Kama unatafuta nyumba ya kupanga DSM, kuna vitu vya kuzingatia usivichukulie poa!

Aisee inakera na kuumiza.
 
Mjenge za kwenu na nyie muweke hayo masharti.
Umefikiria kwa akili fupi, nyumba sio gari ndugu, kuwa utaenda nayo popote.
Kama sehemu ya utafutaji wako ipo permanent utakuwa sawa.
Kumbuka wengine ni wafanyakazi kazi wanaweza kuhamishwa kutoka kituo fulani kwenda kitua kingine au mfanyabiashara akahamisha biashara mkoa mwingine.
 
Nunua kiwanja hata hatua 12 kwa 24.ujenge geto janja,acha utumwa,hizo laki sita utafyatua tofali kibao na kigeto ujanja kiko kama castle house full ujanja,hebu hizo posho unganisha ujenge geto ujanja au cheza mchezo wa kazini.
Unafikiri ukijenga ndo Kero zinaisha?....Bora ukipanga ukipata Kero unahama chap, hata kabla ya kumaliza mkataba. Ukijenga ni kama ndoa ya Katoliki.
1. Umeanza ujenzi fresh, je unaijua matumizi ya kiwanja Cha jirani yako? Wanafunga trubali mkesha daily.
2. Mara jirani anakushitaki umehamisha mpaka, Kila siku mnapelekana Kwa mjumbe. Kutokana na hilo bifu mnajikuta hamuongei Wala kusaidiana Kwa shida Wala Raha.
3 Mara kutokea chizi kafunga njia (unakumbuka issue ya Shukuru Kawambwa?)
4. Mara majirani zako washirikina, Kila asubuhi unakuta vichwa vya kuku na damudamu kwenye kibaraza chako.
5. Unataka ufunge maji jirani anakataa mtu asichimbe kwenye eneo lake. Unatafuta njia mbadala Jirani aliekataa usipitishe maji unakuta kaunga tawi kwenye maji Yako.

Bora tuendelee kupanga, tunakuwa na option nyingi nyingi.

Labda ujenge ushuani ambako Kila kitu planned.
 
Wakati Uingereza inaenda kuitawala America walipambana na mengi,kwa taarifa tuu hizi kero za.maisha ndo maisha yenyewe,uwe na Raha katika dunia hii ili iweje,Unaweza ukawa.na majirani wazuri tuu kumbe mke wako kitanda kimoja ndo mwanga mwenyewe anaweza kuwa vizuri kumbe mkweo kila siku anakuwangia,jitahidi sana kuishi maisha yako,hata hao wanaokukera nao pia wanapambana na luku na bili za maji na watoto machixi kila siku. In fact wanga kila Kona wapo hadi Kizmkazi wapo,kulala ikulu kuwaza li nchi lenye wezi kila Kona unafikiri kazi ndogo.
 
Aisee ni kweli mkuu, changamoto
 
Kwenye safari ya maisha kupanga chumba/nyumba ni sehemu ya kujitafuta. Uchumi wako ndo unaamua upange Kimara au Mbezi beach. Mbagala au Makongo.

Nakumbuka mara ya kwanza napanga chumba baada ya chuo, wahuni walinikaribisha kitaa kwa kuniibia kila kitu getto. Ulikuwa ubatizo kwa maji ya moto.
 
Jenga ya kwako hata Chumba kimoja hii itaweka huru
Huyu jamaa anakumbusha, vitu vya kuzingatia, unapohitaji kupanga, mfano kwa wafanyakazi, Unaweza kuwa na nyumba hata nne, ila ukapata uhamisho, kwenda kufanyia kazi mji mwingine.
.
.Hivyo, ukalazika kupanga, kuna jamaa kipindi cha ujenzi wa barabara mwendokasi Ubongo kimara, yeye akiwa mkazi wa mbezi, na anafanya biashara kariakoo, na huko mbezi alikua anaishi nyumba yake mwenyewe, gari lakutembelea alikua nayo, ila alilazimika kupanga nyumba magomeni, kutokana hali ilivyokua.
.
KIpindi kile kutoka kariakoo mpaka mbezi, unakata masaa 7 hadi 8 hivyo kupanga hakuna mwisho.
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…