permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 11,682
- 14,241
Hili somo lina walakini, jambo la kwanza ni kuwa na vipaumbele au tuseme malengo na baada ya hapo ndio utakuwa katika nafasi nzuri ya kuweka mchakato/system au njia ya kufanikisha hayo malengo. Kwa kuongezea pia ni aina ya lengo ulilojiwekea ndilo linalokupa picha utumie mchakato gani ili kufanikisha lengo husika. Kuanza na mchakato ambao hauna lengo ni sawa ni sawa na kuanza safari ambayo hujui unataka kufika wapi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Swali ambalo najua unajiuliza ni je ina maana sihitaji tena kuweka malengo? Je nitayaendeshaje maisha yangu bila ya malengo? Nitajipimaje?
Majibu ni unapaswa kuweka malengo, kwa sababu ndiyo njia ya kukuwezesha kutoka hapo ulipo sasa na kufika mbali zaidi. Lakini ukishaweka malengo yako, kazana zaidi na mchakato unaofanyia kazi kila siku na siyo lengo hilo tu. Ukiweka nguvu zaidi kwenye mchakato, unajiweka kwenye nafasi ya kufikia lengo lolote ulilonalo.
Hapo chini nimekupa mifano ya jinsi ya kutumia mchakato kufikia malengo yako ya 2020.
Asante.Mada nzuri sana.
Ila ni kitu kile kile ispokua mtoa mada ulichokifanya ni kusisitiza hatua za kufikia malengo mtu aliyojiwekea.
Hivo kwanza ni lazima kuweka malengo alafu kukazania michakato ya kufikia malengo
Asante mkuu kwa nyongeza hii.Malengo hayasimami kama malengo, vinginevyo Mtu anakuwa hajajua nini maana ya malengo.
Malengo yanaambatana na mikakati(mchakato), malengo madogo, ya kati na makubwa.
Mtoa maada ameelezea vyema kabisa, Jinsi gani utayafikia malengo kwa kutumia mikakati (mchakato)
Nikiri tu wazi neno malengo haliepukiki hata ndani ya mchakato kuna "vimalengo vidogo vidogo" ambavyo ndo vinaku sharpen, Focus yako.
Malengo na mchakato huwezi kuvitenganisha.
Nadhani mtoa mada kichwa cha mada ungekiita Namna ya kufikia malengo kwa kutumia mchakato sahihi(the art of setting goals).
Sent using Jamii Forums mobile app