo upanga nikupangishe kwenye nyumba ya urithi ila naogopa kwakuwa Mimi nipo mbali na hapo ndugu zangu watakusumbua kukudai Kodi na kukukopa kwa kigezo Cha wao ni wenyenyumba pia ,mwisho uje kunichana hapa

Japo hata Mimi nikirudi hatutawezana maana nikiishiwa hela lazima wewe kama mpangaji uwajibije ili baba mjengo nisikae kinyonge
Huna hiyo nyumba upanga acha kutulisha chai mkuu
 
Kuna tatizo gani kuishi na mwenye nyumba?

Nifafanulie mapungufu hayo ili nami nijifunze kitu.

Halafu kufunga mageti mapema ni kero isiyomithilika, kwa nini asichongeshe funguo za geti kila mpangaji akakaa na nakala yake ili kuwe na uhuru wa mtu kurudi muda anaoutaka?
Atakwambia usalama
 
Back
Top Bottom